Mwita25
JF-Expert Member
- Apr 15, 2011
- 3,831
- 1,168

Wafanyakazi wote TOL watimuliwa kazi!

What does it have to do with the original topic? Au umekurupuka usingizini?

Wafanyakazi wote TOL watimuliwa kazi!

Mshahara wa Rais wako unataka kuujua ili iweje? Hilo siyo suala la kutangazatangaza ovyo tu kwasababu linaweza kuharibu usalama wa taifa. Lazima tuwe na heshima kidogo kwa mambo ya kitaifa.
wamarekani wote wanajua ni wajibu wao kulipa kodi, je wabongo wangapi wanalipa kodi. Jifananishe na Kenya wewe sio kurukia America.
kwanini msiseme mshahara wa rais tu. Kuna haja gani mpaka msipecify? au ndo maana hamkuuliza wa ben, ali na julias?
I doubt ni hii asking yenu. Nitahoji baada ya JK kutoka madarakani.

Mishahara ya viongozi wakubwa wote ni siri,sababu za kiintelijensia.Mapato ya Rais kwa mwaka ni makubwa mno.........labda katiba mpya ikipatikana itatusaidia kufumbua hilo fumbo.

Mshahara wa Rais wako unataka kuujua ili iweje? Hilo siyo suala la kutangazatangaza ovyo tu kwasababu linaweza kuharibu usalama wa taifa. Lazima tuwe na heshima kidogo kwa mambo ya kitaifa.
Mshahara wa Rais wako unataka kuujua ili iweje? Hilo siyo suala la kutangazatangaza ovyo tu kwasababu linaweza kuharibu usalama wa taifa. Lazima tuwe na heshima kidogo kwa mambo ya kitaifa.
Sasa unataka ili nini wewe mshahara wako mbona mkeo haujui hebu tokeni hapa ....................badala ya kuzungumzia jinsi gani utajiendeleza uinue kipato unataka uujue ili ? hivi CDM kwanini katibu mkuu mwingine hata pewa mshahara na marupurupu mengine kama slaaaaaa?????
Acheni utani basi kwenye ishu serious! Ni vyema mwananchi kujua mkuu wa nchi anapata kiasi gani toka kwenye jasho la watu wake na yeye anachangia kiasi gani kwenye jasho hili. Pia ningeshauri mishahara ya watumishi wote wa umma iangaliwe kujua kama kweli inakidhi mahitaji yao ili kupunguza ubadhirifu kwenye fedha za umma! Haiingii akilini Serikali inamlipa mtumishi wake laki tatu ambapo mtumishi huyu anaishi Dar es Salaam, ana familia (labda watoto wa3), amepanga, anawasomesha watoto, anajigharimia matibabu, analipa kodi, familia inakula, anasafiri kila siku kwenda na kurudi kazini, anachangia shughuli za kijamii na mambo mengine kibao. Je serikali imeshawahi kufikiria na kuainisha ni jinsi gani mtumishi huyu anavyopangilia matumizi ya huu mshahara? Kama bado basi serikali ijue wazi kuwa hili lina mchango mkubwa kwenye ufisadi na ufanisi duni wa sekta ya umma! Matokeo ya hili ni watumishi kuwepo kazini lakini ukweli hakuna wanachofanya huku serikali nayo ikijifanya inalipa mishahara ambayo haina tija yoyote kwa huyu mtumishi. Wanajamii, tulijadili hili kwa kina ili kuona mustakabali wa taifa letu unaelekea wapi.....analipwa laki tatu mshahara sawa na tichaaaa.
Wananchi tuna haki ya kujua mshahara na mapato ya raisi wetu, na Je analipa kodi kiasi gani? Obama anaweka mambo yote hadharani je sisi tunaficha nini? kwa nini mshahara wa raisi uwe siri wakati ni raisi wetu na tumempa ikulu yetu sasa kwa nini tusijue mshahara wake?
Kwa mujibu wa Jedwali la Pili la Sheria ya Kodi ya Mapato.........
EXEMPT AMOUNTS
(Made under section 10)
1. The following amounts are exempt from income tax -
(a) amounts derived by the President of the United Republic or the President of the Revolutionary Government of Zanzibar from salary, duty allowance and entertainment allowance paid or payable to the President from public funds in respect of or by virtue of the office as President;
Sasa kama hali iko hivi, hata asipolipwa chochote ana hasara gani?Niliwahi kuambiwa kwamba mshahara anaolipwa Rais wa JMT ni mdogo kuliko mshahara anaokuwa analipwa Maximo, yule kocha wa Taifa Stars. Na wala siwezi kushangaa kusikia hivyo. Wanaweza kuuanika mshahara wa rais hapa na wote tukashangaa kwamba ni mdogo sana, na kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato, rais hatakiwi kulipa kodi kutoka kwenye mshahara wake.
Lakini kumbukeni kwamba kwenye bajeti iliyopitishwa na Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, ofisi ya Rais imetengewa Shs. 135 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kitaifa/mbalimbali. Pesa hizi Mnyika alizihoji Bungeni lakini hakupewa ushirikiano wa kutosha toka kwa Wabunge wa Magamba. Fungu hili Rais anaweza kulitumia atakavyo, na kwa mujibu wa sheria, fungu hili huwa halikaguliwi na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali!