Nawakubali sana Waislamu kwenye kuzika, nawaza niweke kwenye wosia wangu nikifa nizikwe isizidi masaa 24

Mtu akifa hakuna haja ya kumzika harakaharaka bila sababu za msingi ndio maana kuna dawa za kuzuwia maiti kuoza na mochwari zipo ili kusubiri matayarisho ya kuzika yakamilike
Kuna siasa nyingi sana kwenye hicho kinachoitwa matayarisho ya kuzika. Ndo maana mimi sitachelewesha hili tukio, nahisi huko mbeleni nitagombana sana na watu kwenye hili
 
Watu huwa wanazikwa wakiwa hai. Nina ushahidi kule kwetu Kuna mtu alizima masaa zaidi ya 7 ila ilibidi wazike kesho yake lakini jamaa aliamka na Hali Leo mzima. Sasa tungezika haraka si tungekuwa tumeua sisi??

Angalau marehemu akae hata masaa 10+ ndo azikwe Kuna faida yake pia
Walau masaa 24 tu na isizidi siku mbili
 
Hili wazo huwa linanijia. Kufukiwa na kuliwa na mafunza huwa akili inagoma kabisa sema tu sijui kama katika imani ya Kikristo kuchomwa haina madhara kiroho. Mtu unachomwa wapendwa wako wanabaki na kimkebe tu cha majivu yako kwisha kazi. Cha muhimu tu ni kwamba matter can neither be created no destroyed.

Nafuatilia hii ishu vizuri aisee
Sema hii inabidi uwe na imani fulani kabla, kwamba mwili ni kama boksi tu la mbao
 
Naifikiria sana hii kitu pale mtu anapoachwa wiki nzima hajazikwa, huwa inakuwaga huzuni mara mbili kwa wafiwa.

Solution ya hii kitu nimegundua ni mtu kuzikwa fasta fasta na sio kuchelewa zaidi ya siku mbili.

Mwaka jana kwenye family yangu kuna mtu aliumwa kinoma, nikajisemea hapa akifa nazika kesho. Ila nashukuru Mungu alimponya.

Kongole waislamu, hapo tu ndo nawakubaligi chap chap kijeshi.

Ramadhani Kareem!
Hilo hata kwenye ukiristo linawezekana tu. Andaa mazingira, weka wosia.

Na sio waislam wote wanazikwa siku hiyo hiyo.
 
Tatizo kuna watu wanadhani kumzungusha maiti mikoani au kumvundika ndio vyema zaidi
Ila kuna wengine wanasema tunazika haraka labda bado ana uhai
Hivi hata mende akiwa kafa utashindwa kujua kama ana uhai au hana?

Binadamu mbwembwe nyingi na mwisho wa siku unazika tu
Kabisa aisee, sioni ufahari kwenye kumuweka maiti mda mrefu
 
Back
Top Bottom