SoC04 Tanzania ya mageuzi ya katiba mpya ya wananchi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Editha Joseph l

New Member
May 2, 2024
2
1
UTANGULIZI
Katika nchi yeyote duniani ili kuendelea ni lazima iwe na katiba nzuri na yenye kujali maslahi makubwa ya wananchi , bila hivyo tutajidanganya wote tunafahamu kuwa katiba nzuri ndo mwongozo na dira ya nchi yoyote . Ili kuwa na mabadiliko chanya na maendeleo katika taifa letu ni lazima tuwe na katiba mpya .na katiba hiyo iwe katiba ya wananchi na sio watawala , katiba yetu ni ya kikoloni na iko upande wa watawala na ndo maana raisi anaweza kufanya lolote na hakuna wa kumuhoji . Ningependa kuwe na mageuzi makubwa katika katiba yetu na nchi na wananchi wake viwe ndo vipaumbele .

Mageuzi katika utawala Bora na Sheria
Ili nchi iendelee unatakiwa kuwa na mageuzi makubwa ya kiutawala na Sheria zake na ndo mambo mengine yatafata . Utawala Bora ni pamoja na viongozi Bora watakaokuwa wanaongozwa na katiba nzuri itakayokuwa ya wananchi , na Kwa Hilo taifa letu litapiga hatua .

Uchaguzi huru na wa haki .
Inabidi katiba yetu izingitie maamuzi ya wananchi na kuwe na uchaguzi wa haki Ili tupate viongozi Bora watakao simamia Sheria na kuheshimu katiba ya wananchi , mala nyingi tumeshuhudia uchaguzi ukiharibiwa kutokana na viongozi kuwa juu ya Sheria na kupanga watu wanaowataka Ili kutimiza mambo yao , na ndo maana uratibu wa maendeleo unakuwa mgumu sana kutokana na muundo wa utawala na watu kuchaguana kichama na sio uwezo wa mtu ,

Uhuru wa vyombo vya habari
Vyombo vyetu vingi vya habari havina uhuru na haviweki wazi changamoto za watawala na badala yake vinapangiwa kitu Cha kusema , na hii ni kwasababu katiba yetu Haina vipengele vizuri vya kulinda vyombo hivyo na vingi vyao vimebaki kama machawa wa watawala na ndo maana wananchi wengi wanapoteza haki zao . Tunataka vyombo vya habari huru Ili kuwepo na uwazi .

Usawa katika uongozi
Katiba yetu ya Sasa imebeba upande mmoja na ndo maana akiingia kiongozi wa kike inaonekana hafanyi kazi nzuri na hii ni kwakuwa katiba yetu haijabeba maono ya nchi na watu wake badala yake inempa raisi nafasi kubwa ya maamuzi ya nchi.
Hivo basi imetengenezwa kimfumo dume ikiangalia upande mmoja tu , katiba yetu inabidi iwekwe katika mfumo wa kimaono na raisi kama taasisi itekeleze maono hayo ambayo wananchi wake wanatamani yafanyike Kwa mda wa Miaka 20+.

Kuwepo na vipaumbele vya elimu Bora na ya vitendo .
Inabidi tujue tunataka Nini na ulimwengu uko katika kasi ya elimu gani na Nini kinatakiwa Ili tuwe na taifa bora.Elimu yetu itoe wataalamu wanaofanya vitu ambavyo vinapatiakana katika mazingira yetu Ili kutoa utegemezi wa kuajiriwa .

Kilimo kiwe kipaumbele chetu na kisimamiwe Kwa ukaribu sana.
Inatakiwa serikali ijenge miundo mbinu mizuri ya kilimo na iwawezeshe wakulima Kwa kutoa vitendea kazi vizuri kama pembejeo za kilimo na kuajiri watafiti wa kilimo Ili kuwa na mazao maalumu ya biashara na chakula .

Mageuzi katika sekta ya Afya
Inatakiwa serikali itambue dawa za asili zinazozalishwa nchini Ili kusaidia kukuza upana wa sekta , lakini pia ijenge hospitali moja kila mkoa ambayo itakuwa na dawa za asili na zidhibitishwe na mamlaka husika Kwa matumizi ya binadamu .Badala ya kulipia bima ya Afya serikali iweke tozo maalumu Kwa kila bidhaa zinazo ingia nchini Ili matibabu yotolewe Bure na pesa hiyo ya tozo iwekwe kwenye mfuko wa Afya , hiyo itasaidia na tutapata huduma Bora .

Hatuwezi kukuza uchumi wa nchi kama hatutaweka mifumo madhubuti ya kudhibiti rushwa na ufisadi . Udhibiti wa pesa za ndani Kwa kuweka Sheria ngumu Ili kufuta rushwa naufisadi
Lakini pia serikali kutumia 70% ya Pato la ndani itasaidia kukuza uchumi wetu .

Hitimisho
Ili nchi yetu ipige hatua ni lazima ifunge mianya yote ya rushwa na ufisadi na zitungwe Sheria ngumu sana Ili kudhibiti hilo , hii yote itawezekana Kwa kuwa na katiba Bora na Sheria nzuri za kulinda Mali za umma na sio kulinda watawala kama hii tuliyo nayo . Mfumo mzuri wa utawala , katiba nzuri ndo suluhisho Kwa maendeleo ya nchi yetu , mifumo ya kichawa ndo mmomonyoko wa taifa na kutokuwa na maendeleo katika taifa letu .
 
Mageuzi katika sekta ya Afya
Inatakiwa serikali itambue dawa za asili zinazozalishwa nchini Ili kusaidia kukuza upana wa sekta , lakini pia ijenge hospitali moja kila mkoa ambayo itakuwa na dawa za asili na zidhibitishe na mamlaka husika Kwa matumizi ya binadamu
Kwa suala hili tuwaulize NIMRI?

NI wafamasia wangapi wameajiriwa ili kufanyia kazi tafiti na maendeleo ya tiba asili hadi hivi sasa. Na kama hawatoshi asee mi ni mmojawapo ninayeitaka hiyo kazi😅.

Najua tupo vizuri hadi sasa kwa tafiti za mawodini (clinical) ni rai yangu sasa tuwekeze na katika maabara (experimental studies)


Tukiachana na hilo kwa suala la katiba sina mengi ya kusema zaidi ya picha hii:
Key... penye America toa, weka TANZANIA
Screenshot_20240424-074905_X.jpg
 
Back
Top Bottom