DOKEZO Tabora: Wanafunzi wafukuzwa kwa kujirekodi picha za utupu na kuzisambaza

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wewe kwenye simu umeona mabaya tu
Hujui Kuna mazuri mengi ya simu,
Kwanini mnaamini mtoto kuwa na simu ni dhambi?

Haki ya misingi ni mtoto apate elimu hata iweje, awe mlemavu, awe Malaya, mlevi n.k
Hakuna sheria ya kutengua mtoto asipate elemu
Kamwambie mbunge wako sasa apeleke mswada bungeni ili sheria zibadilishwe ziwekwe unazo taka ww.
 
Sasa mbona kwa kufanya hivyo ndio wamezidisha ttz
We acha tu. Adhabu sio lazima kufukuza shule. MPE adhabu akome asirudie tena na akahadithie wenzake lakini kumfukuza shule ni kumharibia maisha yake tu.

Kwani kwa kupiga picha ya utupu kuna uhakika kwamba hawezi kuifaa familia yake, ukoo wake, na taifa hapo baadae? Huyo huyo akipata mazingira sawia anaweza kuleta mchango bora kabisa kwa nchi kuliko hata wenzake wengi humo darasani anakosoma
 
hakuna siri, kwa mtazamo wangu, katika mawaziri failures wa mama Samia huyu Dkt. Gwajima D anaongoza.

Taifa limeporomoka kabisa kimaadili mpaka naamini kuwa yeye ndiye muhusika mkuu wa maadili kuporomoka kwa kushindwa kwake kudhibiti kwa njia za kisasa.

Nilicheka peke yangu, aliponambia humu JF kuwa anatumia mbinu za enzi za mMkapa kupambana na matatizo ya sasa.

Nilimponda hapohapo, kwani hata nilipojaribu kumshauri alikuwa hanielewi kabisa. Nikaelewa kuwa huyu mwanamke hana ubunifu kabisa.

Tunajionea maadili ya jamii yanavyozidi kuporomoka kila kukicha.
Katika mawaziri wote,ni Dkt. Gwajima pekee anayetenda kazi,wengine wanapiga porojo.
 
Wakuu habari zenu!

Kuna hii taarifa ya hawa watoto wa Shule kufukuzwa huko Tabora, kuna namna sauti inatakiwa kupazwa kutokana na adhabu kubwa waliyopewa ukilinganisha na umri wao, walikuwa na nafasi yakuonywa na kuendelea na masomo ila sio kukatiza mazima.

Wanafunzi wawili wa kike kutoka shule moja ya sekondari mkoani Tabora, wamefukuzwa shule kwa makosa ya kujirekodi picha za utupu na kuzisambaza.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Gwajima D , amewataka maafisa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Jamii na maafisa Elimu wote nchini kuimarisha madawati ya ulinzi wa watoto shuleni ili kusaidia kupunguza mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi.

Soma, Pia:
+
Tabora: Wanafunzi Tabora wakamatwa na simu zaidi 120 zilizoungwa makundi wanayotumia kutumiana picha/video za ngono
Nini sababu ya wao kujirekodi? Lazima wahojiwe pengine kuna watu waliyowashawishi kufanya hayo huenda pia ni vigogo, baada ya uchunguzi ndiyo wapewe adhabu wote waliyohusika ambayo haitawaathiri na maisha yao ya elimu.
 
Kuwafukuza wameasaidia nini?
Mnarudisha wenye mimba, mnafukuza waliorekodi viungo ni ujinga wa hali ya juu.

Hivyo uchi ndio uharibu maizha ya mtoto?

Walitakiwa kuadhibiwa, kurekebishwa na kuonywa
Dkt. Gwajima D
Hii haiko sawa
Tunafukuza ili wasisambaze sumu Kwa watoto wengine kuwarudisha wenye mimba Tanzania mostly ni siasa ila wengi huwa hawarudi
 
Lakini wakuu....
Minaona kwamba malezi ya mtoto hutokea nyumbani.
Ili mtoto awe na nidhabu, mwenye kuheshimu wakubwa, mwenye kutambua maadili mema nk: haya yooye huanzia nyumbani na kisha shuleni anaenda kufuata masomo pamoja na kuzifuata sheria za shule.
Mtoto aliepata msingi wa malezi bora anajulikana tu kuanzia kwenye discipline.
Wazungu na wasomi wao walisha kumbana sana na hayo mambo wakafikia proof na conclusion kuwa huo ni umri wa STUPID AGE ...
Walichokifanya hao watoto ndiyo maana halisi ya STUPID AGE hakuna kipya..kama ...serikali pumbavu ya ccm imeona ni sawa kuwarudisha shule wanafunzi walio zini hadi kupata mimba kabisa na kuzaa na kuwa wamama ....vipi hao kujirekodi tu video iwe kufukuzwa shule
 
Back
Top Bottom