Rais Jakaya Kikwete analipwa mshahara na posho kiasi gani? na analipa kodi kiasi gani?

Hata yeye hajui mshahara wake,tangu ameingia madarakani cjui kama amewai pokea mshahara,Bongo maisha kimjinimnjini hadi magogoni.
 
Sasa kama hali iko hivi, hata asipolipwa chochote ana hasara gani?

That is my point, mshahara kwake wala siyo ishu kubwa. Na unaweza hata kutajwa hapa na mkashangaa kwamba ni mshahara wa kawaida sana!
 
Salaam wakuu,
Kati ya mwaka 1986/87 niliwahi kusoma kwenye gazeti fulani wakati huo, bila shaka lilikuwa gazeti la Mfanyakazi, ya kuwa mshahara wa Rais kwa wakati huo ulikuwa umepanda kufikia takriban shilingi 900,000/= kwa mwezi (Sina hakika kama hii ilikuwa inajumuisha marupurupu mengine ama la).

Kwa wakati huo nakumbuka kima cha chini cha mshahara wa mtumishi wa umma kilikuwa hakizidi shilingi 5,000/= (wale wenye umri kama wangu au walionizidi watakumbuka).
Hii ina maana kuwa, uwiano kati ya mshahara wa mtumishi wa umma wa Kima Cha Chini (KCC) na ule wa Rais kwa wakati huo ulikuwa 1:200.
Kwa maneno mengine Mshahara mmoja wa Rais ulikuwa na uwezo wa kuwalipa watumishi wa umma wa KCC wapatao 200 hivi.

Mshahara wa sasa wa wa mtumishi wa umma wa KCC ni takriban shilingi 150,000/=.
Kama tutachukua uwiano wa mshahara wa mtumishi wa umma wa KCC dhidi ya ule wa Rais kwa mwaka 1986/87 ambao ulikuwa 1:200, ina maana tukadirie kuwa mshahara wa sasa wa Rais haupungui shilingi 30,000,000/= (shilingi za kitanzania milioni thelasini).

Je ni kweli mshahara wa Rais kwa sasa unakaribia au unavuka shilingi milioni 30?
Kama hapana:
1. MSHAHARA WA RAIS KWA SASA NI KIASI GANI?
2. UNAJUMUISHA MARUPURUPU GANI?
3. ANALIPA KODI KIASI GANI?
4. ANAKATWA PENSHENI KIASI GANI
5. KUNA MAKATO MENGINE YOYOTE YA ZIADA?

Nawasilisha.
 
Milioni 30 ni pesa nyng ukizitiza lakini alipwe tu maana ana STRESS huyo? Muda wake uliobaki anaona decade aisee...
 
Jaman mm nina swali hv huyu rais we2 anachukua mshahara kama Tsh. Ngapi hv, akifuatiwa na makamu wake then w/mkuu. Msaada plz.!
 
Lazima Zitakuwa hela nyingi sana, Just Imagine kama anawaleta akina Maksimo na Babu na anawalipa Milioni 15-20 unafikiri yeye anajilipa sh ngapi????.Haiwezi kuwa milioni 30. CHANGANYA NA ZAKO
 
Mara utasikia Rais katoa Million kadhaa msaada wa kujengea shule, kweli hiyo fedha yote hiyo inatoka kwenye mshahara wake au ni Hazina nasi tunapigwa changa la macho tu? kwa nini hawaigi michango aliyokuwa anatoa mwalim Nyerere ambayo kama ni ujenzi basi yeye alikuwa anapiga chepe masaa kadhaa na vibarua then anaondoka, sikuwahi sikia Nyerere eti katoa shillingi kadhaa kwa ajili ya ujenzi wa Shule, Zahanati, Josho, Visima etc na bado kulikuwa na mwitikio mkubwa sana wa maendeleo ukilinganisha na hivi sasa, hivi watu hawa hawajui kuwa Nyerere alishasema kuwa fedha si msingi wa maendeleo? kwa kifupi Rais hata alipwe 50 million hawezi saidia au kumaliza matatizo ya wadanganyika, anapodanganya kuwa anawalipa hao kina Maximo ni uongo uliojificha ndani ya hiyo giriba ya kuficha mshahara wake wakati kuna wafadhili haramu nyuma ya pazia kama kina Barrick
 
wamarekani wote wanajua ni wajibu wao kulipa kodi, je wabongo wangapi wanalipa kodi. Jifananishe na kenya wewe sio kurukia america.


unanisikitisha ndugu yangu! Ina maana hujui bidhaa yoyote mtanzania anayonunua anailipia kodi?au wewe wajua wanaolipa kodi ni wafanyakazi tu wanaokatwa moja kwa moja (direct tax) kwenye mishahara yao....
 
Sawli zuri sana hili..isiwe kwa JK iwe kwa kila Rais wa JMT...analipwa kiasi gani ni muhimu tukafahamu..na kodi anakatwa kiasi gani..
 
Hey! haya mambo kwe2 bongo si sawa na US ambako sheria zao kidogo zipo vizuri sana,but hapa kwetu sheria imespecify baadhi ya mapato ambayo hayakatwi kodi ikiwemo kipato cha raisi,ukiicheki sheria yetu
(THE INCOME TAX,ACT 2004)

SECOND SCHEDULE

EXEMPT AMOUNTS

(Made under section I 0)

"1. The following amounts are exempt from income tax -
(a) amounts derived by the President of the United Republic or the President of
the Revolutionary Government of Zanzibar from salary, duty allowance and
entertainment allowance paid or payable to the President from public funds
in respect of or by virtue of the office as President;
"...............................So cha msingi ni kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria ze2 hapa TZ,coz nyingine zimepitwa na wakati,na nikandamizi sana,otherwise huwezi kujua raisi anakatwa kiasi gani cha kodi ktk mapato yake,na kama ingejulikana ni kiasi gani raisi analipa kodi by just a simple calculation ungeweza kuelewa mshahara wake ni kiasi gani
 

duh! Imenibidi niende kusoma hii! Ni aibu. Kumbe na wabunge nao hawalipi kodi kwenye kile kiinua mgongo cha Tsh25 mil! Huu ni wizi!
 
Kwa nini wasilipe kodi? na wao wanatumia services ambazo kodi zetu zinatumika? Huu ni ubaguzi wa wazi kabisa! Watz tudai wajibu wa kulipa kodi kwa watz wote. Sisi tunafanya kazi ngumu tunalipa direct tax wao wanafanya kazi zisizokuwa na performance appraisal hawalipi direct tax! Hii imekaa vibaya,tuirekebishe.
 

Mimi nilisema kuwa Africa was not ready for independence! Vitu kama hivi vinadhihirisha hii kauli. Wakati Obama analipia hadi msosi wake kule White House, sisi tunampa rais tax freedom...hahaha! Inaelekea hatujui maana ya tax kwanza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…