Rais Magufuli amtembelea Maalim Seif, Serena Hotel

Ndo unapoona wanasiasa wanatumia mtaji wa walalahoi kujinufaisha.

Why serena hotel? ina maana huku bara hana nyumba? kama hana au anayo kweli haiwezekani akakaa hotel ya bei ya kawaida tu kuokoa pesa hizi za walalahoi?

Hawa walalahoi wakitoka kutibiwa tu kesho yake wanatakiwa mzigoni. I never trust mwanasiasa. They always use citizens as a ladder to climb up to their ambitions. Ninyi mnabaki hapa mnajiita TEAM MAFINDO FINDO WENZENU WANAKULA LIFE TU.

Shauri zenu mnatokwa na mapozi hadi mishipa ya kichwa kusimama mkishabikia watu kadhaa ambao mmewachagua wao wawe na maisha bora kwa niaba yenu
 
Ao ndio wanasiasa,wao wanakula maisha nyie uku mnagombania mafupa na makombo!ona wanacheka,ila nyie humu mnafura kwa hasira...dah
wanauana huko visiwani wanachomeana nyumba na kunyoosheana vidole..kiuhalisia wenzao huku wanalipiana ma five star hoteli..
 
Imetokea na p engine hata sasa Viongozi / Maofisa Wakuu walikosa / wanakosa nyumba za umma wakaishi / wanaishi hotelini wakiwa na Familia na kuitia serikali gharama kubwa!
 
Kumbe hata hujui kua ni kodi zetu watanzania ndio zinagharamia marudio ya huo uchaguzi ambao kutokana na ubinafsi wake kauvuruga? kwani ni lazima yeye tu awe rais pale zanzibar, kwamba asipokua yeye uchaguzi haukua wa huru na haki?
Huo unafiki a cha. Ccm lini mmekuwa name uchungu na kodi za waTanzania!? Hiyo Znz kwani lazima mtawale ninyi!?
Wewe
 
Ukiwaangalia usoni kwa makini wote wawili kuna kitu unakiona,,,najaribu kufikiria je hawakuongea chochote kuhusu yanayoendelea Zanzibar? Kama jibu ni ndio, kwanini?!
 
JPM , sijakupa kura lakini sasa nakukubali.

Kiongozi mzuri daima huwa anaonesha njia. Moses aliwaongoza wana waisrael kutoka utumwani na kuwa peleka kwenye " promised land" sio kwa fimbo ya chuma lakinikwa maneno matamu na vitendo vya utu na uungwana.

Kwa hili na kupa tano. Kama kuna uchaguzi wa marudio kura yangu unayo!
Nitaungana nawe, siku atakayokwenda kumpa pole mke na watoto wa Hayati Mawazo!
 
Ameenda kujikomba alishasema mambo ya zanzibar hayamhusu sasa anaenda kumuona ili iweje!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom