Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 40,390
- 97,925
Punguza jazba mama, kumbuka uongozi ni msalaba.Wewe nani kakuambia Hawa hawatasoma tena? Mbona hata huko mahabusu za watoto wanasoma. Mbona mnapotosha ukweli kuwa ilibidi waondolewe pale wakarekebishwe tabia ndiyo waende tena kuanza shule? Mlitaka waachwe pale waharibu wote au?
Halafu mbona mimi nimekuta walishaondolewa shuleni kitambo? Au mnadhani mimi ndiyo jana nimewaondoa? Mbona chanzo cha taarifa nacho kimedanganya? Au nacho nikishtaki?
Haya yote ulipaswa utuelimishe kama hivi leo ndio nimetambua kwamba jela watoto wanasoma.
Unapo kua mkali na kutishia kumshataki mchangiaji na mleta mada sioni kama ni jambo ka busara.
Endelea kutuelimisha ili nasisi huku Ushirombo tupate elimu kupitia wewe nasi tutawaelimisha na wengine.