Ombi kwa Rais Samia: Sheria Mpya ya Uchaguzi Bado ina Ubatili. Haki ya Kuchagua na Kuchaguliwa imeporwa! Irejeshwe kwa Mujibu wa Katiba!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,279
120,689
Wanabodi,
Hii ni makala yangu, Gazeti la Nipashe ya Leo.
20240602_103621.jpg

Makala ya leo ni kutoa shukrani na Asante kwa Rais Samia kwa Sheria Mpya ya Uchaguzi, ila Haki ya Watanzania Kuchagua, na Kuchaguliwa, Bado Imeporwa kwa kukasimiwa kwa Vyama vya Siasa. Hili ni ombi, haki hiyo Irejeshwe kwa Wananchi wenye katiba yao!. Namna pekee ya kuirejesha ni kupitia mabadiliko madogo ya katiba, minimum reforms, kuuondoa, ubatili uliochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!.

Ombi ni ombi tuu, linaweza kukubaliwa au kukataliwa, ila mimi kama mwananchi wa kawaida na raia mwema wa nchi yako, unapo ona kuna jambo fulani halijakaa vizuri, kwanza unaarifu, kisha unashauri the right thing to do, hivyo nimetimiza wajibu wangu kuwasilisha ombi hili.

Naomba kuanza kwa nukuu kutoka kwa Rais Samia.
Hide quoted text

"Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza” - Samia Suluhu Hassan Mwisho wa kunukuu.

hii ni nukuu ya Rais Samia katika andiko lake la miaka 30 ya Vyama Vingi nchini Tanzania. Na baada tuu ya kutoka kwa andiko hilo, mimi niliandika makala ya kumpongeza, Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

Maneno hayo ni maneno makubwa sana na yenye maana kubwa kwasababu yanahusu "kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao", na sio mara moja wala mara mbili, nimekuja humu kueleza kuwa sina wasiwasi kabisa na nia ya Rais Samia katika kuwapatia Watanzania, haki kwa kauli na matendo. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki

Uhuru wa watu kuwachagua viongozi wanaowataka ndio haki ya tatu ndani ya katiba yetu ya 1977. Haki kuu ya kwanza ni haki ya uraia, haki kuu ya pili ni haki ya kuishi, na haki kuu ya tatu ni haki ya kuchagua na kuchaguliwa, ibara ya 5 na ibara ya 21.

Haki hii ina sherti moja tuu la umri wa miaka 18 kupiga kura, umri wa miaka 21, kuchaguliwa diwani au mbunge, na miaka 40, kuchaguliwa kuwa rais wa JMT.

Hakuna shurti la kulazimishwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa, kilichofanyika kuchomekea shurti la mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa, ndani ya Katiba yetu ni uhuni na ubatili tuu uliofanyika kiubatili kinyume cha katiba yetu na Mahakama Kuu iliisha ubatilisha ubatili huo!.

Mimi mwenyewe najihesabu ni mtetezi huru wa haki, huu ubatili wa katiba nimeuzungumza sana.

View: https://youtu.be/3a4SjkV46JY?si=rS6X-ttZFwtlbcyy

View: https://youtu.be/PBpjDhH2XiA?si=y3wvuR5p0UBD03cn

View: https://youtu.be/lBC3xKODSvY?si=SNx0DquDv8knTt1p

Kiongozi yoyote anapoandika ama anapohutubia, kuna mambo mawili, kwenye andiko lake ama hotuba yake.
1. Kati ya andiko la Kiongozi kuna vitu ni maono, mawazo, maneno na maandishi ya Kiongozi yeye mwenyewe kutoka moyoni mwake, kichwani mwake, mawazoni mwake, yaani ni yeye mwenyewe halisi.
2. Viongozi wana wasaidizi ambao huwa wanawaandikia talking notes, na kwa rais wa nchi, ana wasaidizi hotuba ambao wanamuandalia nini cha kusema kwa kumuandikia, kisha Rais kwanza anapitia kile alichoandikiwa lakini sio chake, anaweza kuongeza chake au kupunguza, na ndipo anakuja kuhutubia au kutoa andiko.

Wakati akihutubia, sisi tunaosikiliza, tukisikia kila Rais anachosema kwenye hotuba yake, tunahesabu kila kilichosemwa ni rais kusema.

Wakati Rais akihutubia, kila anachosema ni Rais kusema, msikilizaji huwezi kujua kipi ni cha kwake mwenyewe na kipi ni ameandikiwa tuu lakini sii cha kwake.

Hii pia hutokea kwa wasomaji wa habari kwenye TV zote na redio zote, watazamaji na wasikilizaji, wanamuona mtangazaji, wanamsikiliza mtangazaji, wao wanajua hizo habari wametangaziwa na mtangazaji fulani, wao wanajua ni mtangazaji huyo ndie anajua habari hizo, kumbe hawajui kazi ya mtangazaji wa habari ni kutangaza tuu habari alizoandikiwa na wengine, yeye kazi yake ni kusoma tuu!.

Vivyo hivyo kwenye hotuba za Viongozi, kuna Viongozi wanasoma tuu hotuba walizoandikiwa na wengine lakini sio mawazo yao, sio maneno yao, ila ni matamshi yao!.

Kama nilivyosema kwenye habari, mtangazaji unaandikiwa ,kisha unapewa kuipitia habari hiyo , kwa RTD, taarifa ya habari ni dakika 10, mtangazaji unatakiwa kuipitia nusu saa kabla, ili uielewe na unaposoma, una soma kitu unachokijua.

Kitendo cha kuichukua habari ambayo hujaiandika wewe, ukaipitia na kuisoma kama vile ni umeiandika wewe, kinaitwa "presence" kwa lugha ya Kiingereza, ndio maana watangazaji huitwa presenters, kazi yao ni ku present tuu.

Kuna wakati msomaji wa habari unapitia habari usiyoielewa, unapaswa uulize, ili usisome kitu usichokielewa, ili ukisoma ile presence iwepo. Lakini katika mitikasi hii na ile, kuna siku mtangazaji unakuwa umechelewa kupitia news kabla, hivyo unasoma tuu kwa uzoefu, hata ukikutana na kitu usichokielewa, unakisoma tuu hivyo hivyo kilivyoandikwa, na wasikilizaji na watazamaji watasikia tuu nakuelewa, lakini kwa watu sensitive na kitu kinachoitwa “graphology”, wao watamnote mtangazaji ana jiuma uma ulimi “stammering”, hivyo unajua tuu huyu mtu hajapitia, hiyo habari, ila anasoma kwa uzoefu tuu, hivyo ni anasoma kitu asichokijua, anasema kitu alichoandikiwa lakini hakijui.

Vivyo hivyo hutokea kwenye baadhi ya hotuba za viongozi, anakuwa emeandikiwa kitu asichokijua, anapitia hotuba, kisha anahutubia kitu asichokijua, hii inaitwa "paying lip services" bahati mbaya sikijui Kiswahili chake.

Maneno hayo ya Rais Samia kwenye andiko lake ni maneno makubwa, mazito sana, na mimi nikayaandikia makala kwenye safu yangu gazeti za Jumapili ya Julai 10, 2022 yanye kichwa cha habari , "Rais Samia Akitekelrza Hili, Hakika Tanzania Itabarikiwa" Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

Sasa sheria mpya ya uchaguzi imeishatungwa, ila sheria hiyo mpya bado ina ubatili ule ule tunaoupigia kelele, hali inayonifanya kuanza kujiuliza, hivi haya maneno ya Rais Samia "Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza”
Je ni maneno ya kwake mwenyewe Rais Samia au aliandikiwa tuu na wasaidizi wake hotuba?!.

Kwa vile Rais Samia yeye sio mwanasheria, yeye tunam excuse Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!

Je hii sheria mpya ya uchaguzi, yenye ubatili ule ule, italeta vipi ushindani wa haki wakati Rais Samia ameahidi, "kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza”
wakati sheria mpya ya uchaguzi, watu bado hawana haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka, bali Watanzania tunalazimishwa kuwachagua viongozi waliopitishwa na vyama vya siasa na sio viongozi wanaowataka!.

Tafsiri ya alichokisema Rais Samia, na kilicholetwa kwenye sheria mpya ya uchaguzi ni vitu viwili tofauti, lakini kwasababu muda bado tunao, ndio maana tunaendelea kumuomba rais Samia tufanye mabadiliko hili liangaliwe ili sheria yetu ya uchaguzi, iwe ni sheria ya haki kweli kama Ibara ya 5 na 21 za 1em katiba zinavyosema.

Wasalaam.

Paskali
Rejea za Mwandishi kuhusu hitaji la mabadiliko ya katiba kabla ya mabadiliko ya sheria.
- Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa

Kwa nini unazunguka? Mwambie wewe Samia umepora haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa sababu ni yeye aliyepeleka muswada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi.
Ni kweli ni awamu yake, kwa vile yeye sio mwanasheria, inawezekana kabisa wamemletea batili bila kumweleza ni batili, na Bunge letu la ajabu kabisa, likaipokea miswada hiyo yenye ubatili, ikaipitisha hivyo hivyo na ubatili wake!, wakatunga sheria batili, wakampa Rais Samia akaisaini bila kujua kuwa amesaini sheria batili kwasababu yeye sio mwanasheria Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!

Makala kama hizi, zitamsaidia kuwaita wasaidizi wake na kuwauliza kuwa imekuweje serikali yake itunge sheria batili?, Bunge letu nalo kama Bunge la mazuzu, wakaipitisha hiyo sheria batili hivyo hivyo na ubatili wake, na yeye akaisaini.

P
 
Mpumbavu huwa hatambui kuwa ni mpumbavu na akiambiwa juu ya upumbavu wake huwa anakataa kwa sababu ni mpumbavu.

"Huwezi muelimisha mpumbavu akaacha upumbavu wake"Nyerere
Yaani hapo ndipo mtihani ulipo!! Ukijaribu kumuangalia lisu anavyojitahidi kutoa elimu ya uraia lakini wale wanaofaidi mema ya nchi wanawapanga wa pumbavu na kumuona lisu adui!!
 
Ni kweli ni awamu yake, kwa vile yeye sio mwanasheria, inawezekana kabisa wamemletea batili bila kumweleza ni batili, na Bunge letu la ajabu kabisa, likaipokea miswada hiyo yenye ubatili, ikaipitisha hivyo hivyo na ubatili wake!, wakatunga sheria batili, wakampa Rais Samia akaisaini bila kujua kuwa amesaini sheria batili kwasababu yeye sio mwanasheria Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!

Makala kama hizi, zitamsaidia kuwaita wasaidizi wake na kuwauliza kuwa imekuweje serikali yake itunge sheria batili?, Bunge letu nalo kama Bunge la mazuzu, wakaipitisha hiyo sheria batili hivyo hivyo na ubatili wake, na yeye akaisaini.

P
Acha kutufanya watoto wadogo ni bora useme mimi naogopa kumpa lawama Rais sababu ana mamlaka makubwa ambayo yanaweza kunidhuru kuliko ku beat around the bush.
 
Ni kweli ni awamu yake, kwa vile yeye sio mwanasheria, inawezekana kabisa wamemletea batili bila kumweleza ni batili, na Bunge letu la ajabu kabisa, likaipokea miswada hiyo yenye ubatili, ikaipitisha hivyo hivyo na ubatili wake!, wakatunga sheria batili, wakampa Rais Samia akaisaini bila kujua kuwa amesaini sheria batili kwasababu yeye sio mwanasheria Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!

Makala kama hizi, zitamsaidia kuwaita wasaidizi wake na kuwauliza kuwa imekuweje serikali yake itunge sheria batili?, Bunge letu nalo kama Bunge la mazuzu, wakaipitisha hiyo sheria batili hivyo hivyo na ubatili wake, na yeye akaisaini.

P
Changamoto ni uchawa wa wabunge. Badala ya kujadili muswada kwa kuhakikisha katiba inalindwa wanaishia kumpongeza mleta muswada. Athari yake ni kuwa na sheria batili zisizo na maslahi kwa Taifa!
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu, Gazeti la Nipashe ya Leo.
View attachment 3006431

Makala ya leo ni kutoa shukrani na Asante kwa Rais Samia kwa Sheria Mpya ya Uchaguzi, ila Haki ya Watanzania Kuchagua, na Kuchaguliwa, Bado Imeporwa kwa kukasimiwa kwa Vyama vya Siasa. Hili ni ombi, haki hiyo Irejeshwe kwa Wananchi wenye katiba yao!. Namna pekee ya kuirejesha ni kupitia mabadiliko madogo ya katiba, minimum reforms, kuuondoa, ubatili uliochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!.

Ombi ni ombi tuu, linaweza kukubaliwa na linaweza kukataliwa, mimi kama mwananchi, nimetimiza wajibu wangu kuwasilisha ombi hili.

Naomba kuanza kwa nukuu kutoka kwa Rais Samia.
Hide quoted text

"Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza” - Samia Suluhu Hassan Mwisho wa kunukuu.

hii ni nukuu ya Rais Samia katika andiko lake la miaka 30 ya Vyama Vingi nchini Tanzania. Na baada tuu ya kutoka kwa andiko hilo, mimi niliandika makala ya kumpongeza, Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

Maneno hayo ni maneno makubwa sana na yenye maana kubwa kwasababu yanahusu "kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao", na sio mara moja wala mara mbili, nimekuja humu kueleza kuwa sina wasiwasi kabisa na nia ya Rais Samia katika kuwapatia Watanzania, haki kwa kauli na matendo. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki

Uhuru wa watu kuwachagua viongozi wanaowataka ndio haki ya tatu ndani ya katiba yetu ya 1977. Haki kuu ya kwanza ni haki ya uraia, haki kuu ya pili ni haki ya kuishi, na haki kuu ya tatu ni haki ya kuchagua na kuchaguliwa, ibara ya 5 na ibara ya 21.

Haki hii ina sherti moja tuu la umri wa miaka 18 kupiga kura, umri wa miaka 21, kuchaguliwa diwani au mbunge, na miaka 40, kuchaguliwa kuwa rais wa JMT.

Hakuna shurti la kulazimishwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa, kilichofanyika kuchomekea shurti la mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa, ndani ya Katiba yetu ni uhuni na ubatili tuu uliofanyika kiubatili kinyume cha katiba yetu na Mahakama Kuu iliisha ubatilisha ubatili huo!.

Kiongozi yoyote anapoandika ama anapohutubia, kuna mambo mawili, kwenye andiko lake ama hotuba yake.
1. Kati ya andiko la Kiongozi kuna vitu ni maono, mawazo, maneno na maandishi ya Kiongozi yeye mwenyewe kutoka moyoni mwake, kichwani mwake, mawazoni mwake, yaani ni yeye mwenyewe halisi.
2. Viongozi wana wasaidizi ambao huwa wanawaandikia talking notes, na kwa rais wa nchi, ana wasaidizi hotuba ambao wanamuandalia nini cha kusema kwa kumuandikia, kisha Rais kwanza anapitia kile alichoandikiwa lakini sio chake, anaweza kuongeza chake au kupunguza, na ndipo anakuja kuhutubia au kutoa andiko.

Wakati akihutubia, sisi tunaosikiliza, tukisikia kila Rais anachosema kwenye hotuba yake, tunahesabu kila kilichosemwa ni rais kusema.

Wakati Rais akihutubia, kila anachosema ni Rais kusema, msikilizaji huwezi kujua kipi ni cha kwake mwenyewe na kipi ni ameandikiwa tuu lakini sii cha kwake.

Hii pia hutokea kwa wasomaji wa habari kwenye TV zote na redio zote, watazamaji na wasikilizaji, wanamuona mtangazaji, wanamsikiliza mtangazaji, wao wanajua hizo habari wametangaziwa na mtangazaji fulani, wao wanajua ni mtangazaji huyo ndie anajua habari hizo, kumbe hawajui kazi ya mtangazaji wa habari ni kutangaza tuu habari alizoandikiwa na wengine, yeye kazi yake ni kusoma tuu!.

Vivyo hivyo kwenye hotuba za Viongozi, kuna Viongozi wanasoma tuu hotuba walizoandikiwa na wengine lakini sio mawazo yao, sio maneno yao, ila ni matamshi yao!.

Kama nilivyosema kwenye habari, mtangazaji unaandikiwa ,kisha unapewa kuipitia habari hiyo , kwa RTD, taarifa ya habari ni dakika 10, mtangazaji unatakiwa kuipitia nusu saa kabla, ili uielewe na unaposoma, una soma kitu unachokijua.

Kitendo cha kuichukua habari ambayo hujaiandika wewe, ukaipitia na kuisoma kama vile ni umeiandika wewe, kinaitwa "presence" kwa lugha ya Kiingereza, ndio maana watangazaji huitwa presenters, kazi yao ni ku present tuu.

Kuna wakati msomaji wa habari unapitia habari usiyoielewa, unapaswa uulize, ili usisome kitu usichokielewa, ili ukisoma ile presence iwepo. Lakini katika mitikasi hii na ile, kuna siku mtangazaji unakuwa umechelewa kupitia news kabla, hivyo unasoma tuu kwa uzoefu, hata ukikutana na kitu usichokielewa, unakisoma tuu hivyo hivyo kilivyoandikwa, na wasikilizaji na watazamaji watasikia tuu nakuelewa, lakini kwa watu sensitive na kitu kinachoitwa “graphology”, wao watamnote mtangazaji ana jiuma uma ulimi “stammering”, hivyo unajua tuu huyu mtu hajapitia, hiyo habari, ila anasoma kwa uzoefu tuu, hivyo ni anasoma kitu asichokijua, anasema kitu alichoandikiwa lakini hakijui.

Vivyo hivyo hutokea kwenye baadhi ya hotuba za viongozi, anakuwa emeandikiwa kitu asichokijua, anapitia hotuba, kisha anahutubia kitu asichokijua, hii inaitwa "paying lip services" bahati mbaya sikijui Kiswahili chake.

Maneno hayo ya Rais Samia kwenye andiko lake ni maneno makubwa, mazito sana, na mimi nikayaandikia makala kwenye safu yangu gazeti za Jumapili ya Julai 10, 2022 yanye kichwa cha habari , "Rais Samia Akitekelrza Hili, Hakika Tanzania Itabarikiwa" Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

Sasa sheria mpya ya uchaguzi imeishatungwa, ila sheria hiyo mpya bado ina ubatili ule ule tunaoupigia kelele, hali inayonifanya kuanza kujiuliza, hivi haya maneno ya Rais Samia "Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza”
Je ni maneno ya kwake mwenyewe Rais Samia au aliandikiwa tuu na wasaidizi wake hotuba?!.

Kwa vile Rais Samia yeye sio mwanasheria, yeye tunam excuse Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!

Je hii sheria mpya ya uchaguzi, yenye ubatili ule ule, italeta vipi ushindani wa haki wakati Rais Samia ameahidi, "kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza”
wakati sheria mpya ya uchaguzi, watu bado hawana haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka, bali Watanzania tunalazimishwa kuwachagua viongozi waliopitishwa na vyama vya siasa na sio viongozi wanaowataka!.

Tafsiri ya alichokisema Rais Samia, na kilicholetwa kwenye sheria mpya ya uchaguzi ni vitu viwili tofauti, lakini kwasababu muda bado tunao, ndio maana tunaendelea kumuomba rais Samia tufanye mabadiliko hili liangaliwe ili sheria yetu ya uchaguzi, iwe ni sheria ya haki kweli kama Ibara ya 5 na 21 za 1em katiba zinavyosema.

Wasalaam.

Paskali
Rejea za Mwandishi kuhusu hitaji la mabadiliko ya katiba kabla ya mabadiliko ya sheria.

- Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa

- Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki

- Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
Tanzania hakuna uchaguzi, Bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Na sio kwamba rais haeilewi kinachoondelea, bali uchaguzi wa haki hamlipi yeye Wala chama chake. Watu wajinga tu ama wanaofadika na Sheria hizi mbovu, ndio watajitokeza kupiga kura kwa Sheria hizihizi. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yataleta mabadiliko ya kweli.
 
Ni kweli ni awamu yake, kwa vile yeye sio mwanasheria, inawezekana kabisa wamemletea batili bila kumweleza ni batili, na Bunge letu la ajabu kabisa, likaipokea miswada hiyo yenye ubatili, ikaipitisha hivyo hivyo na ubatili wake!, wakatunga sheria batili, wakampa Rais Samia akaisaini bila kujua kuwa amesaini sheria batili kwasababu yeye sio mwanasheria Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!

Makala kama hizi, zitamsaidia kuwaita wasaidizi wake na kuwauliza kuwa imekuweje serikali yake itunge sheria batili?, Bunge letu nalo kama Bunge la mazuzu, wakaipitisha hiyo sheria batili hivyo hivyo na ubatili wake, na yeye akaisaini.

P
Sio kwamba hajui, huo utetezi wa kwamba sio mwanasheria ni lugha ya hofu. Anajua sana anachokifanya, ila lugha zake toka mwanzo tulisema ni hadaa ili kupata sifa za kisiasa. Sasa imefika wakati wa maneno yake kuwa matendo, ukweli wa tuliosema kuwa ni mtu wa hudaa unadhihirika.
 
Back
Top Bottom