Rais Samia afuta sherehe za Uhuru, aagiza fedha zitumike kusaidia huduma za kijamii

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kufuta sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara na badala yake fedha zilizotengwa zitumike kusaidia huduma za kijamii.

Amesema fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii, huku akieleleza kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii, ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira kwenye maeneo ya kijamii kama masoko, hospitali, kumbi za wazee na wenye mahitaji maalumu.

Hayo yameelezwa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao kazi cha mawaziri kilichofanyika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. "Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za kitaifa".

Amesema Serikali inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika shughuli hizo, ili kujivunia sifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu.

"Ninatoa rai kwa wakuu wote wa mikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi kwa lengo la kuuenzi Uhuru wetu."
View attachment 3168740
Hizi wanaenda kigawana zote hakyamungu. Bora kama mwendazake alizipeleka kwenye mambo yanayopimika! Kufanya usafi na kuhudumia wazee, na kupanda miti? Serious tutapimaje hayo maswala? Hii pesa watu wanagawana Yote asubuhi ni mwendo wa dokezo na Saini feki tu!
 
Yaani nashindwa kuelewa kwanini kusema uhuru wa Tanganyika unaonekana kama mhaini unataka kupindua nchi sasa viongozi wakubwa wa juu kama hawa wanaogopa kusema Tanganyika then wanasema uhuru wa Tanzania bara,sielewi kwanini wanataka kulifuta jina la Tanganyika kwenye history ya hii nchi ya Muungano na kwa masilahi ya nani.
halafu ni kweli, kumbe ni sherehe za uhuru wa Tanganyika, kwahiyo rais ni rais wa Tanganyika, ama la na mapinduzi ya zanzibar yafutwe.
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kufuta sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara na badala yake fedha zilizotengwa zitumike kusaidia huduma za kijamii.

Amesema fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii, huku akieleleza kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii, ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira kwenye maeneo ya kijamii kama masoko, hospitali, kumbi za wazee na wenye mahitaji maalumu.

Hayo yameelezwa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao kazi cha mawaziri kilichofanyika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. "Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za kitaifa".

Amesema Serikali inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika shughuli hizo, ili kujivunia sifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu.

"Ninatoa rai kwa wakuu wote wa mikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi kwa lengo la kuuenzi Uhuru wetu."
View attachment 3168740
Hivi Tanzania ilipata uhuru kumbeee 🤔🤔🤔😀😀😀
 
Yaani nashindwa kuelewa kwanini kusema uhuru wa Tanganyika unaonekana kama mhaini unataka kupindua nchi sasa viongozi wakubwa wa juu kama hawa wanaogopa kusema Tanganyika then wanasema uhuru wa Tanzania bara,sielewi kwanini wanataka kulifuta jina la Tanganyika kwenye history ya hii nchi ya Muungano na kwa masilahi ya nani.
Wanajitoa ufahamu tu lakini ukweli utabakia kuwa usiku ule baada ya kushushwa Union Jack ilipandishwa Bendera ya Tanganyika hivyo ni ujinga tu kukwepa Historia
 
Attachments

  • UNION JACK.jpg
    UNION JACK.jpg
    32.5 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1702085740919.jpg
    FB_IMG_1702085740919.jpg
    1.6 KB · Views: 2
Safi sana. Huu ni uamuzi sahihi
Uwamuzi sahihi wa wapi? Unabadilisha matumizi ya pesa baada ya budget allocation tena iliyoidhinishwa na bunge? Hiyo ni auditing query kama hujui sasa.
Kwamba tangu bunge linakaa na kupitisha hiyo bajeti yeye alikuwa hajui hayo? Kwamba yeye yupo juu ya mhimili wa bunge?
Amka acha uzuzi " hiyo siyo good governance ni samia principles ambazo hushangiliwa na CHAWA
 
Samia principle iliyotokana na Magufuli Principle. Muwe na kumbukumbu mnapokuja na hoja za aina hii.
 
Tungefuta zile Safari au kupunguza delegation nadhani ingekuwa bora zaidi kuliko haya maigizo and by the way issue sio kufuta sherehe ni kupunguza matumizi mwanzo mwisho ila ndio hivyo...

1733319833989.png
 
Sherehe za Uhuru muhimu mno kufutwa ni dharau kwa jwtz

Tungefuta kwanza mbio za mwenye ambazo uteketeza mabilioni ya pesa bila tija ya msingi zaidi ya kuongeza ukimwi kwa vijana

Nategemea na mwakani serehe za mapinduzi na muungano kufutwa ili kupeleka pesa hospital!!!
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kufuta sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara na badala yake fedha zilizotengwa zitumike kusaidia huduma za kijamii.

Amesema fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii, huku akieleleza kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii, ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira kwenye maeneo ya kijamii kama masoko, hospitali, kumbi za wazee na wenye mahitaji maalumu.

Hayo yameelezwa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao kazi cha mawaziri kilichofanyika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. "Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za kitaifa".

Amesema Serikali inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika shughuli hizo, ili kujivunia sifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu.

"Ninatoa rai kwa wakuu wote wa mikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi kwa lengo la kuuenzi Uhuru wetu."
View attachment 3168740
Afute na ziara za kila siku. Pesa ipelekwe kwenye maendeleo
 
Ni maigizo tupu, kama ni maandalizi yameshafanyika kwa 90% sijui NEST ndiyo unakuja kufuta siku 3 kabla why usifute mchakato mzima tangu mwanzo?
 
Back
Top Bottom