barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,882
Ni kweli kuwa Uislam Machame ni wa koo moja,eneo moja la Machame. Chanzo ni Mzee Rajabu katika miaka ya 1930's kuelekea 1940's, kipindi ambacho dunia imefunguka kutoka katika Vita ya Kwanza ya Dunia. Sasa ikawa Mkoloni akiheshimu makoloni yake na watu wake,ikiwamo nidhamu katika kufuata mila na desturi.Hivyo Mkoloni akiwa na wafanyakazi wenye imani za kidini tofauti alianza kuzingatia haya.Barafu,
Liepzig Mission waliingia Kilimanjaro 1893 na kwa miaka yote kuchinja hakukupata kuwa suala.
Mzee Rajabu hakuingia kwa ajili ya kuwa na ruhusa ya kuchinja kwani jamii iliyomzunguka yote ilikuwa inajichinjia wanyama wake bila ya kufata sheria ya Kiislam kwa sababu hapakuwa na Waislam.
Rajab Kirama kaingia Uislam mwaka wa 1930 na Machame hawakuwapo Waislam wa kutosha kuwa na sauti ya kuhitaji uchinjaji kwa mujibu wa sharia.
Uislam Machame ulipata nguvu kuanzia miaka ya mwishoni 1940 baada ya Sheikh Abdallah Minhaj kufika na kuanza kusomesha Uislam.
Utumishi ndani ya serikali ya Kikoloni kulikuwa na Wahindi,Waarabu na Waswahili kutoka maeneo ya Pwani walioenda kufanya kazi katika ofisi za Kikoloni "mikoani" ikiwemo Kilimanjaro.Hapa ndio Mkoloni akaona hitaji rasmi la kuchinja kwa kufuata imani za watu.
Mabadiliko haya yalifanya sehemu ya machinjio ya minada kama Boma la Ng'ombe kupata wachinjaji wenye vigezo vyote(ikiwemo dini ya Uislam). Kigezo hiki kilikuwa rahisi kwa Wasomali na Wagunya wa Mombasa.Ili wachinjaji wa asili kama Mzee Rajabu kuipata nafasi hiyo,iliwabidi kusilimu.Ndio maana Mzee Rajabu kaingia katika Uislam akiwa mtu mzima kabisa kwa umri.
Hii ilifanyika katika machinjio yote ya Tanganyika. Kwa mfano kuna Wazee wengi wa Kiislam walipelekwa Kongwa kwa ajili ya kuchinja, hivi ndivyo Wagogo wa Kongwa walivyoanza kupokea dini hii,sababu mkusanyiko wa manamba wa "Kongwa Groundnuts Scheme" walitoka sehemu mbalimbali za Tanganyika na nje ya Tanganyika wa dini tofauti,Walihitaji mchinjaji mwenye vigezo.
Shamba la ng'ombe Kongwa lilihitaji wachinjaji Waislam ili nyama iuzike vizuri, shamba kubwa na la kisasa la Mgodi wa Williamson Mwadui(Dairy Farm) lilihitaji wachinjaji wa Kiislam toka miaka ya 1930 sbb mgodi ulijumuisha wafanyakazi wa dini tofauti na kulikuwa na duka moja tu la mgodi la kuuza nyama.
Ukisema miaka hiyo hakukuwa na jamii kubwa ya Wachaga waislam,unataka kuondoa ukweli kuwa machinjio ya Boma la ng'ombe hayakuhudumia tu Machame, bali Moshi yote na watumishi wa dini tofauti waliokuwa wakihudumu katika serikali ya Mkoloni.