Rais Magufuli amtembelea Maalim Seif, Serena Hotel

hapo serena anatumia pesa ya nani? CUF JMT au ya kwake?

Deni la yeye kukaa Hotel Raisi Magufuli kasema ataangalia litalipwaje ili apone haraka.Hajasema JMT italipa msije kumzushia.Mimi niko tayari kumchangia shilingi elfu moja kulipia chumba anacholala Seif Shariff Hamad maana naona UKAWA wamemtelekeza mzee wa watu
 
JPM kasema deni watalipa serikali angalia mwisho wa clip hio

Hajasema deni litalipwa na serikali kasema tutaangalia lilipwe.Yaweza kumaanisha kuwa ataongea na raisi Shein wa Zanzibar au atatafuta vyanzo anavyojua mwenyewe hata kukuchangisha wewe.Usimzulie kabisa.Hajasema serikali ya muungano itatoa.
 
Kwa ndege kwenda zanzibar ni dakika 25.Baada ya kulazwa, alipopewa discharge alitakiwa kurudi kwao.Wangemtumia nauli hata ya boti SAA MOJA TU ANGEKUWA KAFIKA KWAO KWENYE NCHI YAKE.
Hivi hapa unahoja au unajifurahisha? Kama ungesoma vizuri na ukakijua chanzo cha ugonjwa kama walivyoeleza madakatari usingepata uthubutu wa kuandika shairi la KIsonge
 
Ao ndio wanasiasa,wao wanakula maisha nyie uku mnagombania mafupa na makombo!ona wanacheka,ila nyie humu mnafura kwa hasira...dah
 
Wacha unafiki hasara gani aliekutia wewe. Nafasi kubwa ya kuvuruga uchaguzi anayo Jecha!
Kumbe hata hujui kua ni kodi zetu watanzania ndio zinagharamia marudio ya huo uchaguzi ambao kutokana na ubinafsi wake kauvuruga? kwani ni lazima yeye tu awe rais pale zanzibar, kwamba asipokua yeye uchaguzi haukua wa huru na haki?
 
Ao ndio wanasiasa,wao wanakula maisha nyie uku mnagombania mafupa na makombo!ona wanacheka,ila nyie humu mnafura kwa hasira...dah

Siasa ni kama DEBATE tu mashuleni.Mkianza mnajigawa darasani makundi mawili.Mnajigawa kwa hiari.Wengine wanakuwa upande wa NDIYO wengine upande wa HAPANA (opposition).Debate ikiisha mnaendelea na darasa kama kawaida.

Siasa pia ni kama timu ya mpira.Ikitaka kufanya mazoezi ikiwa peke yake inajigawa mara mbili wengine wanakuwa upande wa goli lle wengine upande wa goli lingine.Mnacheza weeee mkimaliza mchezo mnatulia kama timu moja mnaendelea na timu.

Tatizo mashabiki ndio watajijua DEBATE ikiisha wao wanaendelea kujadili nani kashinda mchezo ukiisha wao wanaendelea kujadili
 
Magufuli aache unafiki. Si Alisema ya Zanzibar hayamhusu?
Kwani Maalim Seif ni Zanzibar au Rais Magufuli ameenda kuongelea suala la Zanzibar?

Nakumbuka wakati ukiwa unapigia chapuo CCM, comment zako mara nyingi zilikuwa zimejaa hekima na busara! Tangu uingie kwenye kikundi cha Ulipo Tupo na Timu Lowassa, hata common sense imepotea kwenye comment zako nyingi!

Hainishangazi sana kwa sababu hata binadamu anapobadilisha dini ukubwani mara nyingi huwa wanakuwa radical and sometimes nonsensical way of thinking!

Ulipo Tupo at its best!
 
Kwa ndege kwenda zanzibar ni dakika 25.Baada ya kulazwa, alipopewa discharge alitakiwa kurudi kwao.Wangemtumia nauli hata ya boti SAA MOJA TU ANGEKUWA KAFIKA KWAO KWENYE NCHI YAKE.
Muwe na uelewa kidogo
Kupanda ndege sio raha ndio maana hata wakinamama wajawazito hawapandi
Mh Seif katoka Hosp inategemea daktari ameshauri nini
Pia ikumbukwe Maalim si mkzii wa Dar....ni kama mfano useme Mzee Kinana akiwa Unguja ni lazima akae Hotelini
Mnajaza server kwa hoja zenu zisizo na mashiko...na kuonyesha ufinyu wa general knowledge....sometimes kunyamaza ni busara
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom