Shehe Ponda: Ukitaka kuangamiza Taifa lolote Duniani usitumie Mabomu bali Ua Mfumo Wao wa Elimu, Magorofa yataanguka mikononi mwa Wahandisi!

Mimi hajanitosheleza kwa hoja hiyo.

Tuseme rushwa iliyotamalaki kila sekta za umma za Serikali hii ni umbumbumbu wa kielimu wa staff na wananchi kwa ujumla wao?

Majaji wamesomea sheria lakini wanajigeuza vihiyo wa sheria.

Waendesha mashitaka na Dpp wao wanajifanya hawajui sheria na 'kutohoa' maudhui ya mashtaka ya msingi ya kesi za watu na kupelekea kesi kutupiliwa mbali, hawajasoma hao, pamoja na vurugu zingine katikq taasisi za kutoa haki na huduma nchini mwetu?

Mheshimiwa Shehe angeliweka bayana kilichotufikisha kwenye haya, siyo elimu.

Elimu watu wanayo lakini wakiingia kwenye mfumo uliotufikisha hapa wanajifanya hawajasoma na wameokotezwa majalalani.
Elimu ya Tanzania haitoi Maarifa ndicho anachomaanisha

Unaingia Chuo kikuu na kupata Ganda bila Maarifa

Mtu kama Lipumba Kwa mfano ana Maarifa gani? 🐼😂
 
Back
Top Bottom