Picha kutoka gazeti la Mambo Leo la mwaka wa 1934. Watazame Mangi waliopambana na Rajabu Kirama - Mangi Ngilisho na Shangali

Sources of historical information ni pamoja na archives,documentations,historical sites,oral tradition ambayo ndani yake kuna folktales...Si lazima tuwe na njia moja ya kupata jambo fulani la kihistoria.Ukipata kwa njia ya documents mwingine anapata kwa njia ya oral tradition.

Ukilitoa jambo hadharani na kuliandika katika forums maanake unafungua mijadala,kila mtu anajadili kwa kadili ya uelewa wake,ni ajabu kijimilikisha historia ya mahali fulani au kuona cha mtu fulani si sahihi ila chako tu ndio sahihi.Historia haijawahi kuwa mali ya mtu,bali ni urithi wa vizazi unaorithishwa kwa njia mbalimbali kama vile simulizi na maandishi.

Ninayaandika niliyosimuliwa na wazee wenye "authority" ya historia ya eneo husika,unaandika uliyosoma katika documents,moja ya athari ya historia hasa katika uandishi na usimuliaji,ni ushawishi wa msimuliaji na mwandishi kutaka kusimulia kile tu anachoona kwake kina manufaa.Mjadala si sumu,ni njia ya kukubali kuwa tunaweza kujifunza hata kutoka kwa wale walio wakimya lkn wenye kujua mambo mengi....A jack of all trade is a master of None
Barufu,
Sina tatizo na hayo yote uliyosema.
 
Ni kweli wakati wa harakati uhuru wa Tanganyika paliwahi kutokea mgogoro na hawa Mangi ambao baadhi yao hawakutaka kusikia uhuru wa Tanganyika bali walitaka uhuru wa Wachaga peke yao ?

..hizi habari za Wachaga au Mangi kudai uhuru wa Wachaga peke yao siyo za kweli.

..kulichotokea ni kwamba Mangi mkuu alikuwa akipingwa na wasomi wa Kichaga ambao walikuwa wanataka Chaga Council iongozwe na mtu yeyote mwenye sifa na siyo kulazimisha watu toka uzao wa Mangi. Wasomi hao pia ktk siasa za Tanganyika walikuwa wamejiunga na chama cha Tanu, na hali hiyo ndiyo iliyosababisha kuonekane kuwa na mgogoro kati ya Mangi Mkuu Thomas Marealle na Tanu.

..Lingine ni kwamba kulikuwepo na Mangi kama Abdieli Shangali wa Machame ambaye alikuwa anawaunga mkono vijana wasomi waliokuwa wakimpinga Mangi Marealle. Mmoja wa wanachama wa Tanu ambaye alikuwa mstari wa mbele ktk harakati hizo ni Solomon Eliufoo ambaye alikuja kuwa Waziri ktk serikali za Tanganyika na Tanzania baada ya uhuru.
 
Kyalow,
Mavazi yanakwenda na utamaduni wa jamii husika.

Kuvaa kaniki kwa akina mama au msuli kwa wanaume si udhalili.

Angalia picha hiyo hapo chini ya babu zangu wamepiga mwaka wa 1933 siku ya ufunguzi wa ofisi ya African Association, New Street Dar es Salaam:

View attachment 1676833
Kipindi picha inapigwa ndiyo kwanza Mwalimu Nyerere ndio kwanza ana miaka 11.
 
Kipindi picha inapigwa ndiyo kwanza Mwalimu Nyerere ndio kwanza ana miaka 11.
Ferru...
Katika picha hiyo na waliokuwa hai kipindi hiko wako wazalendo wengi walioshuhudia mabadiliko ya TAA na kuundwa kwa TANU mwaka wa 1954.

Katika picha hiyo yuko Ramadhani Mashado Plantan ambae kaka zake wawili walishiriki katika siasa za TAA.

Mwalimu Thomas Saudtz Plantan alikuwa Rais wa mwisho wa TAA katika kizazi cha Wajerumani na uongozi wake ulipinduliwa mwaka wa 1950 na vijana wa enzi za Waingereza wakiongozwa na Abdulwahid Sykes.

Schneider Abdillah Plantan yeye aliungana na vijana katika kuutoa madarakani uongozi wa kaka yake Thomas Plantan.

Ramadhani Mashado Plantan yeye alikuwa mmiliki na mhariri wa gazeti lake mwenyewe Zuhra ambalo ndilo lilikuwa sauti ya TAA na baadae sauti ya TANU na Nyerere.

Alikuwapo pia Mzee bin Sudi yeye mwaka wa 1972 Rais wa Sudan Jaffar El Nimiery alipozuru Tanzania alifika makao makuu ya TANU Lumumba akiwa ameongozana na mwenyeji wake Mwalimu Julius Nyerere.

Mzee bin Sudi ndiyo alisoma risala ya kumkaribisha Nimiery Makao Makuu ya TANU.

Haikupita miezi mingi baada ya sherehe hii Mzee bin Sudi akafariki dunia.
 
"Wakibosho wakimfahamu kama Rajabu Ibrahim Kirama kwa majina yake ya udogoni ya Kirama Muro lakini sasa amewatokea akiwa Rajabu Ibrahim Kirama na yale mavazi waliyozoea kumuona akivaa udogoni hakuwanayo tena."

Mzee kwenye andiko lake,kuna sehemu kaandika hivi,hii ni kusema kuwa,Mzee Rajabu (Kirama Muro) aliingia katika dini hii akiwa mtu mzima.Na chanzo ni hicho,kuwa na "haki" ya kuendelea kuchinja.

Na mgogoro kati yake na Mangi ulikuwa ni wa "LAZIMA" sababu Mzee Kirama Muro alikulia kwenye familia ya Mangi,kusilimu na kuonekana yu mtofauti kwa dini na mavazi,ulikuwa ni "mgogoro" wa lazima wa kimila.

Ndio kusema,hata sasa,Uislam katika uchagga upo kwenye koo za Mzee Rajabu eneo la Machame
Uchagani, Uislam unanguvu eneo linaloitwa Masama pale Mudio.
Kule machame wako wachache.
Pale Kalali Machame wanamsikiti mkubwa tu ila waumini hawafikii 50.
Kuna misikiti mingine maeneo ya Mroma na Uswaa
 
Uchagani, Uislam unanguvu eneo linaloitwa Masama pale Mudio.
Kule machame wako wachache.
Pale Kalali Machame wanamsikiti mkubwa tu ila waumini hawafikii 50.
Kuna misikiti mingine maeneo ya Mroma na Uswaa
Asante mkuu...Wengine tusio na uzoefu sana eneo lile twajumlisha kama Machame!Upo sahihi
 
Uchagani, Uislam unanguvu eneo linaloitwa Masama pale Mudio.
Kule machame wako wachache.
Pale Kalali Machame wanamsikiti mkubwa tu ila waumini hawafikii 50.
Kuna misikiti mingine maeneo ya Mroma na Uswaa
Kiwatengu,
Nimesoma nyaraka kadhaa za Mzee Rajabu Ibrahim Kirama akiandikiana na Mangi Abdiel Shangali, Mangi Ngilisho Sina, Mangi Mkuu Thomas Marealle, viongozi wa serikali District Commissioner wa Moshi.

Nimesoma barua alizoandika kwa Gavana George Stewart katika miaka ya 1930s kipindi ambacho aliiunga Machame na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika iliyokuwa Dar es Salaam na jumuia nyingine za Kiislam Dar es Salaam na Mombasa.

Hakuna popote katika barua hizi nimekuta suala la kuchinja.

Nimesoma barua za nyingi tu za watu wengine katika nyaraka za Mzee Rajabu kuhusu mambo mengi yaliyowakabili Waislam wa Machame lakini sikukuta habari za kuchinja.

Barua hizi zote kwenda kwa Mangi na viongozi wa serikali ya kikoloni Mzee Rajabu alikuwa akieleza ujenzi wa misikiti na shule na kudai Waislam wapewe msaada wa serikali kama ule unaotolewa kwa shule za kanisa.

Hii ni mifano michache tu.
Suala la kuchinja hakuna popote nilipolikuta.
 
Inawezekana hakuna lakini nikuambie kuwa huu ndio ukweli kuhusu mzee rajabu.
Pilipili...
Ukweli unahitaji uthibitisho vinginevyo ndiyo kama hivi "ukweli," unashindwa na yale yanayopatikana katika utafiti.

Kulikuwa na tatizo kubwa sana la historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Walikuja watu na "ukweli," uliolazimishwa kuhusu Julius Nyerere kuwa TANU iliundwa na yeye.

Mimi nilieleza kuwa huo "ukweli," unapingana na ukweli ulioko katika nyaraka za Sykes.

Hawakupenda kufahamishwa kuwa African Association iliasisiwa na Kleist Sykes 1929 na wanae wawili Abdul na Ally ni katika wazalendo 17 walioasisi TANU na kadi zao za TANU ni no. 2 na 3 no. 1 ikiwa ya Julius Nyerere.

Nikaeleza niliyosoma katika nyaraka za Sykes kuanzia mwaka wa 1929 na nikaandika kitabu kudhihirisha ukweli wa kweli.

Hili la "ukweli" usio na ithibati ndiyo ninaloliona na hapa katika historia ya Rajabu Kirama.
 
Nimejifunza sana kutokana na wachangiaji wa humu,na nimeona kuwa watu mnaweza kuwa na perspective tofauti ya history moja na hii inaweza kutokana na sources zenu kuwa tofauti.Mohammed Said,Barafu,Joka kuu na Bangusule michango yenu mizuri.Mohammed Said na Barafu kubalini kuwa mnakuja na miono miwili tofauti lakini mengi mnayoandika yanaendana,sio lazima mwe sawa kila kitu. Endeleeni kumwaga historia tunu wengi tunafaidika na kufuatilia.

Sent from my SM-G960F using JamiiForums mobile app
 
Nimejifunza sana kutokana na wachangiaji wa humu,na nimeona kuwa watu mnaweza kuwa na perspective tofauti ya history moja na hii inaweza kutokana na sources zenu kuwa tofauti.Mohammed Said,Barafu,Joka kuu na Bangusule michango yenu mizuri.Mohammed Said na Barafu kubalini kuwa mnakuja na miono miwili tofauti lakini mengi mnayoandika yanaendana,sio lazima mwe sawa kila kitu. Endeleeni kumwaga historia tunu wengi tunafaidika na kufuatilia.

Sent from my SM-G960F using JamiiForums mobile app
London 1,
Ingia mohamedsaidsalum.blogspot.com fanya search kwa jina au matukio.
 
Huyu mzee alikuwa mchagga gani huyu wasomali wanampelekesha wanavyotaka?

Hata hivyo! suala la kutokutahiriwa linamewekewa chunvi kwa sababu kiasili wachaga hufuata mila za tohara kama wakurya huwezi kuoa ukiwa hujatahiriwa na hufanyika kwa Marika maarufu kama LUMBO
Kiboko ya mchaga Ni msomalii '

chezea hhengine hhangu hhagumuu" Ni msemo maarifu wa mzee elme pale boma ngombe alikua anatoa fozi za bakora jwa wachaaga
 
Kiboko ya mchaga Ni msomalii '

chezea hhengine hhangu hhagumuu" Ni msemo maarifu wa mzee elme pale boma ngombe alikua anatoa fozi za bakora jwa wachaaga
Hivyo kabisa sijui alitaka kizazi gani, yapo mengine yalipotelea Mombasa
 
Kichuguu,

..Mangi Thomas Marealle wa Marangu alichaguliwa kuwa Mangi Mkuu mwaka 1952.

..katika uchaguzi huo alimshinda Abdieli Shangali ambaye alikuwa Mangi wa Machame.

..Thomas Marealle aliondolewa ktk nafasi yake mwaka 1959 baada ya Chaga Council kupiga kura ya kuachana na utaratibu wa kuongozwa na Mangi Mkuu.

..Naamini hizo ndizo sababu zilizopelekea Mangi Thomas Marealle kuwa maarufu kuliko Mangi wenzake kama Abdieli Shangali wa Machame, John Ndaskoi Maruma wa Rombo, au Petro Itosi Marealle wa Vunjo.
 
Kichuguu,

..Mangi Thomas Marealle wa Marangu alichaguliwa kuwa Mangi Mkuu mwaka 1952.

..katika uchaguzi huo alimshinda Abdieli Shangali ambaye alikuwa Mangi wa Machame.

..Thomas Marealle aliondolewa ktk nafasi yake mwaka 1959 baada ya Chaga Council kupiga kura ya kuachana na utaratibu wa kuongozwa na Mangi Mkuu.

..Naamini hizo ndizo sababu zilizopelekea Mangi Thomas Marealle kuwa maarufu kuliko Mangi wenzake kama Abdieli Shangali wa Machame, John Ndaskoi Maruma wa Rombo, au Petro Itosi Marealle wa Vunjo.
JK,
Hebu angalia haya maneno hapa chini:

''Lakini ukoloni ulikuwa na faida zake, na Rajabu Ibrahim Kirama nyota yake itakuja kunyanyuka na mwanga wake kuangaza sehemu nyingi za Uchaggani, lau kama itakaribia karne moja kabla ya historia kumtambua.

Nyota hii ya Rajabu Ibrahim Kirama itang’ara ilhali Chifu Abdieli Shangali anaishuhudia kwa macho yake.

Uhasama huu baina ya Chief Abdiel Shangali aliyekuwa akipambana na Rajabu Ibrahim Kirama kwa ajili ya jitihada zake za kueneza Uislamu Uchaggani taratibu ukapoteza ukali wa nguvu zake kwani Wachagga haukupita muda mrefu wakajitazama upya na kutambua kuwa kwa hakika adui hakuwa nduguye Mchagga Muislam; adui mkuu kwao wote ulikuwa ukoloni ambao ulihitaji nguvu ya pamoja kukabiliana nao.

Katika jitihada hizi za kujiletea maendeleo Wachagga wakaunda Kilimanjaro Chagga Citizens Union (KCCU) Umoja wa raia wa Kilimanjaro.

Petro Njau akiwa kiongozi ili isimamie maslahi ya Wachagga kama taifa.

Katika kanuni za KCCU, zinawataja Wachagga kama watu waliozaliwa huru na wenye haki ya kulinda uhuru wao.[1]

Petro Njau anaeleza kuwa KCCU kilikuwa, ‘chama cha siasa cha kikabila’.

Hii fikra ya kuwa Kilimanjaro yote ni nchi ni fikra ambayo ilijijenga sana katika kabila la Wachagga. Kwani kila viongozi wa Wachagga walipokuwa na mkutano wa viongozi ukisoma taarifa za mikutano hiyo maneno, ‘nchi’, ‘taifa’, ‘raia’, ‘uchaguzi’, ‘kura’, na ‘utawala’, yanajitokeza katika majadiliano kiasi kura imepata kufananishwa na johari, yaani kitu chenye thamani kubwa.

Petro Njau katika kura anaeleza wazi akitaka ieleweke kuwa kuwa, ‘kura moja kwa mtu mmoja’.

Wachagga walikuwa na bendera, walikuwa pia na wimbo wa taifa na siku maalum ya Wachagga maarufu kwa jina la ‘Chagga Day’.

Petro Njau akimwandikia Mangi Mkuu Thomas Marealle alimfahamisha kuwa kachaguliwa kwake kwa kura za Wachagga ndizo zilizompa heshima ndani ya taifa la Wachagga.''
(Nimenyanyambua kutoka kitabuni)

Ningependa kukufahamisha kuwa Petro Njau alikuwa moja wa waandishi wa Rajabu Ibrahim Kirama mwingine ni Joseph Merinyo.



[1] Kanuni za Chagga Citizens’ Union, Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom