SoC03 Taswira ya Nchi ni Taswira ya kiongozi

Stories of Change - 2023 Competition

Mbojo

JF-Expert Member
May 31, 2011
1,587
1,289
Kabla ya uhuru Nchi nyingi za Afrika na Asia zilikua zinalingana katika maendeleo. Tofauti tunazoziona hivi Sasa ni matokeo ya viongozi waliokuwepo madarakani.

Viongozi ambao walikua na maono waliziwezesha Nchi zao kupiga hatua hasa katika maendeleo ya kielimu,afya, usafiri,umeme n.k.

Nchi za Afrika zilizopiga hatua zilibahatika kuwa na siasa safi, umoja na mshikamano na utekelezaji wa pamoja wa dira ya Nchi husika.

Huwezi kuleta maendeleo kama huna maono. Maono Bora kwa viongozi walioko madarakani huzaa huduma Bora kwa jamii nzima inayoongozwa.

Ili kiongozi awe Bora lazima awe na wasaidizi waliobora. Hapa ndipo tunapata kuona umuhimu wa elimu Bora katika kuchochea maendeleo.

Jamii isiyoelimika haiwezi kuyaishi maono ya kiongozi aliyeko madarakani.Hivyo Nchi yenye migogoro, umaskini uliokithiri na ukosefu wa huduma kwa jamii ni matokeo ya kiongozi waliyenaye.

Ili kuboresha huduma kwa jamii, Serikali za Afrika zinapaswa kuwekeza katika elimu. Elimu Bora inatokana na walimu bora.

Serikali nyingi za Afrika zinapenda kutumia watu wasio na elimu Ili kuwaburuza, hawapendi kukosolewa na wengi hufikiri wanaongoza wasio na uelewa.

Hivyo viongozi wengi wanajikita katika ufujaji wa Mali za serikali na kushindwa kujenga Nchi zao. Umaskini wa Afrika unatokana na viongozi wasio na maono wanaojilimbikizia Mali na wengi kuwa vibaraka wa mabepari.

Afrika inahitaji viongozi wenye maono, waliopikwa kwenye elimu bora, Afrika ina maliasili nyingi lakini tunashindwa kuendelea kwasababu ya uongozi dhaifu.

Afrika inapaswa kuwa na mifumo madhubuti ya uchaguzi ili iweze kupata viongozi bora, mifumo ambayo itaondoa rushwa, itawafanya wapiga kura wawe tu ni watu walioelimika.

Mfumo itakayoondoa mbumbumbu bungeni, maana huwezi tungiwa sheria na aliyeshindwa Kisha Nchi ipate maendeleo. Mifumo itakayojali uwakilishi wakila kundi bungeni.

inahitaji mifumo itakayodhibiti upotevu wa mapato, mifumo itakayoinua wafanya biashara kiuchumi, mifumo itakayoinua kilimo.

Afrika inahitaji watu wenye maono hayo. Hivyo muonekano wa Nchi ulivyo ndivyo ulivyo uongozi wao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom