Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,531
- 49,369
CHADEMA katika kampeni yake ya NO REFORM NO ELECTION, haitafuti upendeleo bali inatafuta haki na ulinzi wa thamani ya kura. Hivi CCM kama huwa inashinda kwa haki, si ndiyo ungekuwa muda sahihi kukubali mapendekezo yote yatakayoufanya mchakato wa uchaguzi kuwa huru, wa haki na wa uwazi ili wawadhihirishie Watanzania na Dunia nzima kuwa wamekuwa wanashinda kwa haki? Kwa nini waligomea maoni ya wananchi na taasisi za dini, chama cha wanasheria Tanganyika na chama cha wanasheria wanawake, na hata maoni yaliyotolewa na watu maarufu katika Taifa letu?
Taasisi za dini, vyama vya upinzani, Chama cha wanasheria Tanganyika, Chama cha wanasheria wanawake, watu maarufu kama Jaji Warioba, Prof. Shivji, Butiku; wote waliwiana katika mapendekezo yafuatayo:
1. Mwenyekiti na makamishna wote wa TUME YA UCHAGUZI wasiteuliwe na Rais - CCM na Serikali yao wamegoma.
2. Uchaguzi usisimamiwe na wakurugenzi wala watumishi wa umma -- CCM na serikali yao wamegoma.
3. Matokeo ya uchaguzi, kwa ngazi zote, kuanzia udiwani mpaka Urais, kunapokuwa na haja, yahojiwe mahakamani - CCM na serikali yao wamegoma.
4. Watendaji wa Tume ya Uchaguzi, wakifanya uovu wanapotekeleza wajibu wao, washtakiwe mahakamani - CCM na serikali yao wamegoma.
5. Uhesabuji kura na majumuisho, vifanyike kwa uwazi kama inavyofanyika kwenye mataifa mengine - CCM na serikali yake wamegoma.
6. Polisi waondolewe kwenye michakato ya uchaguzi, wabakie na wajibu wao wa kulinda usalamawa raia - CCM na serikali yake, wamegoma.
Jiulize hayo mambo yote yaliyopendekezwa na wadau mbalimbali yalikuwa na kasoro gani? Kwa kugomea mapendekezo haya yaliyokuwa na dhamira njema, kuna mtu yeyote bado anaamini CCM ya sasa ina dhamira njema na Taifa hili?
Watanzania wenye dhamira njema, hata kama wamo ndani ya CCM, tuungane dhidi ya ushetani wa kupora mamlaka ya wananchi.
NO REFORM NO ELECTION.