Nashauri serikali ianzishe route za daladala zinazo zunguka duara bila kurudi nyuma pia daladala zipewe namba maalumu ili zitambuliwe na abiria

Chukua mfano huu gari inatoka mawasiliano:
1. Mawasiliano → Ubungo Mataa → Riverside External →GarageMwananchi → Tabata Reli → Tabata Bima → Tabata Segerea → Mbezi → Goba → Mwenge → Mpakani → Lufungila → Mlimani City → Mawasiliano
Mtu yupo mwananchi anataka kwenda mawasiliano, hapo atapanda gari gani?
 
upo sahihi ila kwa maelezo ya mtoa mada ni kwamba hayo magari mawili yote yanatoka mbezi hadi makumbusho lakini mawili hayo yanapita njia tofauti na yatakutana makumbusho na hoja ya mtoa mada sasa hayo mabasi mawili yasirudi tena mbezi kwa kutumia njia waliyojia makumbusho bali wabadilishane yaani yule aliyepita njia namba moja atarudi mbezi kwa kutumia njia namba mbili aliyotumia mwenzie na pia wa namba mbili atarudia kwa njia namba moja ya yule mwingine hivyo watakuwa wanazungukana..
Mkuu sidhani umenielewa vizuri....... Mbezi- Makumbusho kuna magari ya route mbili,na yote yanapishan barabarani
 
Kuboresha Mfumo wa Usafiri wa Umma: Pendekezo la Njia za Duara na Namba za Daladala

Usafiri wa umma ni moja ya huduma muhimu kwa wakazi wa miji mikubwa kama Dar es Salaam, ambapo watu wengi wanategemea daladala kama njia ya usafiri wa kila siku.

Hata hivyo, kuna changamoto nyingi zinazohusiana na usafiri huu, kama vile msongamano wa magari, ucheleweshaji, na ukosefu wa mifumo ya kisasa ya usafiri.

Ili kuboresha hali hii, pendekezo la kuanzisha njia za duara za daladala na kutumia namba maalum kwa kila daladala linaweza kuwa suluhisho bora.

Route au njia ya kwanza,

1. Mawasiliano → Ubungo Mataa → Riverside External → Garage Mwananchi → Tabata Reli → Tabata Bima → Tabata Segerea → Mbezi → Goba → Mwenge → Mpakani → Lufungila → Mlimani City → Mawasiliano

Route au njia ya pili,
2. Mbezi → Kimara → Ubungo → Manzese → Magomeni → Kariakoo → Buguruni → Tabata Reli → Tabata Bima → Tabata Segerea → Mbezi

Route zingine wadau watazitaja hapa kwa mtindo wa kuzunguka.

Njia za duara ni mfumo ambapo daladala moja inazunguka maeneo fulani bila kurudi nyuma. Hii inatoa faida nyingi, ikiwa ni pamoja na:

Kupunguza Msongamano wa Magari: Kwa kuwa daladala zitakuwa zikizunguka, abiria hawatalazimika kusubiri daladala irudi tena kwenye maeneo yale yale. Hii itasaidia kupunguza msongamano kwenye barabara na kufanya usafiri kuwa wa haraka.

Kupunguza Muda wa Kusubiri: Kwa kuwa daladala zitakuwa zikizunguka kwa utaratibu, abiria wataweza kupanga safari zao kwa urahisi na kupunguza muda wa kusubiri.

Badala ya kutegemea majina ya maeneo, kuanzisha namba za daladala kutafanya usafiri kuwa rahisi kwa abiria. Hii itawawezesha abiria kutambua daladala zinazohitajika kwa kutumia namba maalum. Angalia mfano wa gari lenye namba:
View attachment 3188118

Hii inasaidia mambo yafuatayo:

1. Abiria wataweza kutambua ni daladala gani wanahitaji kuchukua kwa kutumia namba maalum, jambo litakalosaidia kupanga safari zao vizuri.

2. Namba maalum zitawawezesha abiria kutambua njia na ratiba za daladala kwa urahisi, jambo litakalosaidia kupunguza mchanganyiko wa majina ya maeneo.

Pendekezo hili lina faida kubwa kwa abiria, ikiwa ni pamoja na:

Kupanga Safari kwa Usahihi: Abiria wataweza kufahamu ni daladala gani wanahitaji kuchukua na katika muda gani, hivyo kupunguza vikwazo kwenye safari zao.

Kupunguza Muda wa Kusubiri: Mfumo wa duara utasaidia kupunguza muda wa kusubiri kwa abiria kwa sababu daladala zitakuwa zikizunguka kwa utaratibu.

Rahisi kwa Wageni: Mfumo wa namba za daladala atawawezesha wageni na wasafiri wa mara ya kwanza kutambua njia za usafiri kwa urahisi zaidi.

Mwisho kabisa kwa serikali:
Serikali inaweza kuanzisha programu ya simu au ramani za kidijitali zitakazowawezesha abiria kupata taarifa za njia na ratiba za daladala. Teknolojia hii itawawezesha abiria kujua daladala zinazopatikana na ratiba zao kwa wakati halisi, jambo litakalosaidia kuboresha usafiri wa umma.
Imagine uko Tabata Bima unataka kwenda Mwananchi itabidi uzunguke hadi Mawasiliano uanze round kurudi Mwananchi. Upotevu wa muda na fedha maana nauli itakuwa kubwa kwasababu ya mzunguko mrefu ilhali uendapi ni karibu sana.
 
Hapana mkuu yaani route zitakua nyingi sana. Kuna daladala zingine zitapita hapo Tabata Bima zikitokea Gongo la Mboto au Segerea. Route zitakua nyingi ila daladala zitakua hazirudi nyuma. Zitakua nyingi tu mkuu.
 
Kuboresha Mfumo wa Usafiri wa Umma: Pendekezo la Njia za Duara na Namba za Daladala

Usafiri wa umma ni moja ya huduma muhimu kwa wakazi wa miji mikubwa kama Dar es Salaam, ambapo watu wengi wanategemea daladala kama njia ya usafiri wa kila siku.

Hata hivyo, kuna changamoto nyingi zinazohusiana na usafiri huu, kama vile msongamano wa magari, ucheleweshaji, na ukosefu wa mifumo ya kisasa ya usafiri.

Ili kuboresha hali hii, pendekezo la kuanzisha njia za duara za daladala na kutumia namba maalum kwa kila daladala linaweza kuwa suluhisho bora.

Route au njia ya kwanza,

1. Mawasiliano → Ubungo Mataa → Riverside External → Garage Mwananchi → Tabata Reli → Tabata Bima → Tabata Segerea → Mbezi → Goba → Mwenge → Mpakani → Lufungila → Mlimani City → Mawasiliano

Route au njia ya pili,
2. Mbezi → Kimara → Ubungo → Manzese → Magomeni → Kariakoo → Buguruni → Tabata Reli → Tabata Bima → Tabata Segerea → Mbezi

Route zingine wadau watazitaja hapa kwa mtindo wa kuzunguka.

Njia za duara ni mfumo ambapo daladala moja inazunguka maeneo fulani bila kurudi nyuma. Hii inatoa faida nyingi, ikiwa ni pamoja na:

Kupunguza Msongamano wa Magari: Kwa kuwa daladala zitakuwa zikizunguka, abiria hawatalazimika kusubiri daladala irudi tena kwenye maeneo yale yale. Hii itasaidia kupunguza msongamano kwenye barabara na kufanya usafiri kuwa wa haraka.

Kupunguza Muda wa Kusubiri: Kwa kuwa daladala zitakuwa zikizunguka kwa utaratibu, abiria wataweza kupanga safari zao kwa urahisi na kupunguza muda wa kusubiri.

Badala ya kutegemea majina ya maeneo, kuanzisha namba za daladala kutafanya usafiri kuwa rahisi kwa abiria. Hii itawawezesha abiria kutambua daladala zinazohitajika kwa kutumia namba maalum. Angalia mfano wa gari lenye namba:
View attachment 3188118

Hii inasaidia mambo yafuatayo:

1. Abiria wataweza kutambua ni daladala gani wanahitaji kuchukua kwa kutumia namba maalum, jambo litakalosaidia kupanga safari zao vizuri.

2. Namba maalum zitawawezesha abiria kutambua njia na ratiba za daladala kwa urahisi, jambo litakalosaidia kupunguza mchanganyiko wa majina ya maeneo.

Pendekezo hili lina faida kubwa kwa abiria, ikiwa ni pamoja na:

Kupanga Safari kwa Usahihi: Abiria wataweza kufahamu ni daladala gani wanahitaji kuchukua na katika muda gani, hivyo kupunguza vikwazo kwenye safari zao.

Kupunguza Muda wa Kusubiri: Mfumo wa duara utasaidia kupunguza muda wa kusubiri kwa abiria kwa sababu daladala zitakuwa zikizunguka kwa utaratibu.

Rahisi kwa Wageni: Mfumo wa namba za daladala atawawezesha wageni na wasafiri wa mara ya kwanza kutambua njia za usafiri kwa urahisi zaidi.

Mwisho kabisa kwa serikali:
Serikali inaweza kuanzisha programu ya simu au ramani za kidijitali zitakazowawezesha abiria kupata taarifa za njia na ratiba za daladala. Teknolojia hii itawawezesha abiria kujua daladala zinazopatikana na ratiba zao kwa wakati halisi, jambo litakalosaidia kuboresha usafiri wa umma.
Una wazo zuri Sana ila kama Tu mwendokasi mwenye njia Yake Yuko vile hizo gari sasa zitakuwaje?
2.Bongo bado ni developing country hatujafikia level hizo za developed country
 
Ngoja tuone...
Route zitakua ndefu sana kwa hizi barabara zetu...

Cc: Mahondaw
Route hazitakua ndefu. Chukulia mfano daladala inatoka Mwenge Mpaka Buguruni inarudia route hiyohiyo mara mbili. Sasa ukaamu kuipa hiyo daladala namba 709 ikiwa na maana ni mojawapo ya daladala inayopita route ya Mwenge, kuelekea Mpakani, ipite Ubungo, riverside, External, Garage, Mwananchi, Tabata Reli, Buguruni, Ilala, Kariakoo, Jangwani, Magomeni, Morocco, Victoria, Mwenge. Kisha inaanza tena mzunguko Mwenge, kuelekea Mpakani, ipite Ubungo, riverside, External, Garage, Mwananchi, Tabata Reli, Buguruni, Ilala, Kariakoo, Jangwani, Magomeni, Morocco, Victoria, Mwenge.
 
Duara ni A B C na D (Ring Road) sasa kama either hakuna C na D au C na D kuna abiria wachache au Kutoka B kwenda C kuna mwendo mrefu Huoni kwamba its more efficient kutoka A to B and Back as well as C to D and back ?.., Hata Ulaya kuna Ring Roads au Circular Routes ila sio zote... (Mfano Birmingham UK Route 11C ni circular ila nyingine zote ni kwenda kupaki na kugeuza)

Pili namba Majina ni katika kurahisisha kueleweka and as of now ambapo routes za mabasi ni chache majina tu yanaeleweka zaidi ni rahisi kusema Keko Kariakoo au Gamboshi Kayenze kuliko basi namba 34
Mkuu umeeleza vizuri sana. Wasalimie hapo UK. Lakini hata hizi daladala za saivi zingepewa namba naona kama ingewezekana. Namba ni utambulisho wa daladala ili abiri aweze kuitambua kiurahisi. Mfano saivi ukisahau mzigo kwenye daladala sidhani kama unaweza kuupata kiurahisi. Lakini kama zingekua na namba ungeweza kukumbuka nilipanda daladala namba fulani ngoja nilisubiri lirudi nitaulizia mzigo wangu. Lakini kwa mfumo wa saivi daladala zote zinafanana majina. Namba plate haiwezi kutumiwa na abiria.
 
You mean namba exclusive kwa kila daladala ?!!! That is Impossible Ila kinachowezekana ni kila Route inakuwa na Namba ambapo sasa hivi kila Route ina majina (mfano Kariakoo Posta) na kuhusu kupotea ni kutokuwa na uaminifu mfano kwenye sehemu ambazo zimeendelea na mabasi yapo chini ya mtoa huduma mmoja mkubwa be it consurtium or whatever.., mzigo ukipotea unapelekwa katika lost property ofisini wewe unachofanya ni kupiga simu huko au kuufuata huko...
 
Back
Top Bottom