Rais Samia afuta sherehe za Uhuru, aagiza fedha zitumike kusaidia huduma za kijamii

Ili fedha zielekezwe kwenye kampeni za CCM 2025.
Hayo mengine ni matangazo ya kupambia tu.
 
Huku ni kudanganyana. Yaani hizo fedha leo tarehe 04/12, bado tu hazijaanza kutumika, kwa ajili ya tukio la tarehe 9/12?

Kama kweli Samia angekuwa serious angetangaza hili angalau miezi mitatu mbele, sio siku tano watu walishanunua suti, wameshona sare, nk. Fedha zimeshatumika sana kwa ajili ya maandalizi na kuzuia sasa ni kuwapa watu ulaji tu.

Sisi Watanzania sio wajinga wa kudanganywa kirahisi kiasi hiki. Watu alishakula 60% ya tenda halafu unawaambia hakuna sherehe. Hizo hela utarudishaje? Mihemuko ya kisiasa ni kitu cha ovyo sana katika uongozi
 
Walicho mfanyia huyu mama s.mtaa wamepiga patakatifu

Dunia hii usimwani mtu
 
Tumeshuhudia maadhimisho ya sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika zikifutwa na marais Magufuli na Samia Suluhu Hassan wakiwa kama marais wa JMT. Je! Ni lini ambapo maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar yamewahi kutokufanyika kwa sababu kama hi zzz i zinazo tolewa!?

Tanganyika ilikwisha kupoteza hadhi yake toka 1964, bila ridhaa ya Watanganyika wenyewe. Walipelekeshwa tu kwa wakati huo na kisha kuambiwa Tanzania ndiyo Tanganyika, huku Zanzibar ikibakia na "identity" yake.

Watanganyika bado tuna "socialism hangover" huku watawala wana "enjoy" mvinyo mpya wa "capitalism"
 
Bajeti ya sherehe iliyofutwa ni shilingi ngapi?
Tusaidieni wazee wa Hansard.

Swali zuri hili ukute bajeti bilioni kadhaa! Mmh! Tunahitaji majibu/muongozo kwenye hili. Maana kama taifa stars ilikua m700 basi hizo sherehe zitakua zaidi.
 
Hamia Burundi. Pumbav
 
Hivi ile kizimkaz festivo bajet yake mliipata!
Futa na hizo samia marathon sjui samia blah blah zote hizo ni njiaa za kupiga tu

Ova
Subiri majibwa ya Chura kiziwi yaione post yako yatakavyobweka..
 
Maigizo tu hayo mbona hawataki wananchi watumie haki yao ya kuchagua na kuongozwa na viongozi wanao wataka.
 
Haya ni maamuzi mazuri aliyofanya Mh Rais Samia Suluhu Hassan, Kongole kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…