Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 24,793
- 74,961
Umeandika madudu gan haya sasa????
Wanageuza taifa kuwa familia ya kambare. Baba, mama, mtoto wote wanasimamisha sharubu.Mamlaka aliyotumia sio yake, angekua mbunge sawa. Mbunge ndio mwenye haki ya kuzungumza hadharani kama hivyo na isingeonekana ni kosa.
RC Antony Mtaka kama watoto wakimdharau Waziri wetu je watamheshimu nani kumsema Waziri mbele ya watoto umekosea.
Hiyo sio nidhamu waziri yupo juu yako huwezi kumsema na kuwakataza watoto wasifuate maagizo yake.
Kama ulikua na nia hiyo ungesubiri umwambie kwenye mkutano wa viongozi wa serikali kuu mkiwa pamoja lakini sio kama hivyo.
Hao watoto wanajua waziri wa elimu ni kiongozi wako hata wewe ni boss wako wa elimu kwenye mkoa wako. Sasa hivyo ulivyo msema na kujiwekea mamlaka hadharani kwakweli umekosea sana.
Jitokeze tu uwaombe radhi waTanzania kwa kumkosea adabu Waziri wa Elimu.
Hayo mamlaka uliyoyatumia ulitakiwa uyatumie kwa maafisa elimu wa mkoa, maafisa elimu wa wilaya na wakuu wa wilaya kwenye mkoa wako.
jamaa amekosea sanaRC atakuwa anavuta bange
Lakini Ndalichako sialipigiwa Sana debe hapa jf mpk JPM akamteua?Waziri ndalichako mwenyewe ni mzigo inabidi apunzishwe tu hyo nafasi licha ya uprof wake wizara imemshinda
Una hakika watoto wa Mtaka wanasoma kayumba?RC Mtaka akili kubwa hata akiondolewa haimaanishi Ndalichako ni competent kwenye nafasi aliyonayo.
Prove wrong alichosema RC Mtaka, hao mawaziri watoto wao wanasoma shule za kata? Kutwa wao kutoa matamko kuhusu elimu
Kutokusoma shule ya kata sio kosa wala jinai. Kama waziri au mtu yeyote ana uwezo wa kumpeleka mwanae shule iliyo bora zaidi sio jinai.RC Mtaka akili kubwa hata akiondolewa haimaanishi Ndalichako ni competent kwenye nafasi aliyonayo.
Prove wrong alichosema RC Mtaka, hao mawaziri watoto wao wanasoma shule za kata? Kutwa wao kutoa matamko kuhusu elimu
Ni sahihi kwan kuna uongo kaongea hapo? Hiyo kweli tupu mkuuAmeteleza kwa kusema ukweli!!! Binafsi nawakubali sana watu wanaosema ukweli.
Hayo mambo ya kubembelezana na kufichiana madhaifu, yalishapitwa na wakati.
Badala ya kujadili issue, unatumia tukio hilo kutema chuki zako binafsi dhidi ya Ndalichako.RC Mtaka akili kubwa hata akiondolewa haimaanishi Ndalichako ni competent kwenye nafasi aliyonayo.
Prove wrong alichosema RC Mtaka, hao mawaziri watoto wao wanasoma shule za kata? Kutwa wao kutoa matamko kuhusu elimu
Ndalichako ndiyo kavuka mipaka ya kuwa "waziri juha". Yaani anasema asichokijua anajua asichokisema.Una hakika watoto wa Mtaka wanasoma kayumba?
Yule alikuwa anatafuta sifa za kijinga kwa wananchi hata kama alikuwa na pointi, ila alivuka mipaka ya uwasilishaji wa ujumbe wake.
Watoto wa Mtaka hawasomi Kayumba.Una hakika watoto wa Mtaka wanasoma kayumba?
Yule alikuwa anatafuta sifa za kijinga kwa wananchi hata kama alikuwa na pointi, ila alivuka mipaka ya uwasilishaji wa ujumbe wake.
Hua ni dhambi kusema ukweli siku hizi hasa pale unapokua kati ya genge la watawala.Binafsi nimepata fursa ya kutazama clip moja ikimuonyesha mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dodoma akiongea nawananchi kuhusu suala la kambi za masomo ya ziada kwa wanafunzi wakati wa likizo.
Kama mwananchi nimesiitishwa na baadhi ya maneno yaliyotumika pale.
Hoja yangu hapa sio SAHIHI au KUTOKUWA SAHIHI kwa tangazo lile la mheshimiwa waziri wa elimu.
Hata mimi binafsi, natofautiana na tangazo lile la kusitisha camp za masomo wakati wa likizo kwa watoto wetu.
Tatizo lililopo hapo ni lugha, iliyotumiwa na mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dodoma kwenye kufikisha ujumbe wake kwa wananchi
Je kulikuwa na ulazima gani kwa mheshimiwa mkuu wa mkoa, kusema kuwa aliyetoa/ waliotoa tangazo lile, alifanya/walifanya hivyo kwa kuwa tu mtoto/ watoto wake wanasoma nje ya nchi?
Maana ya kauli hiyo inaweza kuwa.
Kwamba kuwa watu tuliowapa/ waliopewa dhamana ya kusimamia elimu nchini kwetu, hawana uchungu wa elimu yetu, kwa sababu tu watoto wao wasoma nje ya nchi.
Kauli hiyo sio kwamba tu inamdhalulisha mteule wa Rais, bali pia inaweza kuwa inamkosea heshima hata aliyemteua yeye mheshimiwa mkuu wa mkoa Dodoma.
Kama ningekuwa mimi ndio mkuu wa mkoa wa Dodoma.
Ningewaambia wananchi, nyie endeleeni na utaratibu wa kuweka kambi za masomo ya ziada, wakati sisi kama uongozi wa mkoa, tunaendelea kufanya mawasiliano na wenzetu wa wizara ya elimu.
Uongozi ni dhamana, ni dhamana kubwa, ni muhimu sana kwa kiongozi kuchunga ndimi zao, pale wanapozungumza na wananchi/ umma.