Polisi Moshi yazuia jeneza la mwili wa Ndesamburo kupitishwa barabarani

That is too much kwanini Chadema mnapenda kutafuta lawama na serikali. Huyu mzee wetu ameshafariki kwa kumheshimu na kumuenzi fateni taratibu za kidini kumzika. Mnapenda kutafutia serikali lawama and then mmpate huruma kutoka kwa wananchi. Kutafuta umaarufu wa chama sio kwenye misiba.
Hata nyerere alitembezwa mitaani pia,
 
Wachagga mbwembwe hadi kwenye kifo jamani! Eti mwili utembezwe mtaani for what??

Nimecheka sana eti wanatangaza jeneza limetoka Nairobi lina thamani kati ya $2000 mpaka $10000 utadhani akizikwa humo haozi..!
Mchaga hachagui kwa pa kuonyesha mbwembwe maana uwezo wanao, unashangaa jeneza? Ivan kazikwa na hela, acha wivu mkuu, wachaga msiba kwao ni shererhe ndio maana kuna kula, kunywa na mziki pia haukosi!
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi wa Moshi limezuia utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa kuutembeza katika barabara za viunga vya manispaa hiyo, mwili aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, marehemu Philemon Ndesamburo .

Majibu ya barua yaliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Polisi Moshi, yamezuia mwili huo kupitishwa katika barabara za kati kati ya mji kwa kile walichoeleza kuwa leo Juni 5 na siku ya kazi na kuna shughuli za mbalimbali zinazoendelea.

Sababu ya pili iliyotolewa na ofisi hiyo ni kwamba wakiupitisha mwili huo barabarani watasababisha msongamano mkubwa ambao utakuwa chanzo cha usumbufu kwa watumiaji wengi wa barabarani.

“Ofisi ya Mkuu wa polisi wa wilaya inatoa maelekezo kuwa mwili wa Ndesamburo ukitolewa KCMC, upitishwe barabara ya YMCA kupitia Lucy Lameck Road hadi uwanja wa michezo wa Majengo ambapo kumepangwa kufanyika kwa shughuli zote za kutoa heshima za mwisho.

Jana mmoja wa wanakamati ya mazishi ya Ndesamburo, Anthony Komu aliliambia Mwananchi kuwa mwili wa Ndesamburo utachukuliwa KCMC saa 4 asubuhi na kupitishwa katika barabara kuu za mji wa Moshi ili kuwawezesha ambao hawatapata nafasi ya kufika Majengo, kuuaga mwili huo.
Sitaki

Sitaki kuamini kuwa watanzania tumefanywa vipofu na wavivu wa kufikiri namna hii, chuki zisizokuwa na msingi na kushindwa kutumia akili kumetawala maisha yetu na tumegeuzwa kuwa tishu za wanasiasa ambao wanajitafutia ulaji kwa kutumia saikolojia zetu, mtanzania mwenzangu jiulize

Kuna haja gani ya msiba kupitishwa mitaani kama kweli wananchi wanahaja ya kuaga? Kwanini watu wasiende eneo la kuagia na kutoa heshima zao za mwisho kuliko kufanya kama kuwalazimisha? Kunatengenezwa hoja gani hapo, kwamba mitaa yote watu walijaa kumuaga Ndesa ili iweje?

Nilini watanzania tutaacha kutumia misiba kwa manufaa ya kisiasa? Mtu ameshafariki kila mtu anataka afanye yake msibani kujionyesha si mfanye kazi ktk maeneo yenu watu wawaone kwa utenfaji wenu?

Kama sio kufilisika kimawazo ni nini kumuingiza Gambo kwenye mazishi ya Ndesamburo wakati ana mkoa wake mnataka kuaminisha umma kuwa mkoa wa Kilimanjaro una viongozi wanaoshikiwa akili na watu wengine na kwamba nafasi walizonazo haziwatoshi au?

Hebu fikirieni kama watu wenye akili sio kila kitu lawama lawama tu muacheni mzee wa watu akapumzike amemaliza safari yake hapa duniani amefanya makubwa na mengi kwa nchi yake, chama chake na jamii yake hayo mnayotaka kufanya kupitia yeye yawekeni akiba mkifa nyie yatafanyika kama ndio njia itakayowafikisha mbinguni. Pumzika kwa amani babu NdesaPesa.
 
Back
Top Bottom