Njama za uhaini za kina Hans Poppe (Sehemu ya 2️⃣)

Jan 28, 2024
96
133
Screenshot_20240419-112347.jpg

Karibu katika sehemu ya pili ya uchambuzi wa kina wa kesi ya Hatibu Gandhi na wenzake dhidi ya Jamhuri. Kesi iliyo na historia ya kuvutia na kusisimua sana, kesi iliyoficha mengi yasiyojulikana haswa na kizazi cha sasa cha Tanzania. Kesi inayomuhusisha nguli wa maswala ya michezo mzee wetu marehemu Zacharia Hans Poppe na wenzake waliotaka kufanya mapinduzi dhidi ya serikali ya Mwl Nyerere mnamo 1983.

But first, some background.
Katika sehemu ya kwanza , tuliangazia zaidi katika historia ya Zacharia Hans Poppe tukigusia maisha yake ya awali kabisa na mazingira ya kisiasa na kiuchumi ya wakati huo yaliopelekea kuhusika katika kesi hii ya uhaini (Treason). Tulifunga kwa maswali muhimu yaliyoachwa wazi kama vile; ni akina nani waliohusika katika kupanga njama hizi za uhaini pamoja na Luteni Hans Poppe?Na ni nani aliyewasaliti, kusababisha kukamatwa kwao?

Sasa, tukiwa na azma ya kufichua vilivyofichika na kuleta mwangaza katika kesi hii ya kihistoria, sehemu ya pili itaenda kwa undani zaidi katika majibu ya maswali hayo. Sehemu hii itaeleza namna kila muhusika alivyohusika katika case hii na namna ya njama zao za usaliti zilivyojulikana na serikali.

Sasa tuanze na sehemu ya pili,
NJAMA ZA UHAINI ZA HANS POPPE NA WENZAKE (Kabla ya kukamatwa)
Je, ni akina nani waliokuwa nyuma ya njama hizi?
Nitakusanua. Ipo ivi, njama nzima za tukio hili la mapinduzi zilipangwa na Pius Mtakubwa Lugangira (almaalufu kama 'Uncle Tom') akishirikiana na Captain Hatty Macghee (Hatibu Gandhi) pamoja na komandoo pendwa wa Mwl, Nyerere Muhammed Tamimu. Ambapo hawa wote waliingia nnchini kutoka abroad kati ya November na December 1982. Mapinduzi haya yalipangwa kufanyika ifikapo January 9, 1983.

Baada ya kuingia nnchini, watatu hao walianza kushawishi na kuajili baadhi ya watu (especially wanajeshi) japo baadhi yao walikataa ila wapo waliokubali ikiwemo Captain Christopher Kadego, aliyekuwa Mwanajeshi wa tank unit in Dar Es Salaam; Lieutenant Eugene Maganga, huyu yeye alikua mwanajeshi wa JWTZ na finalist wa BA degree in Political Science UDSM; Captain Metusela Suleiman Kamando, Captain Vitalis Gabriel Mpunda na Captain Rodrick Roushan Roberts hawa wote walikua ni marubani wa JWTZ Airwings at Ukonga Dar Es Salaam; Captain Dietrich Oswald Mbogoro pamoja na Captain Zacharia Hans Poppe, wao hawa walikua katika jeshi la Ulinzi wa Anga. Mwisho ni P3794 Lieutenant Badru Rwechungura Kajaja aliyekua mwanajeshi kutoka kambi ya Nachingwea.

Inasemekana, December 1982 Hatibu Gandhi pamoja na Capt Kamando walitembelea Zanzibar mara kadhaa katika nyumba namba 80B Drive-in. Pia wakati huo huo bwana Hatibu Gandhi aliorganise vikao kadhaa na wanajeshi waliofanikiwa kuwapata (Kena Hans Poppe) katika nyumba namba 65-E 32P iliyopo Kinondoni Mkwajuni kando ya Barabara ya Livingstone jijini Dar es Salaam, iliyokuwa ya ndugu yake Gandhi aliyejulikana kama Zahara Abdulla Sengumba. On
other side, Uncle Tom yeye alifikia Motel Agip lakini alikua akitembelea zaidi katika nyumba namba 1127 Chore Road at Masaki, Dar Es Salaam iliyokuwa mali ya ndugu yake Christopher Pastor Ngaiza ambaye alikua mshauri wa raisi (Nyerere kwa wakati huo). Ngaiza yeye alisema kuwa Uncle Tom alimuomba kutumia nyumba hiyo kwaajili ya vikao vyake vya biashara na aliitumia nyumba hiyo kipindi yeye (Ngaiza) akiwa hayupo Dar Es Salaam. Kwaio nyumba hizi mbili ya Kinondoni (ya Bi. Zahara) na ile ya Masaki (ya Mh. Ngaiza) ndizo zikawa zinatumuka kwaajili ya kusuka mpango mzima wa mapinduzi.
Screenshot_20240419-215439.jpg

WALIOPELEKEA NJAMA HIZO KUJULIKANA NA KUZUIWA
Tutakumbuka mara baada ya Uncle Tom, Hatibu Gandhi na Muhammad Tamimu kuingia nnchini, walijaribu kuapproach watu mbalimbali, si kena Hans Poppe pakee, hivyo basi wapo wale waliofatwa na kukataa kujiunga na mpangu huu, watu hao ni pamoja na Captain Muhammad Suleiman Mape wa Navy Unit, lakini yeye hakureport chochote juu ya swala hilo. Walikuwepo pia Komando Captain Albert Ballati pamoja na Staff Sergeant Boniface Temu wao walijifanya kukubaliana na mpango wa kina Uncle Tom kumbe walikua wakireport mpango mzima kwa usalama wa Taifa.

Hawa (Ballati na Temu) sasa ndio waliokua wakiwachoma (kuwachunguza na kusnitch) wenzao (kena Gandhi) kwakutoa taarifa mbalimbali juu ya mipango ya mapinduzi iliyopangwa na kena Gadhi. Kwamfano, ni hawa ndio waliowaambia usalama wa taifa juu ya mpango wa Hans Poppe kuzima Battery No 2 siku mbili kabla ya tukio.

Mbali na hayo, upo ushuuda wa baadhi ya watu waliotoa ushaidi wa either kusikia ama kuambiwa juu ya mpango huu wa mapinduzi kutoka kwa wahusika wenyewe (kena Hatibu Gadhi). Mfano, Abdullah Mhando alidai kusikia juu ya swala kwa Hatibu Gadhi alipokua akimuendesha (as Taxi driver), Iddi Mushi Stambuli aliyejua juu ya swala hili baada ya kukutana Capt Christopher Kadego bar jijini Arusha na pia yupo Lieutenant Augustine Pancras Ndenjembi aliyeambiwa na Lieutenant Kajaja walipokutana katika kambi ya Lugalo.


Haya yote yanatupa majibu ya swali letu; Je, ni kina nani waliwasaliti kena Hans Poppe na kupelekea kukamatwa kwao?. Kuepusha kuwachosha wasomaji, Swali pekee linalobakia katika mkasa huu ni Je, ni hatua gani za kisheria zilichukuliwa baina ya wahusika?. Jibu la swali hili tutakua nalo katika sehemu ya tatu ya mkasa huu. Kama ni embe, basi hapa tumefika kwenye kokwa, ndo kwanza utamu wa simulizi hii unaenda kuanza. Hivyo basi, tukutane katika sehemu inayofwata itayochambua kwa undani hatua zote za kisheria zilizochukuliwa kwa akina Hans Poppe.
 
Hanspope unayemzungumzia ni huyu wa juzi wa Clabu ya Simba? Coz mzee Hanspope mwenyewe akiwa na cheo Cha polisi Cha SACP alifariki vitani Uganda mwaka 1979.

Bila shaka if am not mistaken mwili wake ulirudishwa mwaka 1981 ukazikwa Kwa Heshima.
 
Hanspope unayemzungumzia ni huyu wa juzi wa Clabu ya Simba? Coz mzee Hanspope mwenyewe akiwa na cheo Cha polisi Cha SACP alifariki vitani Uganda mwaka 1979.
Bila shaka if am not mistaken mwili wake ulirudishwa mwaka 1981 ukazikwa Kwa Heshima.
Ndio huyo huyo Mkuu
 
Hanspope unayemzungumzia ni huyu wa juzi wa Clabu ya Simba? Coz mzee Hanspope mwenyewe akiwa na cheo Cha polisi Cha SACP alifariki vitani Uganda mwaka 1979.
Bila shaka if am not mistaken mwili wake ulirudishwa mwaka 1981 ukazikwa Kwa Heshima.
Upo sahii, ni huyo huyo wa simba. Ukifatilia kwanzia sehemu ya kwanza 👉 Thread : 'Kwanini Hans Poppe na wenzake walitaka kumpindua Mwl. Nyerere? (SEHEMU YA 1️⃣) inayopatikana hapa, inaweza kukupa urahisi wa kuelewa story hii
 
Hanspope unayemzungumzia ni huyu wa juzi wa Clabu ya Simba? Coz mzee Hanspope mwenyewe akiwa na cheo Cha polisi Cha SACP alifariki vitani Uganda mwaka 1979.
Bila shaka if am not mistaken mwili wake ulirudishwa mwaka 1981 ukazikwa Kwa Heshima.
Huyo wa Simba ambaye alikufa kwa Corona ni mmoja wa wadunguaji wazuri sana na ndio maana akawa anambishia Magufuli. Sema Mabere Nyaucho Marando walimuua Tamimu pale Kinondoni Mkwajuni, Nyerere akachukizwa sana na kuuliwa kwa Taminu.
 
Hanspope unayemzungumzia ni huyu wa juzi wa Clabu ya Simba? Coz mzee Hanspope mwenyewe akiwa na cheo Cha polisi Cha SACP alifariki vitani Uganda mwaka 1979.
Bila shaka if am not mistaken mwili wake ulirudishwa mwaka 1981 ukazikwa Kwa Heshima.
Ndio yeye
 
Nampongeza Hans Pope nyerere alikua anatakiwa kupinduliwa kweli nchi ilikua imeshamshinda alikua na mawazo mfu had raia wakaanza kuvaa magunia
 
N
Huyu wa Simba?
Ndio yeye, luteni usu wa kwanza kwa umri wa miaka 19 JWTZ, alihukumiwa kifungo cha maisha akasamehewa na mwinyi, akatoka na kua tajiri mkubwa miaka kadhaa mbele.

Hii story usipotaja wale askari kutoka ifakara, itakua imekosa mvuto kabisa.
 
Huyo wa Simba ambaye alikufa kwa Corona ni mmoja wa wadunguaji wazuri sana na ndio maana akawa anambishia Magufuli. Sema Mabere Nyaucho Marando walimuua Tamimu pale Kinondoni Mkwajuni, Nyerere akachukizwa sana na kuuliwa kwa Taminu.
Tamimu alikua mtu na nusu, mkasa wa kifo chake, utakuja katika sehemu ya tatu
 
Back
Top Bottom