Tache maneno: DED wa Itigi ni msomi

Hivi,mtu anaweza kuwa Mkurugenzi bila kupitia ukuu wa Idara za Halmashauri?
Yes, what's matter ni kuwa amefikia level ya senior kwenye vyeo vyake - hapo anaweza kuteuliwa kushika madaraka yoyote nchini
 
Msomi mzuri sana, je ana machapisho?

Hivi kiwa msomi ni lazima uwe na machapisho?

Kwa imani yangu naamin kuwa msomi ni yeyote kwanza anaye jua kusoma na kuandika lugha yake ya taifa na kuielewa na pia anajua kuhesabu na kukokotoa hesabu za kawaida kama +, - /, * na pia anakuwa mbunifu na mwenye mawazo chanya kwa maendeleo yake binafsi,na ya jamii yake na ya watu wanao mzunguka na taifa kwa ujumla. Huyo kwangu mimi ndiyo huwa namuona msomi,

Usomi kwangu sio vyeti vya degree,masters ,PhD nk.maan wapo wengi wenye vyeti hivi lakin wanaprove failure kwa mambo hata madogo na ambayo hayahitaji vyeti kila uchwao utadhan hawana elimu kabisa hata ya awali zaid ya utu uzima.
 
Hata iweje MAGUFUkaLI kakosea uteuzi huu kwa sana tu. Kuna watu wamesoma Political Admin au Law au Economics na wako Halmashauri au Mikoani kama Waratibu wa Wilaya au Mikoa, ila ka waacha kachukua makada wa@CCM tu!!

Ama kweli amefanya Demotivation to employees' work morale.

Kuna hadi walimu wa Nganza Sec kawachukua, KISA MSUKUMA. Kajaza tu kabila lake.
Kuwa mwalimu wa ngazi ya secondari sio kigezo cha kuto pewa madaraka. Hoja ya msing je?? Walio pewa madaraka hayo wana kidhi na wana uwezo wa kumudu majuku yao katika nafasi hizo walizo pewa? Na ili uwezw kujua utendaji wake huwezi kutumia kigezo cha kuwa mwalimu wa sec kuwa atashindwa kutekeleza majukumu yake, nadhan hapa upo wrong.huenda utendaji kazi wake ni zaid ya hicho cheo kipya alicho pewa sasa ambacho wewe unaona kimempwaya.
 
Hivi kiwa msomi ni lazima uwe na machapisho?

Kwa imani yangu naamin kuwa msomi ni yeyote kwanza anaye jua kusoma na kuandika lugha yake ya taifa na kuielewa na pia anajua kuhesabu na kukokotoa hesabu za kawaida kama +, - /, * na pia anakuwa mbunifu na mwenye mawazo chanya kwa maendeleo yake binafsi,na ya jamii yake na ya watu wanao mzunguka na taifa kwa ujumla. Huyo kwangu mimi ndiyo huwa namuona msomi,

Usomi kwangu sio vyeti vya degree,masters ,PhD nk.maan wapo wengi wenye vyeti hivi lakin wanaprove failure kwa mambo hata madogo na ambayo hayahitaji vyeti kila uchwao utadhan hawana elimu kabisa hata ya awali zaid ya utu uzima.
Naona tunataka kurudiarudia mada. Hili la nani msomi na vigezo vya kuitwa msomi vinaeleweka. Wameshaandika na kama unataka kupingana na maandishi yao hiyo fursa ipo na unaweza kuifanya. Fanya utafiti halafu unauweka hadharani kwamba unayo maarifa mapya kuhusu dhana ya usomi.
Vinginevyo kila mtu atajistarehesha kwa dhana yake bila kuwajuza wenzake. Kama ndivyo pitia kwenye hii taarifa ili ufahamu na kuongeza maarifa:Intellectual - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Kuwa mwalimu wa ngazi ya secondari sio kigezo cha kuto pewa madaraka. Hoja ya msing je?? Walio pewa madaraka hayo wana kidhi na wana uwezo wa kumudu majuku yao katika nafasi hizo walizo pewa? Na ili uwezw kujua utendaji wake huwezi kutumia kigezo cha kuwa mwalimu wa sec kuwa atashindwa kutekeleza majukumu yake, nadhan hapa upo wrong.huenda utendaji kazi wake ni zaid ya hicho cheo kipya alicho pewa sasa ambacho wewe unaona kimempwaya.
Je unafahamu Promotion criteria na muongozo wake ktk utumishi wa umma?
Huwezi kuwa Mwl from nowhere ukawa mkurugenzi hata siku moja hujawahi kukaimu nafasi hiyo wala taratibu zake huzifahamu!! Bora Mwl awe makaguzi au Afisa Elimu.

Ndio ujinga tulio nao watanzania Rais anateuwa supervissor wake wa Thesis ya PhD (Mkemia) kuwa mkurugenzi TIB (Fedha) afu utegemee ufanisi. Tuache kufanya kazi kwa mazoea bali Professionalism na Experience vitumike.
Na nidhambi kubwa sana kuchanganya serikali na siasa (Makada wa Chama flani) ktk nafasi za kitaalamu.
Kwa ujumla, baadhi yao wanaweza kuwa na Elimu ila siyo tija kwa wao kuteuliwa nafasi ya ukurugenzi.
 
Naona tunataka kurudiarudia mada. Hili la nani msomi na vigezo vya kuitwa msomi vinaeleweka. Wameshaandika na kama unataka kupingana na maandishi yao hiyo fursa ipo na unaweza kuifanya. Fanya utafiti halafu unauweka hadharani kwamba unayo maarifa mapya kuhusu dhana ya usomi.
Vinginevyo kila mtu atajistarehesha kwa dhana yake bila kuwajuza wenzake. Kama ndivyo pitia kwenye hii taarifa ili ufahamu na kuongeza maarifa:Intellectual - Wikipedia, the free encyclopedia
Dhana ya usomi haikutoka kwa mungu ila kila mtu aliona idea yake ina faa kuwaaminisha wengine na idea iliyo bebwa na watu wengi ikaaminika ndiyo sahihi , lakini hiyo hatufungi ,hivyo si vibaya kwa mtu mwingine aka generate idea yake kuhusu hilo maana hata hayo unayo yaamin yametolewa na watu ambao ni binadamu wenzio.
 
Je unafahamu Promotion criteria na muongozo wake ktk utumishi wa umma?
Huwezi kuwa Mwl from nowhere ukawa mkurugenzi hata siku moja hujawahi kukaimu nafasi hiyo wala taratibu zake huzifahamu!! Bora Mwl awe makaguzi au Afisa Elimu.

Ndio ujinga tulio nao watanzania Rais anateuwa supervissor wake wa Thesis ya PhD (Mkemia) kuwa mkurugenzi TIB (Fedha) afu utegemee ufanisi. Tuache kufanya kazi kwa mazoea bali Professionalism na Experience vitumike.
Na nidhambi kubwa sana kuchanganya serikali na siasa (Makada wa Chama flani) ktk nafasi za kitaalamu.
Kwa ujumla, baadhi yao wanaweza kuwa na Elimu ila siyo tija kwa wao kuteuliwa nafasi ya ukurugenzi.
Hayo yooote unayo yaongea wewe ni mazoea na utaratibu wa kurithi tu na si uhalisia, ni sawa na kuzoea kunywa uji au chai asubuhi na ukimuona mtu anasonga ugali alfajili uta mshangaa lakin mshangao wako si halali kwa sababu utakuwa umebebwa na hali ya mazoea kuwa asubuhi yake ni chai,supu na uji lakin hakuna baya endapo utaamua kusonga ugali alfajiri na kula.

Lakini pia usiamini kuwa kila kada hana taaluma utakuwa upo wrong ndio maana unaweza kuwa dereva wa daladala lakin umesha soma na una taaluma ya human resource management
Sasa siku umepata kazi watu watashangaa imekuwaje

Kuwa kada hakumfungi mtu kupewa nafasi serikalin na nikwambie tu kuwa mmeleta hiyo mada kwa vile wengi wao mnawafahamu ku ni wana ccm lakin vinginevyo msinge sema lakin ukweli ni kwqmba ukada wa chama sio kufuli la kukufanya usishike nyadhifa za kiutendaji ndan ya serikali.
 
Dhana ya usomi haikutoka kwa mungu ila kila mtu aliona idea yake ina faa kuwaaminisha wengine na idea iliyo bebwa na watu wengi ikaaminika ndiyo sahihi , lakini hiyo hatufungi ,hivyo si vibaya kwa mtu mwingine aka generate idea yake kuhusu hilo maana hata hayo unayo yaamin yametolewa na watu ambao ni binadamu wenzio.
Kwa kawaida katika tasnia ya usomi huwa ukiona jambo jpya unatafuta hadhira na kuwaelekeza wenzio. Watakuuliza maswali, na baadae kunakuwepo na muafaka wa hayo uliokuwa nayo. Sasa kama kuzuka na jambo ambalo halina muafaka wa jamii ya wasomi inatia shaka kukubalika. Huo ni ustaarabu na utaratibu uliojengeka katika jamii yao hao wasomi. Kama jambo halikufuata utaratibu na ustaarabu wake ni vigumu kuliafiki. Je hili lako limefuata utaratibu na ustaarabu wao? La kama halijafuta utaratibu na ustaarabu wake jitahidi ulielekeze huko ili ujijengee heshma.
 
Hayo yooote unayo yaongea wewe ni mazoea na utaratibu wa kurithi tu na si uhalisia, ni sawa na kuzoea kunywa uji au chai asubuhi na ukimuona mtu anasonga ugali alfajili uta mshangaa lakin mshangao wako si halali kwa sababu utakuwa umebebwa na hali ya mazoea kuwa asubuhi yake ni chai,supu na uji lakin hakuna baya endapo utaamua kusonga ugali alfajiri na kula.

Lakini pia usiamini kuwa kila kada hana taaluma utakuwa upo wrong ndio maana unaweza kuwa dereva wa daladala lakin umesha soma na una taaluma ya human resource management
Sasa siku umepata kazi watu watashangaa imekuwaje

Kuwa kada hakumfungi mtu kupewa nafasi serikalin na nikwambie tu kuwa mmeleta hiyo mada kwa vile wengi wao mnawafahamu ku ni wana ccm lakin vinginevyo msinge sema lakin ukweli ni kwqmba ukada wa chama sio kufuli la kukufanya usishike nyadhifa za kiutendaji ndan ya serikali.
Sija ona hoja uliyo jibu hapo!!

KAZI IPO KWA UELEWA HUU!!
 
Kwa kawaida katika tasnia ya usomi huwa ukiona jambo jpya unatafuta hadhira na kuwaelekeza wenzio. Watakuuliza maswali, na baadae kunakuwepo na muafaka wa hayo uliokuwa nayo. Sasa kama kuzuka na jambo ambalo halina muafaka wa jamii ya wasomi inatia shaka kukubalika. Huo ni ustaarabu na utaratibu uliojengeka katika jamii yao hao wasomi. Kama jambo halikufuata utaratibu na ustaarabu wake ni vigumu kuliafiki. Je hili lako limefuata utaratibu na ustaarabu wao? La kama halijafuta utaratibu na ustaarabu wake jitahidi ulielekeze huko ili ujijengee heshma.
Kama uliisoma vyema post yangu utakuwa umeona kuwa sijajumuisha jamii kwa kile ninacho kiamini na ndio maana nikasema mimi ninavyo uelewa usomi na si jamii inavyo uelewa usomi, hapo nilimaanisha mimi ,,mimi sipo katika jamii inavyo uelewa usomi ndio maana mimi nikaamua kuuelewa tofauti na hayo mazoea ,

maana kama ni jamii imeaminishwa vingi visivyo na uhalisia na vyenye utata kuviamini moja kwa moja na ndio maana kuna baadhi ya mambo yana endelea kufanyiwa marekebisho kutoka kana na wale walio tangulia walivyo iaminisha jamii na kuona kuwa wanacho kiamin hakipo hivyo kilivyo katika uhalisia wake.
 
Hapa hakuna aliyeaminishwa ni taratibu na ustaarabu ulipo ndivyo unavyotaka. Na hakuna kuaminishana, hizo taratibu na ustaarabu upo wazi na unaeleweka na upo katika kumbukumbu za kiofisi. Kama kuna marekebisho ni vyema yakawekwa wazi ili kila kitu kifahamike kwa jamii. Unajua ofisi za umma haziendeshwi kiimla au kuaminisha watu. Inatengenezwa misingi, sheria na taratibu na wahusika wanafahamishwa hayo mabadiliko.
Kumekuwa na kauli ambayo sio njema na wala haina afya katika utendeshaji wa serikali kwamba kuna baadhi ya mambo yanaendelea kufanyiwa marekebisho. Hayo mambo hayatamkwi, hayatajwi hadharani na hakuna mtu anayeyajua kiundani. Hii ndio utaratibu wa kiimla na hauna staha katika uendeshaji wa shughuli za umma.
 
Hapa hakuna aliyeaminishwa ni taratibu na ustaarabu ulipo ndivyo unavyotaka. Na hakuna kuaminishana, hizo taratibu na ustaarabu upo wazi na unaeleweka na upo katika kumbukumbu za kiofisi. Kama kuna marekebisho nyeyoteakawekwa wazi ili kila kitu kifahamike kwa jamii. Unajua ofisi za umma haziendeshwi kiimla au kuaminisha watu. Inatengenezwa misingi, sheria na taratibu na wahusika wanafahamishwa hayo mabadiliko.
Kumekuwa na kauli ambayo sio njema na wala haina afya katika utendeshaji wa serikali kwamba kuna baadhi ya mambo yanaendelea kufanyiwa marekebisho. Hayo mambo hayatamkwi, hayatajwi hadharani na hakuna mtu anayeyajua kiundani. Hii ndio utaratibu wa kiimla na hauna staha katika uendeshaji wa shughuli za umma.
Kwan huo utaratibu ulitoka wapi na chanzo chake nini?kwani ni inborn kama njaa?? Au kama kimo ,urefu au ufupi? Kama sio basi ni imani iliyo aminishwa katika jamii na kuwekwa kama huo utaratibu unao usema ambao pia unaweza kufanyiwa mabadiriko wakati wowote na mtu yeyote .
 
LUHENDE PIUS GERALD SHIJA MKURUGENZI MPYA WA ITIGI.

* Pius alimaliza Sekondari O' level Kilosa Sekondari ( 1990- Kizunguzi), akaenda form six kisha diploma, akawa mwalinu wa sekondari.

* Mwanzoni mwa miaka ya 2000 akawa Mkaguzi wa shule huko shinyanga. 2005-2007 Alikuwa akisoma diploma in education management and administration (ADEM-BAGAMOYO).

* Mwaka 2008 akaenda ARUSHA UNIVERSITY, alipomaliza akapelekwa ukaguzi kanda ya Tabora-Kigoma.

* Mwaka 2013 Alianza Masters of Education in educational planning and administration- JORDAN UNIVERSITY.

Mwaka 2015 alihamia ukaguzi kanda ya mashariki. Na aligombea ubunge jimbo la Kishapu akashindwa kura za maoni.

**************************
Namfahamu shija ni msomi sana. Jamaa yuko smart. Niklikuwa naye pale chuo kikuu tukifanya degree yetu ya kwanza pamoja. Ni mtaratibu, mtu makini na asiye na papara.
 
Hivyo vyuo nilikuwa sijasikia hata kimoja!
Acha ujinga. Uvisikie wewe. Ulimwengu wa kujisifia kutokana na chuo ulichosoma sasa umekwisha. Tunataka kuona product yako kwa jamii. Ninafanya kazi na watu wengi wananaodaiwa kusoma vyuo vikubwa lakini hawana kitu. Mtu hawezi chochote then anasema nimesoma Mzumbe au Udsm. Hakuna kitu.
 
Kwan huo utaratibu ulitoka wapi na chanzo chake nini?kwani ni inborn kama njaa?? Au kama kimo ,urefu au ufupi? Kama sio basi ni imani iliyo aminishwa katika jamii na kuwekwa kama huo utaratibu unao usema ambao pia unaweza kufanyiwa mabadiriko wakati wowote na mtu yeyote .
Naona niweke kando makasia. Tunapwelea kwenye bahari moja chombo kimoja ila fikra tofauti. Marumbano yasiyo na dira ya kisayansi ambayo yamekosa tashtiti mujarabu. Kunena vitu visivyo na taratibu wala staha ya kisayansi wengine hatuwezi. Nachelea sana kuonekana sijui ustaarabu wa maamuzi ya kisayansi na ustaarabu wa kifikra. Kila akheri!
 
Hii CV nimeshindwa kuiunganisha. Hongera lakini hebu nisaidieni huko nchini Jordan alienda kusomea Kitu gani?
 
Kuna mambo muhimu yanayozingatiwa wakati wa kuteua watendaji wakuu wa idara au taasisi. Usomi pekee hautoshi. Hata hivyo hakuna SI unit ya Usomi inayo weza kutofautisha msomi na asiyekuwa msomi. Kama mtu ana Elimu ya ngazi ya Masters degree unawezaje kusema si msomi ? Unapotaka kuajiri daktari kwenye hospitali, msomi ni yupi kati ya mtu mwenye Advanced Diploma ya Uganga na yule aliye na PhD ya Mechanical engineering? Mimi sioni mantiki ya Vyeti kuwa kigezo cha kuteua kwakuwa vyeti bila ya Field Competence ni bure. Kwamfano tu :Ukitazama kwenye sekta Elimu, Kuna walimu wana vyeti vyama Master's degree ya Education lakini wanazidiwa katika teaching competence na walimu wa chini yao. Kuna mwalimu wa Diploma anatoa A za Chemistry katika mitihani ya Form 4 kila mwaka wakati shule hiyo hiyo Kuna mwalimu wa Degree hujawahi kutoa hata B ya Chemistry zaidi ya D na F.
 
"...Mwaka 2013 Alianza Masters of Education in educational planning and administration- JORDAN UNIVERSITY...
"

hawa nao wanatoa Masters degree?!
 
hapo kwenye kugombea ubunge kura za maoni angekuwa aligombea kupitia upinzani asingechaguliwa nafasi aliyo chaguliwa
 
Back
Top Bottom