Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,153
10,825
1.Wakati Tanzania bara wanafukuza wamachinga hovyo na kuwarudisha nyuma kimaendeleo, upande wa Zanzibar Rais Mwinyi amewapa vitambulisho na kuwapa uhuru wa kupiga kazi masaa 24.

2. Wakati Tanzania bara Makamba akipandisha bei ya kuunga umeme mpaka zaidi ya laki 9, upande wa Zanzibar Rais Mwinyi ameshusha gharama ya kuunga umeme mpaka laki 2 tu kwa mtu ambaye hana nguzo.

My take.
1. Smartphone zimeondolewa VAT ili zishuke bei na watanzania wengi wanunue na serikali ikate tozo, kwa nini wasishushe bei ya kuunga umeme ili wakate tozo pia?

2. Serikali inatoa elimu bure kwa nini umeme ishindwe?

3. Serikali inatoa mikopo vyuo vikuu?

4. Serikali inakusanya kodi ya majengo kupitia Luku.

Hiyo serikali imewezaje yote hayo alafu ishindwe kushusha bei ya kuunga umeme?
 
1.Wakati Tanzania bara wanafukuza wamachinga hovyo na kuwarudisha nyuma kima endeleo ,upande wa Zanzibar Rais Mwinyi amewapa vitambulisho na kuwapa uhuru wa kupiga kazi masaa 24.

2. Wakati Tanzania bara Makamba akipandisha bei ya kuunga umeme mpaka zaidi ya laki 9, upande wa Zanzibar Rais Mwinyi ameshusha gharama ya kuunga umeme mpaka laki 2 tu kwa mtu ambaye hana nguzo.
Wote hao ni wazanzibar warudi kwao
 
Nyie midomo payu hapa tz aje rais wa aina yoyote kelele ni zile zile, kuanzia nyerere walitaka kumpindua, mwinyi mkapiga kelele hafai mlaini sana, mkapa fisadi kelele lungo, kikwete ndio hadi watoto wadogo wakawa wanamtukana, magufuli ndio balaa sasa ni samia atatoka atakuja mwingine mwendo ni huo huo. Ila kelele zote hizo ni kwamba mnakuwa mmeguswa maslahi yenu na wala si maslahi ya taifa. Poleni sana
 
Watanzania watu wa ajabu sana, unataka uungiwe umeme kwa elfu 27..gari ya Tanesco iwekwe mafuta, wafanyakazi walipwe na wewe utoe elfu 27.

Hivi ile remote feeder ya units yenyewe tu pesa ngapi?

Na hapo hutaki kusikia deni la taifa linaongezeka..

Machinga anachukua bidhaa anaenda kuuzia mbele ya fremu ya mtu, halipii fremu, halipi VAT, halipi leseni, halipi usafi, halipi Zimamoto, hana bili ya umeme wala maji..na wewe unaona sawa tu hiyo hali iendelee.

Ifike mahali tuwe serious tunataka nini

Zanzibar wameshusha umeme mpaka laki mbili kwa wale wasio na nguzo na bado unafanya comparison na elfu 27??
Hivi Zanzibar ina watu wangapi?? Kimsingi yote ilipaswa kuwa na umeme toka enzi za Sultan
 
Watanzania watu wa ajabu sana, unataka uungiwe umeme kwa elfu 27..gari ya Tanesco iwekwe mafuta, wafanyakazi walipwe na wewe utoe elfu 27..
Hivi ile remote feeder ya units yenyewe tu pesa ngapi...
Kuna maelfu ya watu wameungwa umeme kwa elfu 27 hata mimi nimeunganishiwa umeme kwa elfu 27.

Kumbuka Tanesco wanakusanya rundo la kodi pale unaponunua umeme ya kifupi ni kwamba kuunganishia umeme ilitakiwa iwe bure au bei chini sana kama mtu anapofungua akaunti ya bank au anaponunua laini ya simu
 
Hayo makato ya luku yanachukua miaka mingapi kutosha kulipia nguzo moja ya umeme?? Je nguzo ina life time ya miaka mingapi??

Hayo makato yanachangiaje kwenye bei ya transfoma?? Mafuta ya transfoma?? Wire??..n.k

Na bado ukiona shoti kidogo tu unapiga emergency Tanesco..unadhani wanaweka mafuta kwenye gari na kusaga tairi kwa ileile elfu 27?? Na hapo hawajalipwa overtime!!

Tafakari kidogo
Kuna maelfu ya watu wameungwa umeme kwa elfu 27 hata mimi nimeunganishiwa umeme kwa elfu 27.

Kumbuka Tanesco wanakusanya rundo la kodi pale unaponunua umeme ya kifupi ni kwamba kuunganishia umeme ilitakiwa iwe bure au bei chini sana kama mtu anapofungua akaunti ya bank au anaponunua laini ya simu
 
Back
Top Bottom