Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,686
- 1,237
Mashindano ya Samia Kagera Cup 2024 yaliyowakutanisha vijana na wananchi wa Mkoa Kagera kwa kuwahamasisha kushiriki kikamilifu na kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024, kushiriki shughuli za maendeleo, kuonyesha vipaji pamoja na kuongeza ushiriki katika shughuli za Kijamii.
Akizungumza katika fanaili ya Ligi hiyo iliyofanyika uwanja wa Kaitaba - Bukoba kwa kuzikutanisha timu ya Biharamulo FC na Karagwe FC, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amepongeza waandaaji wa mashindano hayo kwa kuunga mkono jitihada za Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kukukuza Sekta ya Michezo.
Bashungwa ametoa rai kwa vijana na wananchi wa Mkoa wa Kagera kujitokeza na kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwachagua viongozi watakaoleta maendeleo kwa wananchi.
Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Sera ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imetoa fursa kwa vijana kujitokeza katika ushiriki na usimamizi wa maendeleo kwa jamii ambao unaanzia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kadhalika, Bashungwa amewapongeza wadau na wadhamini waliofanikisha Mashindano hayo ambao ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, KPD Clearing and Forwarding, Clouds Media Group, Shadaka Sports na Chama Cha Mpira Mkoa wa Kagera.
Kwa upande wake, Mwanzilishi na Muandaaji wa Samia Kagera Cup, Leodgar Leonard Kachebonaho ameeleza Mashindano ya Samia Kagera Cup yamelenga kuwahamasisha vijana kwa kuwatia moyo kuwa sehemu ya mchakato wa kidemokrasia, hususan katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024 ili kuunda jamii yenye usawa, haki na ustawi kwa kushirikiana.
Kachebonaho ameeleza Mashindano hayo yalianza tarehe 09 Novemba 2024 kwa kuzikutanisha Timu nane za Wilaya zote za Mkoa wa Kagera ambapo mashindano hayo yatakuwa endelevu kila mwaka
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-11-24 at 14.45.44.jpeg430.2 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2024-11-24 at 14.45.45 (1).jpeg388.8 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2024-11-24 at 14.45.48.jpeg477.7 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2024-11-24 at 14.45.50.jpeg464.5 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2024-11-24 at 14.45.51.jpeg603 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2024-11-24 at 14.45.53.jpeg491.2 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2024-11-24 at 14.45.55.jpeg388.8 KB · Views: 3