Nape amjibu Lissu: Kama CHADEMA mnachukia ufisadi, mfukuzeni Lowassa

Kama LOWASA ni fisadi kashasema mpelekeni mahakamani mbona hamumpelaki ? waziri analalamika LOWASSA fisadi si ampeleka mahakamani ? Sasa waandishi wa habari ni mahakimu wa ufisadi huoni hizo ni siasa za kitoto?
mkuuu wala usihofu atapelekwa msije mkasema anaonewa
 
nami nampongeza kwa kuwapa ukweli hao cdm. napenda kuwaeleza cdm kuwa nape si kiongozi wa kuokoteza au wa kubangaiza. nape ametengenezwa ndani ya ccm (cast in situ) na hazina kubwa kwa ccm kwa miaka mingi ijayo.
 
Nape amenukuliwa na kituo cha television cha AZAM TWO, akimjibu Tundu Lissu kuhusiana na kauli aliyoitoa kuwa ufisadi ni ajenda ya CHADEMA ya kudumu, Nape ameanza kumshambulia LOWASA , na akisema kuwa kama CHADEMA kina ajenda ya ufisadi kimfukuze LOWASSA.

Nimeshangazwa na uwezo madogo alionao NAPE katika kujenga hoja kwa sababu zifuatazo, (1) kwa nafasi aliyonayo serikalini kwa sasa hakupaswa kuanza kumshambulia mtu badala ya hoja (2) hakupaswa kumtaja Lowassa kwani ufisadi wa LOWASSA hajuathibitishwa na Tume yoyote na hata mahakama yoyote (3) Lowassa alishatoka ndani ya Chama Tawala na sasa yupo upinzani kama kulikuwa na kikwazo kumpeleka mahakamani kushindwa kumfikisha mahakamani kwa sasa maelezo au madai ya Nape ni kichekesho (4) Nyuma ya LOWASSA kuna watanzania zaidi ya millioni sita kwa kiongozi kama hakupaswa kuendeeleza madai yasiyothibitishwa (5) ukiwa ni mda mchache tuu toka tuingie toka uchaguzi NAPE kama kiongozi hakupaswa kuendeleza siasa za wakati wa uchaguzi.

Nafikiri Lowassa anapaswa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya NAPE, ili aweze kuthibitisha madai yake
mimi naweza kukubaliana na Nape kwamba Lowasa ni fisadi kwa maneno ya nape ambae ni waziri serekalini, ila namuuliza nape serikali yake inamuogopa Lowasa? na haina ubavu wa kuwashughulikia mafisadi? sasa kama yeye nape ni waziri na inawezekana hata Raisi nae anaamini kwamba Lowasa ni fisadi wanashindwa vipi kumchukulia hatua? ikiwa ushahidi wanao? hii naonyesha kwamba serikali ni dhaifu kwa Lowasa
 
Hoja ni ufisadi...ili ieleweke vizuri, lazima mtu atajwe.Hatutaki mambo ya kufumbiana macho hapa. Na usitarajie ufisadi ufanywe na kuku, ni binadamu na anayefanya ufisadi lazima abainishwe bila kupepesa macho.

Na ikiwa Lowassa anaona anaonewa (kama yeye mwenyewe anavyopenda kutumia hili neno) basi aende Mahakamani. Tutakutana nae huko. Ila napenda kurudia tena hapa, Lowassa ni fisadi mkuu.
Hamy d mbona lowasa alikwisha sema Richmond ni ya mwenyekiti na nyie mna kaa kimya kwa mwenyekiti? au nidhamu ya woga? je kama kweli lowasa fisadi kwanini mwakyembe asiseme ukweli alio uficha sasa?
 
Kama LOWASA ni fisadi kashasema mpelekeni mahakamani mbona hamumpelaki ? waziri analalamika LOWASSA fisadi si ampeleka mahakamani ? Sasa waandishi wa habari ni mahakimu wa ufisadi huoni hizo ni siasa za kitoto?
Hao anaowataka Lissu wamepelekwa mahakama ipi?

Lowasa lazima atajwe kwa sababu yeye ndiye kielelezo muafaka cha UFISADI NCHINI!
 
Hoja ni ufisadi...ili ieleweke vizuri, lazima mtu atajwe.Hatutaki mambo ya kufumbiana macho hapa. Na usitarajie ufisadi ufanywe na kuku, ni binadamu na anayefanya ufisadi lazima abainishwe bila kupepesa macho.

Na ikiwa Lowassa anaona anaonewa (kama yeye mwenyewe anavyopenda kutumia hili neno) basi aende Mahakamani. Tutakutana nae huko. Ila napenda kurudia tena hapa, Lowassa ni fisadi mkuu.

Chombo gani cha kisheria au mamlaka ipi imethibitisha ufisadi wa Lowassa?
 
Yaani wewe na mfungaji wa bao la mkono kichwani hamnazo kabisa ndo maana mna payuka hovyo hovyo. kama lowasa ni fisadi kuna kikwazo gani ya kumshitaki? P ropaganda za kishenzi hazina mashiko kwenye masikio ya watanzania

Yaani hawa watu huwa hawatumii akili vizuri ndio maana jana walipitisha bango lenye maudhui ya ubaguzi kwenye sherehe za mapinduzi.
 
Eti wote walio toka ccm chama mama afrika kumbe ule ulikuwa ni mapango maharumu .kwa rugha ya kigeni ni system tokomeza upinzani hewa tanzania .natumeshaona mtu wao ameumwa wamehenda kumcheki
 
Nape anaropoka ropoka tuu, tusubiri atakapokuwa anawekwa kati bungeni kama hayo majibu yake ya kuropoka yatamsaidia. Huyu asipo angalia ndio atakuwa wa kwanza kuonekana mzigo kwenye serikali ya Pombe
 
Shida yenu ni chuki na ubaguzi hamna lolote majambazi wakubwa.Huyo Nape Alishindwa kumwambia mwenyekiti wake aache kuiba Makonteina leo tunachokisikia hata masikio hawataki kuyasikia.Kumbe wale wateuliwa wenu kazi yao ilikuwa kukwapua Makonteina na kulikosesha Taifa mapato.
Nape hatakiwi hata kufungua mdomo wake na kuropoka
Mbona mwanasheia Lissu alishindwa kumshauri Mbowe asiuze chama kwa bei isiyo na VAT kwa fisadi Lowassa. Shida ya watu wa CHADEMA wanaona wamejificha kichakani.
 
Mbona mwanasheia Lissu alishindwa kumshauri Mbowe asiuze chama kwa bei isiyo na VAT kwa fisadi Lowassa. Shida ya watu wa CHADEMA wanaona wamejificha kichakani.
Ngoja amshauri auze kule kwenu ndio uzuri wa kuwa na wajasiria mali kuliko wapishi wa waganga wa kienyeji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom