Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Waziri ananusurika vipi ? Hii ni mwendelezo wa double standard .
Uwezi kusema mchuzi una chumvi nyingi alafu nyama isiwe na chumvi wakati vyote vimepikwa kwenye chungu kimoja.

Kilicho mnusuru waziri yeye si mtaalamu wa masuala ya Mahesabu hebu kapitie CV za Irene halafu katizame CV za Jenister baadaye akili yako itakufahamisha kwanini Irene alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa mifuko ya hifadhi, alafu utafahamu alishindwaje kurekebisha mahesabu, pia utajiuliza kwanini alikuwa msemaji na mtetezi mkuu ktk kuitetea hiyo 25% ilikuwa ni kwa manufaa ya nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo kanuni zilitungwa na Irene au wataalam wa wizarani?
Wataalam au niseme mwanasheria wa Wizara akishirikiana wadau huandaa kanuni. Sheria ni ya Wizara. Na mamlaka ni mdau wa kanuni na sheria. Kifupi Majukumu ya Wizara ni kuandaa sera, sheria, kanuni, miongozo, WARAKA n.k. Hapa sijui Mh. Waziri anakwepa vipi.
 
Unataka kuona matokeo? ??Basi subiri hitimisho. Executive summary ndiyo hiyo imetoka
Hotuba yake yote analalamika uwekezaji wa Dege Beach... Dege Beach..... Dege Beach

Amwite nyumbani Ramadhani Dau amweke lupango aliyejenga Dege Beach kama yeye mwanamme kweli asiye na mchezo na ufisadi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo kanuni ni copy and pest kutoka mfuko wa PPF wao walikuwa wana zitumia toka enzi ya Nyerere.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mahali nimeshauri wamtumie David Mattaka ambaye ndiye "Acturual" wa kwanza Tanzania kwa ushauri wa hayo mambo. Maamuzi mengine tutakwenda kutumia kodi kulipa mafao ya wastaafu badala ya michango yao
 
Watu wote walishirikishwa vyama vya wafanyakazi vilishirikishwa? Unajua waliomponza mpaka zigo likamuangukia ni akina nani? Ogopa workers unions Ktk masala ya maamuzi kuhusu maslahi yao hali ya hewa inaweza ikachafuka maramoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
vyama vya wafanyakazi vya tanzania havijawahi kusimamia hata mara moja maslahi ya wafanyakazi wa Tanzania, kwenye swala la kikotoo walishirikishwa mwanzo mwisho sema baada ya kusikia kelel za wafanyakazi ndio na wao wakaibuka ningewaelewa kama wangepiga kelele toka mwanzo lakini iliwachukua muda mrefu kueleza misimamo yao kwa kifupi hawana tofauti na wanasiasa hata matumizi mabovu ya mifuko ya hifadhi ya jamii katika hiyo mifuko kuna wawakilishi wa wafanyakazi kwenye bodi ya hiyo mifuko lakini jiulize kwanini bado mifuko inafuja pesa za wafanyakazi.
Hiyo miradi anayolalamikia rais mingi ilifanyika wakati mkurugenzi mkuu wa NSSF akiwa Ramadhani dau lakini rais amempa ubalozi, tumia kichwa chako kuchambua mambo usisubiri kuchambuliwa
 
vyama vya wafanyakazi vya tanzania havijawahi kusimamia hata mara moja maslahi ya wafanyakazi wa Tanzania, kwenye swala la kikotoo walishirikishwa mwanzo mwisho sema baada ya kusikia kelel za wafanyakazi ndio na wao wakaibuka ningewaelewa kama wangepiga kelele toka mwanzo lakini iliwachukua muda mrefu kueleza misimamo yao kwa kifupi hawana tofauti na wanasiasa hata matumizi mabovu ya mifuko ya hifadhi ya jamii katika hiyo mifuko kuna wawakilishi wa wafanyakazi kwenye bodi ya hiyo mifuko lakini jiulize kwanini bado mifuko inafuja pesa za wafanyakazi.
Hiyo miradi anayolalamikia rais mingi ilifanyika wakati mkurugenzi mkuu wa NSSF akiwa Ramadhani dau lakini rais amempa ubalozi, tumia kichwa chako kuchambua mambo usisubiri kuchambuliwa
Mkuu kama uko karibu na kwa Mangi
Agiza novida napitisha hela, we nitaje tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Dkt amekaa pale muda mrefu sana na hakuweza kutoa ushauri au kukataa miradi mibovu yenye harufu ya 10% mfano ile ya Kigamboni na majengo mengi yaliyojengwa na Mifuko isiyo na tija. Hata jana wakati wachangiaji wote walikuwa wanamaddress Mhe. Rais yeye anamdress Rais kama Mhe. Mwenyekiti. Huu ni utovu wa nidhamu. Alilewa madaraka.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isaka.

Mapema leo Rais Magufuli alifanya kikao cha wazi na Viongozi waTUCTA, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA) kujadili masuala yahusuyo Mafao ya wafanyakazi hususani KIKOKOTOO na Rais Magufuli alifikia hitimisho kwamba Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika).
Pia soma
> Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika) - JamiiForums

Irene Charles Isaka, Director General, Social Security Regulatory Authority - JamiiForums
Mbona taarifa zinasema atapangiwa kazi nyingine
 
Nieleweshe kosa la Irene Kisaka ni lipi?
Baada ya kikao Rais alibaini kuwa walio kuwa wanamshauri akiwemo huyu Irene kuhusu Kikokotoo walikuwa wanampotosha sasa alipata ukweli kutoka kwa wahusika ndio maana aliamua kumtengua maana alipata ukweli halisi
 
Ubaya wa fitina, malipo hapa hapa. Hii nafasi ilikuwa Carine, wakamfitini.
 
Hivi kanuni hutungwa na nani? CEO wa SSRA ataondokaje kwenye nafasi halafu waziri, mwanasheria mkuu, wa shirika na wizara wabaki salama?

Huyu mama yeye si alikuwa anasimamia kanuni tu ambazo zimetungwa na wizara wakishirikiana na ofisi ya AG....??
 
Kama unapata shida kuona kosa lake ngoja nikupe mfano huu: Umempa mkandarasi mkataba wa kujenga nyumba. Baadae ukakabidhiwa nyumba yako na kuichukua. Baada ya siku mbili nyumba ikapasuka ufa! Je mkandarasi hatawajibika kwa sababu tu wewe ulikubali kuipokea ile nyumba?
Inategemeana Mkataba mumeufunga vipi, kwa mfano kama mulikubaliana baada ya kumaliza kazi Nyumba litakuwa chini ya uangalizi wake kwa muda wa miezi 6 na Ubovu wowote utakaotokea utakuwa juu ya Fundi yaani arekebishe, na Fundi atawajika ndani ya kipindi hiko tu baada ya kipindi hiko cha miezi 6 kuosha hapo Mwenye nyumba utahusika.
 
Mnyika ndo amefanya kazi, kawaida sheria husainiwa na rais na nadhani rais aliipitisha tuu akizani ipo sawa kumbe sio. Kumbuka hili sakata limetrend sana kwenye mitandao ya kijamii na hadi linapitishwa yeye alikuwa wapi muda huo wote. Wakati anfingua barabara ya kimara mnyika ndo alimpa challenge kwa mara ya mwisho.
Nadhani alienda kujifikiria na kuona akina mnyika wako sahihi, lakini kutufanya mazuzu anatumbua mkurugenzi wa SSRA, hapo anachotaka kukifanya nazani ni ku exchange madaraka ya watumishi wawili.
 
Back
Top Bottom