Swali, Youtube huwa wanalipa kutokana na nchi uliosajili chaneli yako?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
33,916
50,267
Nimeona baadhi ya chaneli za Youtube, zinazomilikiwa na watu wa huko US, Canada, UK, Nigeria, SA n.k ambazo baadhi zina maudhui ya kusaidia wahitaji mbalimbali ili kuvutia watazamaji.

Kinacho nishangaza zaidi, kila video wanazozitoa ni kusaidia tu watu; sasa najiuliza, ina maana huko kwao Youtube inawalipa sana kiasi cha kila video kuwa na maudhui ya kusaidia watu kifedha na mali?

Na kama ni hivyo, wanazipataje hizo fedha? Na huku kwetu, je wanalipwa sawa na hizo nchi zingine?

Leteni majibu​
 
Jibu ni ndio na hapana . Lakini kwanza fahamu yafuatayo. 1. Malipo ya Toutube ni kweli yanaweza kuathiriwa na Visitor anapotoka (Geos) hii inamaana visitor akitokea Tanzania utalipwa kidogo kuliko akitokea Canada, kenya , au ulaya.
2. Niche Aina ya maudhui , kila maudhui ya kiwango chake cha kulipwa mfano mtu anayepost content ya insuarence atalipwa hela kubwa kuliko anayepost Michezo. Hovyo huenda aina ya maudhui wanayoposti yanahela zaidi.

Kwanini ndio na hapana? Youtuber wa huko wana nafasi kubwa kuwapata views wa nchi zinazolipa zaidi. Lakini hata youtuber wa Tanzania anaweza kutarget kupata hao visitor. Kwao sio ajabu kupata dollar 10000$ kwa siku . Lakini suala la kusaidia inawezekana ni kutafuta content au kweli wana moyo wakusaidia
 
Jibu ni ndio na hapana . Lakini kwanza fahamu yafuatayo. 1. Malipo ya Toutube ni kweli yanaweza kuathiriwa na Visitor anapotoka (Geos) hii inamaana visitor akitokea Tanzania utalipwa kidogo kuliko akitokea Canada, kenya , au ulaya.
2. Niche Aina ya maudhui , kila maudhui ya kiwango chake cha kulipwa mfano mtu anayepost content ya insuarence atalipwa hela kubwa kuliko anayepost Michezo. Hovyo huenda aina ya maudhui wanayoposti yanahela zaidi.

Kwanini ndio na hapana? Youtuber wa huko wana nafasi kubwa kuwapata views wa nchi zinazolipa zaidi. Lakini hata youtuber wa Tanzania anaweza kutarget kupata hao visitor.
Kwenye hii video, unaweza kutoa maoni gani?

View: https://www.youtube.com/watch?v=Ixu3S_dwogU
 
Kwa nini kunakuwa na tofauti hizo za rate?
Sababu wanaoweka matangazo ndio wanaamua. Purchasing power ya Mtamzania si sawa na Usa.

Mfano Vodacom Tanzania anaweka Tangazo YouTube anasema mimi Nita lipa sh 5 kwa view, ina maana Mtanzania aki angalia basi mwenye video analipwa let's say sh 3. Wanatoa hela ndogo sababu hata ukiona Tangazo hutawaingizia sana hela.

Ila kampuni za Marekani kama Apple zikiweka Tangazo wanalipa zaidi sababu wa husika wanaowatarget purchasing power yake ni kubwa hivyo hata wakilipa sana hela itarudi. Na wao Apple waliweka Tangazo wana specify kabisa Mtanzania asioneshwe aoneshwe Mmarekani, Muingereza, Japan Etc.

Hivyo ili content creator apate hela inabidi aweke content zinazotarget nchi tajiri ili apate matangazo yenye hela.
 
Kwanini yule mwenye viewers wa marekani analipwa zaidi?
Malipo ya youtube hutegemea matangazo. Ngoja nikuulize swali wewe nimfanya biashara wa Iphone kuna watu wawili wanakutangazia biadhara , 1. Mmoja anaenda kukutangazia kwenye shule ya primary kwa wanafunzi huko kitohori . Wapili anaenda kukutangazia biashara kwa wadada wa chuo. Wewe utamlipa Yupi zaidi?
 
Kwenye nchi zilizoendelea watu wana vipato vikubwa kwahiyo wanaweza kufanya manunuzi mtandaoni.

Huku kwetu watu wana vipato kidogo kipaumbele ni mahitaji ya msingi tu.

Ulishawahi kuona tangazo youtube ukaamua kununua hicho kitu? Umewaona watanzania wangapi wakifanya hivyo?
Inawezekana uko sahihi, nini sasa kifanyike ili na sisi youtube zitufanye tuwe matajiri?
 
Sababu wanaoweka matangazo ndio wanaamua. Purchasing power ya Mtamzania si sawa na Usa.

Mfano Vodacom Tanzania anaweka Tangazo YouTube anasema mimi Nita lipa sh 5 kwa view, ina maana Mtanzania aki angalia basi mwenye video analipwa let's say sh 3. Wanatoa hela ndogo sababu hata ukiona Tangazo hutawaingizia sana hela.

Ila kampuni za Marekani kama Apple zikiweka Tangazo wanalipa zaidi sababu wa husika wanaowatarget purchasing power yake ni kubwa hivyo hata wakilipa sana hela itarudi. Na wao Apple waliweka Tangazo wana specify kabisa Mtanzania asioneshwe aoneshwe Mmarekani, Muingereza, Japan Etc.

Hivyo ili content creator apate hela inabidi aweke content zinazotarget nchi tajiri ili apate matangazo yenye hela.
Kuna video nimeziambatanisha, ebu ziangalia utupe elimu, kwa maudhui waliyonayo, yanavutia vipi kampuni kuweka tangazo.​
 
Back
Top Bottom