SoC03 Tanzania: Katiba Mpya sio 'Tatizo', Viongozi wetu wanapatikanaje?!

Stories of Change - 2023 Competition

Mjukuu wa Hassan-Juma

Senior Member
Dec 3, 2022
109
93
Miongoni mwa udhaifu mkubwa wa mfumo wa demokrasia ni nadharia yake ya 'wengi wape'. Nadharia maarufu ya utawala inayotaka kiongozi achaguliwe na kundi kubwa la watu bila kujali wasifu au uwezo wa watu hao kwenye kuchambua ubora wa kiongozi wanayemtaka.

Viongozi wengi wanaofanikiwa kuingia madarakani hutokana na ushawishi wao kwenye kundi kubwa la wapiga kura na sio ubora wao wa kuongoza. Wapiga kura wachache wenye macho ya kuona udhaifu wa mgombea hawawezi kushinda kwenye sanduku la kura mbele ya wengi waliopewa! Demokrasia haikupi ahadi ya kupata kiongozi bora, isipokuwa inakupa uhakika wa kupata kiongozi anayependwa na watu wengi (kwa sababu zao).

Matokeo yake, takribani mfumo mzima unatawaliwa na viongozi wenye tamaa ya madaraka na sifa duni ambao hupelekea rushwa, kutokuwajibika na ufisadi uliokithiri.

Makala hii itaangazia umuhimu wa kudhibiti demokrasia ya upatikanaji wa viongozi wetu, faida zake na itapendekeza mfumo na mchakato wa kupata viongozi bora.

MIFANO YA MIFUMO YA UPATIKANAJI WA VIONGOZI

China sio taifa la kidemokrasia, lakini muundo wake wa kuchagua na kuteua viongozi ni mojawapo ya mifano bora inayoweza kushuhudiwa. Hapa sikusudii kuzungumza kuhusu udhibiti wa shughuli za kisiasa nchini China, bali namna yao bora ya upatikanaji wa viongozi wa taifa lao.

Siri kubwa ya ukuaji wa haraka wa China ni ubora wa viongozi wake. Viongozi huwa wanateuliwa, kuchambuliwa, kufunzwa na kupimwa utendaji kabla ya kupanda ngazi moja baada ya nyingine ya uongozi. Na kamwe hawapatikani kutokana na umaarufu au ushawishi wao. (Profesa Zhang Weiwei)
MCHAKATO WA UONGOZI - CHINA_014558.jpg

Upande mwingine, kupitia mfumo wa demokrasia, nchi nyingi zilizoendelea zimepiga hatua kubwa ya kimaendeleo. Uwepo wa mifumo imara ya serikali inayotokana na wastani mzuri wa kiwango cha elimu cha raia wake, husaidia kwa kiasi kikubwa kuchagua viongozi bora na kurahisisha mifumo ya utawala na uwajibikaji. Ni sahihi kusema kwamba, miongoni mwa nguzo muhimu za udhibiti wa upatikanaji wa viongozi wao ni uelewa na wastani mkubwa wa elimu wa raia wake.

DEMOKRASIA YA TANZANIA

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, lakini pia mchakato wa kuinua kiwango cha elimu cha watu wake hauwezi kuchukua 'usiku mmoja'. Maana yake ni nini?! Sio sawa kubadili mfumo wa kiutawala kuwa wa Chama kimoja kama China, lakini pia kunakili na kuitumia demokrasia ya magharibi kama ilivyo kwa watanzania ambao kiwango chao cha elimu ni duni na hawana umahiri wa kutathmini ubora wa viongozi, hili nalo ni kosa kubwa!

images.jpeg

Picha: mtandaoni

Utamlaumu kwa lipi mzee Masudi wa Mahenge kwa kuchagua kiongozi mbaya ilhali umempa uhuru wa kupiga kura na wala yeye hafahamu namna ya kutathmini ubora wa kiongozi kutokana na kiwango cha elimu yake?!

Ipo haja ya kutafsiri demokrasia ya upatikanaji wa viongozi ili iendane na hali halisi ya taifa letu. Na kuhakikisha kila zao la mwisho litakalopigiwa kura na wananchi ni zao bora kabisa! Je, nini kifanyike?!

Mfumo mzima wa upatikanaji wa viongozi unapaswa kuboreshwa kwa kuzingatia mambo makuu mawili;

1/. UONGOZI UWE TAALUMA YA LAZIMA

Uongozi unapaswa kuwa taaluma ya lazima na inayothibitishwa na mamlaka. Kwa kuanzia kwenye uwepo wa mifumo na taasisi maalum zinazosimamiwa na mamlaka hiyo za kuibua vipaji nchi nzima na kuviendeleza kwa kuvijengea uwezo na taaluma ya kuongoza. Iwe ni kipaji kilichoendelezwa, au ni msomi wa chuo kikuu na vyuo vya kati n.k, hawa wote ni lazima kabla ya kuingia kwenye uongozi wathibitishwe ubora wao.

Taaluma hii inaweza kutolewa chini ya chombo rasmi kilichoundwa na Kupewa mamlaka kupitia program maalum ya mafunzo ya uongozi yenye mtihani na mafunzo ya vitendo kwa ajili ya kuongeza umahiri na ubobevu wa wahitimu na baada ya hapo watakuwa tayari kuteuliwa au kugombea nafasi tofauti za kisiasa.

2/. KUDHIBITI UWEZO NA NAFASI.

Lengo kubwa hapa ni kufungamanisha ufaulu uliothibitika wa mtaalamu wa uongozi, utendaji wake, nidhamu, maono yake, kujitoa kwake kwa ajili ya taifa, pamoja na elimu yake kwenye nafasi husika anayoteuliwa au kugombea. Mfano, kuwa na wabunge ambao ni wataalamu wa sheria na uchumi, au wakuu wa mikoa na wilaya wenye ufaulu wa juu sana wa mafunzo ya uongozi na waliohudumu kwenye nafasi nyingine zilizothibitisha ubora wao kisiasa, hali kadhalika kwa mawaziri na nafasi nyingine zote.

MAPENDEKEZO YA MCHAKATO WA UONGOZI.jpg

Mambo haya makuu mawili yanakwenda sambamba na uundaji wa chombo huru cha usajili, udhibiti wa nidhamu na ubora wa viongozi chenye mamlaka ya kuadhibu kama ilivyo kwa taaluma zingine, mfano bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) na Baraza la madaktari Tanganyika (MCT).

Taratibu zingine zote za ndani ya chama cha siasa zinapaswa kuwa hatua ya pili baada ya kiongozi kuthibitishwa usajili na uanachama hai ndani ya chombo chenye mamlaka ya kuandaa na kusimamia ubora wa viongozi, na utaratibu huu unaweza kurahisishwa kupitia mifumo ya TEHAMA.

FAIDA ZA KUDHIBITI MCHAKATO WA UPATIKANAJI WA VIONGOZI

1/. Kuondoa wimbi la viongozi-walaghai wa kisiasa. Uwepo wa mikasa ya ubadhirifu wa mali za umma kama ESCROW na RICHMOND ni uthibitisho kwamba viongozi wengi wametanguliza maslahi binafsi mbele kuliko maslahi ya umma. Muundo huu utasaidia kuchuja dhamira za viongozi na kupunguza walafi wa kisiasa.

2/. Kuimarisha usalama wa nchi dhidi ya ujasusi kutoka dola zingine. Uwepo wa mchakato maalum utasaidia kuthibitisha utaifa, uadilifu na usiri wa viongozi kwenye kutunza taarifa za nchi. Pia kudhibiti mianya ya urahisi wa kuwa kiongozi ambayo inaweza kutumiwa na nchi maadui au makundi maovu kupenyeza majasusi ili kupata taarifa za nchi au wananchi na kisha kuzitumia kulidhuru taifa.

3/. Kupata viongozi bora wanaotii sheria. Katiba bora bila viongozi watii wa katiba ni kazi bure. Hata baadhi ya mambo mazuri ya katiba ya sasa hayakufuatwa wakati wa awamu ya tano. Mfano wa mambo yaliyokiukwa ni matumizi nje ya bajeti, kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa n.k. Kama ilivyo muhimu kuwa na katiba nzuri, basi ni muhimu zaidi kuwa na viongozi watii wa katiba, walioandaliwa.

HITIMISHO: Ingawa makala hii imependekeza mfumo wa upatikanaji wa viongozi, bado haifungi uwepo wa mawazo mbadala yanayoweza kuwa bora zaidi.

Mawazo hayo yanaweza kuwa na mapendekezo ya mfumo mwingine mpya au yanaweza kuboresha zaidi mfumo uliopendekezwa, yote hayo ni muhimu ili kufikia lengo mama la makala hii ambalo ni uandaaji wa viongozi kupitia mfumo thabiti, uliodhibitiwa na utakaotupatia viranja bora kwenye safari hii nzuri ya ujenzi wa taifa.

Ahsanteni sana.
 
Miongoni mwa udhaifu mkubwa wa mfumo wa demokrasia ni nadharia yake ya 'wengi wape'. Nadharia maarufu ya utawala inayotaka kiongozi achaguliwe na kundi kubwa la watu bila kujali wasifu au uwezo wa watu hao kwenye kuchambua ubora wa kiongozi wanayemtaka.

Viongozi wengi wanaofanikiwa kuingia madarakani hutokana na ushawishi wao kwenye kundi kubwa la wapiga kura na sio ubora wao wa kuongoza. Wapiga kura wachache wenye macho ya kuona udhaifu wa mgombea hawawezi kushinda kwenye sanduku la kura mbele ya wengi waliopewa! Demokrasia haikupi ahadi ya kupata kiongozi bora, isipokuwa inakupa uhakika wa kupata kiongozi anayependwa na watu wengi (kwa sababu zao).

Matokeo yake, takribani mfumo mzima unatawaliwa na viongozi wenye tamaa ya madaraka na sifa duni ambao hupelekea rushwa, kutokuwajibika na ufisadi uliokithiri.

Makala hii itaangazia umuhimu wa kudhibiti demokrasia ya upatikanaji wa viongozi wetu, faida zake na itapendekeza mfumo na mchakato wa kupata viongozi bora.

MIFANO YA MIFUMO YA UPATIKANAJI WA VIONGOZI

China sio taifa la kidemokrasia, lakini muundo wake wa kuchagua na kuteua viongozi ni mojawapo ya mifano bora inayoweza kushuhudiwa. Hapa sikusudii kuzungumza kuhusu udhibiti wa shughuli za kisiasa nchini China, bali namna yao bora ya upatikanaji wa viongozi wa taifa lao.

Siri kubwa ya ukuaji wa haraka wa China ni ubora wa viongozi wake. Viongozi huwa wanateuliwa, kuchambuliwa, kufunzwa na kupimwa utendaji kabla ya kupanda ngazi moja baada ya nyingine ya uongozi. Na kamwe hawapatikani kutokana na umaarufu au ushawishi wao. (Profesa Zhang Weiwei)
View attachment 2686863

Upande mwingine, kupitia mfumo wa demokrasia, nchi nyingi zilizoendelea zimepiga hatua kubwa ya kimaendeleo. Uwepo wa mifumo imara ya serikali inayotokana na wastani mzuri wa kiwango cha elimu cha raia wake, husaidia kwa kiasi kikubwa kuchagua viongozi bora na kurahisisha mifumo ya utawala na uwajibikaji. Ni sahihi kusema kwamba, miongoni mwa nguzo muhimu za udhibiti wa upatikanaji wa viongozi wao ni uelewa na wastani mkubwa wa elimu wa raia wake.

DEMOKRASIA YA TANZANIA

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, lakini pia mchakato wa kuinua kiwango cha elimu cha watu wake hauwezi kuchukua 'usiku mmoja'. Maana yake ni nini?! Sio sawa kubadili mfumo wa kiutawala kuwa wa Chama kimoja kama China, lakini pia kunakili na kuitumia demokrasia ya magharibi kama ilivyo kwa watanzania ambao kiwango chao cha elimu ni duni na hawana umahiri wa kutathmini ubora wa viongozi, hili nalo ni kosa kubwa!

View attachment 2686864
Picha: mtandaoni

Utamlaumu kwa lipi mzee Masudi wa Mahenge kwa kuchagua kiongozi mbaya ilhali umempa uhuru wa kupiga kura na wala yeye hafahamu namna ya kutathmini ubora wa kiongozi kutokana na kiwango cha elimu yake?!

Ipo haja ya kutafsiri demokrasia ya upatikanaji wa viongozi ili iendane na hali halisi ya taifa letu. Na kuhakikisha kila zao la mwisho litakalopigiwa kura na wananchi ni zao bora kabisa! Je, nini kifanyike?!

Mfumo mzima wa upatikanaji wa viongozi unapaswa kuboreshwa kwa kuzingatia mambo makuu mawili;

1/. UONGOZI UWE TAALUMA YA LAZIMA

Uongozi unapaswa kuwa taaluma ya lazima na inayothibitishwa na mamlaka. Kwa kuanzia kwenye uwepo wa mifumo na taasisi maalum zinazosimamiwa na mamlaka hiyo za kuibua vipaji nchi nzima na kuviendeleza kwa kuvijengea uwezo na taaluma ya kuongoza. Iwe ni kipaji kilichoendelezwa, au ni msomi wa chuo kikuu na vyuo vya kati n.k, hawa wote ni lazima kabla ya kuingia kwenye uongozi wathibitishwe ubora wao.

Taaluma hii inaweza kutolewa chini ya chombo rasmi kilichoundwa na Kupewa mamlaka kupitia program maalum ya mafunzo ya uongozi yenye mtihani na mafunzo ya vitendo kwa ajili ya kuongeza umahiri na ubobevu wa wahitimu na baada ya hapo watakuwa tayari kuteuliwa au kugombea nafasi tofauti za kisiasa.

2/. KUDHIBITI UWEZO NA NAFASI.

Lengo kubwa hapa ni kufungamanisha ufaulu uliothibitika wa mtaalamu wa uongozi, utendaji kazi wake, nidhamu yake, maono yake, kujitoa kwake kwa ajili ya taifa, pamoja na elimu yake kwenye nafasi husika anayoteuliwa au kugombea. Mfano, kuwa na wabunge ambao ni wataalamu wa sheria na uchumi, au wakuu wa mikoa na wilaya wenye ufaulu wa juu sana wa mafunzo ya uongozi na waliohudumu kwenye nafasi nyingine zilizothibitisha ubora wao kisiasa, hali kadhalika kwa mawaziri na nafasi nyingine zote.

View attachment 2686870

Mambo haya makuu mawili yanakwenda sambamba na uundaji wa chombo huru cha usajili, udhibiti wa nidhamu na ubora wa viongozi chenye mamlaka ya kuadhibu kama ilivyo kwa taaluma zingine, mfano bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) na Baraza la madaktari Tanganyika (MCT).

Taratibu zingine zote za ndani ya chama cha siasa zinapaswa kuwa hatua ya pili baada ya kiongozi kuthibitishwa usajili na uanachama hai ndani ya chombo chenye mamlaka ya kuandaa na kusimamia ubora wa viongozi, na utaratibu huu unaweza kurahisishwa kupitia mifumo ya TEHAMA.

FAIDA ZA KUDHIBITI MCHAKATO WA UPATIKANAJI WA VIONGOZI

1/. Kuondoa wimbi la viongozi-walaghai wa kisiasa. Uwepo wa mikasa ya ubadhirifu wa mali za umma kama ESCROW na RICHMOND ni uthibitisho kwamba viongozi wengi wametanguliza maslahi binafsi mbele kuliko maslahi ya umma. Muundo huu utasaidia kuchuja dhamira za viongozi na kupunguza walafi wa kisiasa.

2/. Kuimarisha usalama wa nchi dhidi ya ujasusi kutoka dola zingine. Uwepo wa mchakato maalumu utasaidia kuthibitisha utaifa, uadilifu na usiri wa viongozi kwenye kutunza taarifa za nchi. Pia kudhibiti mianya ya urahisi wa kuwa kiongozi ambayo inaweza kutumiwa na nchi maadui au makundi maovu kupenyeza majasusi ili kupata taarifa za nchi au wananchi na kisha kuzitumia kulidhuru taifa.

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia?????!!!!!!?????????
 
Wazazi wengi hawana elimu ya malezi thus wanatoa viongozi wabovu wanaotumia nguvu badala ya akili ni kwa sababu ya malezi ya kibabe babe
 
Ni muhimu kuhakikisha mfumo unatambua udhaifu huu na ujiandae kukabiliana na hali hii, ikiwemo kwa kuandaa mfumo wa malezi ya watoto utakaotupatia viongozi bora.
 
Viongozi wawe wanapatikana kwa syndicate na siyo box la kura siyo ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom