CHADEMA mkichukua nchi mwaka 2358 mtaanza kumtaja waziri mkuu kwanza. Ila kwa sasa twende na utaratibu uliopo.Akitambua uwepo wa viongozi na waalikwa katika Mkutano wa wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara, Rais Samia kaanza kwa kutambua uwepo wa Makamu wa Rais kisha Rais wa Zanzibar na ndio akamataja Waziri Mkuu wa Tanzania, Bwana Kassimu Majaliwa.
Swali langu ni je, kati ya Raisi wa Zanibar na Waziri Mkuu wa Tanzania, ni nani mwenye cheo kikubwa?
Zanzibar si ni sehemu ya Tanzania, sasa iweje Rais wa Zanzibar ambae ni sehemu tu ya Muungano awe juu ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?