Ndugu zangu yamenikuta naomba mnisaidie

Ila mkuu wewe ni mwalimu kiaje?mwandiko wako majanga pia inaonekana wewe ni mshamba sana tena ule wimbo wa bushoke mume bwege unakuhusu ndio maana binti anakuchezea na kukurusha rusha kama mahindi ya bisi. Huna msimamo,unahudumia mwanamke hujamuoa wala kumchumbia kapimwe akili

Halafu ukute family members wako wanaishi maisha ya tabu sana wakikuomba hela mkali huku ukiwasimanga kumbe unazichezea kwa mwanamke anaekudharau aiseee
17882505_196233997550194_3715390673772347392_n.jpg
 
Ndugu yangu soma,wazazi,ndugu jamaa, wanategemea urudi na degree umeanza masomo mengine,usichanganye mapenzi na masomo tena afadhali upate anaekupenda ..hebu jiulize huyo binti anakupenda?kama jibu ni hapana muache huna cha kupoteza,utazeeka kwa mwanamke asiye wako,SOMA UPATE ULICHOFUATA DAR.
 
Hizi ndugu zangu zote ni za nini?

Acha kulia lia wewe chukua uamuzi wa kiume.

Unabwaga manyanga ama unabeba msalaba wako.

Uanaume sio wingi wa ndevu.
 
Igweeeeeeeeeeee,


Ndugu wana jamvi Mimi nikijana ambae nasoma chuo Fulani hapa mjini dar es salaam na nimwalimu halimashuri Wa secondary halimashauri hapa Tanzania.

Naomba ushauri kwenu kwa sababu mnamo oktober mwaka 2015 nilikuja kuanza masomo yangu ya shahada ya kwanza na siku moja nikapata mwaliko Wa Kwenda kwenye sherehe ya harusi nakukutana na binti mmoja nae mwanachuo nakuanzisha mahusiano.


Ndugu zangu Mimi nimeondoka mkoani sijaoa na Wala sina mtoto .Tumeanzisha mahusiano Mimi nilikuwa naishi hostel yeye alikuwa kapanga chumba ikumbukwe ni vyuo tofauti.

Tumekaaaa mda mrefu ktk mahusiano mpaka January 2017 kodi yake ilikuwa imeisha tukaamua kuhama kutoka alipo pale na kuhamia sinza ambapo hapo mlipaji Wa kodi nilikuwa Mimi.Ambayo ni Tsh 150000 kwa mwenzoni alilipa laki 1.

Ndugu zangu baada yakulipa kodi ile yule binti aliniambia nitakuwa nakuja kulala pale Mara moja moja atakapo nihitaji.Nilimkatalia katakata nikamuwleza tutaishi wote hapo mwishoni mwa mazungumzo alikubali akasema sawa but usihame moja kwa moja hostel. kwa sababu siku moja moja utaenda kulala huko rafiki zangu wakija kunitembelea kwa sababu wanajua naishi mwenyewe nikasema sawa kiukweli toka nikae nae pale tangu January nimelala hostel Mara 4 tu pindi yeye alipokuja na marafiki zake.

Ndugu zangu nimeishi nae yeye chuoni kwao anaingia masomo ya jioni anatoka SAA tatu.Ndugu zangu toka niiishi nae kanifulia nguo zangu Mara 2 tu nakudai kuwa suruali zangu za kadeti ni ngumu hawez fua.Pia Mimi namuhudumia every thing isipokuwa silipi ada tu.

Ndugu huyu binti anaishi na kaka yake wazazi wake walishafariki but kaka ake ni mwajiriwa na anadada zake wanafanyakazi nilitegemea hata kuwa tegemez kwa kila kitu kwangu.

Wiki lililopita aliens a kwao Gongolamboto kwa ajili ya kula sikukuuu. Ndugu zangu siku ya pasaka yenyewe tumewasiliana vizuri nakudai kuniambia niwahi kurudi nyumbani.Tukio la jina lililotokea siwez amino macho yangu ameaga kwao anaenda kwake kumbe anaenda kwingine nimepiga cm hapokei nikampigia dada yake ndo kuniambia kaaga nyumban toka saaa1 kasoro anaenda kwake nikamuandikia SMS kumwambia unaofanya utoto akanijibu yupo nyumbani umeme umekata lakini Dada yake ndo hayupo nyumbani.Dada take nikampigia akanambia mimi siwez sema uongo hayupo nyumbani .Mnamo saaa 5 name dk 36 usiku akanipigia cm yule binti nakuomba msamaha alikuwa kwa rafiki yake Doreen sasa yupo nyumbani.Sijamjibu chochote zaidi yakumuambia pumbafu.

Ndugu zangu nimeishi na huyu mwanamke kikubwa anapenda nimpikie ingawa hua Niko ngangari nimemikia nikihesabu kam haizidi mara 10 toka January 15 mwaka huu
Ndugu zangu naombeni ushauri nifanyaje. juuu ya haya
Mwalimu hauko peke yako hapo kuna jamaa wana SHARE
 
Ha ha ha kosa ulilofanya ni kukubal kumpangishia
Ungepanga kwako then yeye aje akute una kila kitu chako ndio maana unapigwa exile marafiki zake wakija
Watoto wa Mjini wajanja saana.....
 
mkuu huwezi kulazimisha maji kupanda mlima ,hata ukijaribu kuyavuta kwa pampu ila kaa ukijua umeme ukikatika maji yanarudi chini..

Jitafakari upya mkuu ,Ulinde uwanaume wako kwa hali na mali
 
kibovu umeongelea kumpikia,,kodi nk,,,ila hujaainisha kama papuchi huwa unapewa!! Swali ni Je! Huwa unaipata hio haki??
Je? Kama unaipata huoni kama humkazi vizuri hadi afikirie mtu wa kumpa dawa vizuri???
Pia Mwalimu kibovu una mpango wa kuzaa nae!!.
 
Matukio ya wanzuoni kawaida sana unazungumza mambo ya kupika kufua kulipa kodi VIP unamtimizia haja ya mwili?

Kulipa kodi kitu gani?
Anyways kuhusu kusaidiana washakuambiaga kwa Uzi zilizopita zake mwanamke pesa matunzo atatoa mwanaume ukweli mchungu
 
Jamaa kalipishwa kodi na matumiz anatoa then na exile bado anapigwa
Dah..... Si aliingia king mwenyewe.

Hapo Kodi yeye alilipa pengine kuna mfadhili mwingine alilipa.

Hivi Ni lazima ufuliwe?
 
Back
Top Bottom