Kama ni tapeli kiasi hicho.......kwa nini hashtakiwi.........?.........
Ninataka kumshtaki Rose mhando kwa utapeli. Tafadhari naomba wabobezi Wa kisheria hapa Ndani. Mara ya kwanza niliandaa tukio tanga hakutokea sbb alipata ajali, nilimlipa nikasamehe. Mara ya pili niliandaa tamasha Morogoro.. Nikamlipa hakutokea kwa maelezo aliyojieleza.. Mara ya tatu nimeandaa tamasha Tanga hajatokea tena mara hii nikiwa nimeandikishana nae. Kilichoniuma zaidi ni pale aliponidanganya kwa kutaka pesa zaidi na kuniambia yuko njiani anakuja nimtumie pesa ya mafuta ya Gari.. Kumbe hata wazo la kuja Kwenye tamasha. Hana mpaka sasa ameshakula zaidi ya milioni nne kwa style. Tofauti je naweza fungua kesi mahakamani. Naomba msaada. Sasa hivi nilimpigia simu hapokei..
Pole sana kwa tatizo, naamini umeshapata msaada hadi sasa. Asikudanganye mtu eti uweke mkataba hapa! Achana na hio habari. Kama unasema hata Msama amemchoka basi samehe kwa mara ya mwisho then move forward tena kama utaweza futa kabisa huu uzi.
Nilishasikia kipindi fulani kuwa kawapiga pesa watu wa Manyara nadhani.... au kuna mtu anatumia namba yake? Mmeshaongea hivi uso kwa uso?
Acheni kucheza na akili za watu nyie...
Kama wewe unajua umempa pesa na kuandikishiana na kwenye hiyo show hajatokea na ni mara ya tatu sijui kuna haja gani ya kutuuliza sie umshtaki ama laa...wee nawe utakua promota feki tuu hujitambui ndio maana Mshamba anakupiga mapesa hovyo!!!
Fedha zenyewe Wanalipa ndogo million moja, mbili . Rose ni mwanamziki mkubwa watampaje fedha kidogo kiasi hicho?
Huyu Muhando hamnazo kwanza anatuaibisha Wakagulu bora aseme amezaliwa huko huko ugogoni Kweli masikini akipata...
Lakini nimeshawahi kumsikia mara nyingi akilalamikiwa..tatizo nini???? Kafulia au?
Nanyi wapendwa wenzake kama mnahitaji mziki wake kiasi hicho kwanini msitafute njia ya kumsaidia aenende kwa misingi ya imani yenu??? Naona inakua TOO MUCH..... ROSE ROSE ROSE doooh
hapo ndipo mtakapojua mnawahitaji sana wanasheria, wawasaidie namna ya kuandika mikataba yenu hiyo. mimi ni mwanasheria, lakini kwasababu wewe uliyeandika hapa ninakufahamu, ni mimi nimpendwa mwenzako, hakushauri achana na kupelekana mahakamani,nenda kaongee naye uso kwa uso, asipokuelewa nenda kwa mzee wake wa kanisa, asipokuelewa tafuta rafikir zake/waimbaji wenzake kadhaa waombe mwende mkasuluhishane, ....akigoma maeneo yote haya jua ni tapeli hivyo nenda mahakamani, lakini kabla haujafanya hayo usiende mahakamani kwasababu atakachokipata mahakamani (madhara) na wewe yatakuathiri. najua ninachokisema.
Swali lako limenikumbusha Kampeni za 2015 GE.
Tapelivaliyekubuhu huyo mkuuu,njombe aliwapiga milioni tatu kavu kavu. Pole