MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
924
1,096
Watumishi wa Serikali katika Kada mbalimbali ambao waliondolewa kazini kutokana na tuhuma za kuwa na vyeti feki vya taaluma. Serikali imeagiza mchakato wa kuwalipa mafao yao uanze mara moja.

Siku ya leo Mawaziri Wawili watafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu michango ya pensheni waliyokatwa Watumishi waliondolewa kazini baada ya zoezi maalumu la Uhakiki wa vyeti .

Mkutano huo utaongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menijementi ya Umma na Utawala Bora. Mhe.Jenista Mhagama

Pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.

Mkutano utaanza saa tatu kamili asubuhi katika ukumbi wa PSSSF Tower ghorofa ya Nne Dodoma.
 
Watapewa michango yao tu, sio ya mwajiri wala sio pension.

Wengi wameliwa vichwa wakiwa na mshahara chini ya m1 na wakiwa kazini pungufu ya miaka 15 na ikumbukwe walianza kazi na mishara midogo sana pungufu ya laki.

Watapata hela pungufu ya milion 6
 
Watapewa michango yao tu, sio ya mwajiri wala sio pension.

Wengi wameliwa vichwa wakiwa na mshahara chini ya m1 na wakiwa kazn pungufu ya miaka 15 na ikumbukwe walianza kaz na mishara midogo sana pungufu ya laki.

Watapata hela pungufu ya milion 6
Umejauje?
 
Kuna watu Unakuta yeye alitumia cheti kimoja na ndugu yake mmoja Akaenda police Mwingine Nursing sasa katika kuwatafuta hawa vyeti feki ..huyo wa police akafungiwa mshahara sasa huyo automatically akajiondoa so hapo ...inakaaje ktk kupewa kiinua mgongo?
 
Watapewa michango yao tu, sio ya mwajiri wala sio pension.

Wengi wameliwa vichwa wakiwa na mshahara chini ya m1 na wakiwa kazn pungufu ya miaka 15 na ikumbukwe walianza kaz na mishara midogo sana pungufu ya laki.

Watapata hela pungufu ya milion 6
Milioni 6 si haba.... Kuliko kudhulumiwa mazima. Naona watu wakienda kujiajiri na kupata mapato makubwa kuliko waliyokuwa wakipata wakiwa wameajiriwa....

Mitano tena kwa mama
 
Mtu akiwa na cheti feki ukweli ni kwamba inabatilisha hata ajira aliyoipata kwa kutumia vyeti hivyo. Katika jambo hili nasimama na JPM.

Mambo ya kugushi nyaraka ni kinyume cha sheria. Kwa hiyo basi ile kutokushtakiwa na kuhukumiwa ilikuwa ni huruma tosha kutoka serikalini. Sasa suala la kuwalipa waliogushi vyeti linatoka wapi wakati ajira zao zilikuwa batili!?

Katika baadhi ya mambo nilimuelewa sana JPM. Alikuwa jasiri, mwenye uthubutu wa kuchukua hatua na kufichua uozo. Sasa msimamo wa serikali umeshabadilika na kutaka kuwapa shavu wakosaji!?

RIP Magufuli.
 
Watapewa michango yao tu, sio ya mwajiri wala sio pension.

Wengi wameliwa vichwa wakiwa na mshahara chini ya m1 na wakiwa kazini pungufu ya miaka 15 na ikumbukwe walianza kazi na mishara midogo sana pungufu ya laki.

Watapata hela pungufu ya milion 6
Michango yao sio pension?
 
Kati ya serikali na wao nani mwizi hapo??

Hawajaiibia tu serikali pia wamesababisha watu wenye sifa kukosa hizo nafasi.

Hawa hawakustahili kulipwa, walipaswa washtakiwe kwa ulaghai au kughushi nyalaka ( wataalamu wa sheria wanaweza kufafanua zaidi)
Serkali iinayoongozwa na watafuta sifa matokeo yake ndio haya! Ushawahi kujiuliza hata nchi za wenzetu Mfano ulaya huko uwe na cheti feki na ubainike hali itakuwaje? Unahangaika kuwapatia hela wezi badala ya kuwapa mitaji vijana wasio na ajira mtaani!
 
Na kwanini walifanya sabotage ? Kutumia vyeti ambavyo sio halali
Mifumo ya elimu ya zamani ilikuwa siyo tafiki.

Unakuta mkoa mzima una private secondary school moja. Darasa zima wanaenda secondary school wanafunzi wawili. Kurudia darasa la 7 ni marufuku. Mtu anaenda mahali pengine, anarudia darasa kwa kutumia jina la mtu mwingine. Au aliyepata nafasi ya kuendelea sekondari za serikali ameamua kutokwenda, anaenda seminary school, anampa nafasi ndugu yake.

Hao watumishi walionewa kwa sababu ya nafasi zao. Mbona akina Bashite, Madelu, Bagalile (wachache tunaowafahamu), hawakufukuzwa.
 
Mtu akiwa na cheti feki ukweli ni kwamba inabatilisha hata ajira aliyoipata kwa kutumia vyeti hivyo. Katika jambo hili nasimama na JPM.

Mambo ya kugushi nyaraka ni kinyume cha sheria. Kwa hiyo basi ile kutokushtakiwa na kuhukumiwa ilikuwa ni huruma tosha kutoka serikalini. Sasa suala la kuwalipa waliogushi vyeti linatoka wapi wakati ajira zao zilikuwa batili!?

Katika baadhi ya mambo nilimuelewa sana JPM. Alikuwa jasiri, mwenye uthubutu wa kuchukua hatua na kufichua uozo. Sasa msimamo wa serikali umeshabadilika na kutaka kuwapa shavu wakosaji!?

RIP Magufuli.
Tuambie Ben alipo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom