Na kweli Diamond na wengine mna damu ya kunguni

Mi nadhani kwasababu hili swala limeshafika kwa Sir Gwajizo tutulie tu ili tupate kumfahamu viziri Almasi. Nina imani Gwaji huwa hamuonei mtu ila husema ukweli hata kama ni mchungu
 
I WISH NYIMBO ZOTE ZINGEKUWA ZA "KUFOKAFOKA" HAWA WABANA PUA HAWANA MSAADA WOWOTE KWA WATU WA CHINI. KAZI YAO KUJIPENDEKEZA CCM ESPECIALLY HUYU almasi.

Halafu asee sijui kwann imetokea automatically hawa wa kufoka wako upinzani na wabana makalio wako "yanga"
 
Kila mtu anasema lake.Nasubiri huyo mkatoliki aeleze ilikuaje akafika kituoni
 
Bwana Diamond na wengine wachache waache kuleta siasa, utani na unafiki kwenye roho na maisha ya watu.

Inaonesha wazi hauna msimamo, mara umeamua kukaa kimya mara unajishtukia unajidai "Kwakweli kwa hili siwezi kukaa kimya" , ...mara ghafla tena "Nina damu ya kunguni wacha nikae kimya...halafu bado unaawambia watanzania masikini wa download nyimbo yako kwa shilingi 300 kwamba mambo ya kuogofya ambayo hatujayazoea nchini kwetu unataka watanzania wakae kimya, mambo ya ovyo ovyo tu, sinema sinema tu za ovyo ovyo zinatokea vijana wakae kimya,wasanii wakae kimya, na kutafuta mikwaruzano na mtu kama Gwajima.. halafu wakishanunua hako kanyimbo utabaki kua tajiri, kumbuka aliepatwa na matatizo hayo ni baba mwenye familia kama wewe tu. Na ni kijana mwenzio. Sasa nashangazwa na akili zako finyu. Halafu useme Mungu atawasaidia watakua salama, lakin kama hatupazi sauti ina mana gani kumtaja Mungu akusaidie na wewe hujajisaidia hujachukua hatua ? Tunashukuru Mungu hata hivyo wamepatikana.

Na naona ume retreat ghafla baada ya kuona gwajima ametoa warning kesho kwamba " almasi itageuka maji" kwamba tutaelezwa yote na watanzania watajua mbivu na mbichi. Ama kweli una damu ya kunguni.
Choko duandomo
 
Hapana,kazi yako ni kuponda wale wote wanaomuongelea vibaya Makonda. Kazana kijana ndio ujira wako huo.

Sawa ndugu uwe na wakati mwema.....

Nayaheshimu maoni yako......

Siku utakapokuwa huru kifikra ndio siku ambayo utaanza kuishi dunia yako.....
 
Mkuu tatizo kubwa hapo ni UNAFIKI, UBINAFSI NA NJAA ndizo zinazomsumbua.
 
Mi huyo mondi toka siku nyingi nilishajua si mtetezi na huo wimbo wenyewe usikute bashite kamtuma aimbe.
 
Back
Top Bottom