Mtume Boniphace Mwamposa amtembelea Paul Makonda ofisini kwake Arusha

nampongeza kiongoz yoyote i anayethamini uwepo wa Mungu na kutambua kwamba ana msaada katika analolifanya.Hata kama anafanya kwa kuigiza.

Pongezi kwako Makonda,umeona Mbali sana.kwa sababu unaongoza watu unahitaji msaada wa Mungu kwa vyovyote vile.
 
Mt 6:5-15

Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa
maana wao wapenda kusali hali wamesimama
katika masinagogi na katika pembe za njia, ili
waonekane na watu. Amin, nawaambia,
Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe
usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani,
na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele
za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye
sirini atakujazi. Nanyi mkiwa katika kusali,
msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa;
maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa
sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi
msifanane na hao; maana Baba yenu anajua
mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. Basi
ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina
lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako
yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na
usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule
mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu,
na utukufu, hata milele. Amina.] Kwa maana
mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu
wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali
msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba
yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
 
Ohooooo!

Pengo na Mwamposa ndiyo washauri wabaya wa Makonda
Mbowe ,Lema na Lisu watu wanawaombea ni Askofu Mwamakula na Shehe Katimba ambao hata makanisa au misikiti yao haijulikani vilipo na hayajawahi kuwa na matokeo yoyote hayo maombi yao
Makonda anaombewa na watu wanaojulikana na ambao maombi yao huwa yana majibu na watu wanashuhudia waliopata majibu
 
Mbona maskini/walofilisika tuu ndiyo huanguka mapepo na kuwehuka? Walokole maskini wajitafakari kamavipi wajiuzulu...
Mbona hammwagii maji wala hamuuzii mafuta? Hamvui viatu amsilibe mafuta?
Mwamposa alipo anirudishie buku nne zangu nlinunua maji mbili na mafuta mbili na sijaona kitu oote
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda amekutana na kuzungumza na Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Inuka Uangaze, Boniface Mwamposa ofisini kwake, jijini Arusha

View attachment 2962309

Mwamposa aliyeambatana na viongozi wengine wa Kanisa hilo wamempongeza Makonda kwa kuendelea kuaminika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumtaka kuendelea kuwatumikia wananchi kwa nguvu na jitihada zake zote

Aidha, Mwamposa sambamba na watumishi wenzake wa Mungu walimuombea baraka Mkuu wa mkoa huyo sambamba na kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kumpa utashi, afya njema na nguvu za kuwatumikia wananchi wa mkoa huo

View attachment 2962315

Makonda leo, Jumamosi Aprili 13.2024 anafanya kikao cha ndani na Wakuu wa taasisi, Wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali pamoja na kusikiliza kero za wadau mbalimbali ikiwemo wa sekta ya maliasili na utalii.

Pia soma: Makonda amtumia Mwamposa kupata umaarufu kwa kisingizio cha Salamu za Rais Samia , ni mbinu duni sana
Mtumishi wa Mungu au wa shetani, watumishi wa Mungu ni wale wenye uwezo wa kinabii wa kukemea maovu. Hawa wanyakyusa ni matapeli wa kidini, wako tayari kupongeza na kuwaombea waovu ili waendelee na uovu wao
 
Mbona maskini/walofilisika tuu ndiyo huanguka mapepo na kuwehuka? Walokole maskini wajitafakari kamavipi wajiuzulu...
Mbona hammwagii maji wala hamuuzii mafuta? Hamvui viatu amsilibe mafuta?
Mwamposa alipo anirudishie buku nne zangu nlinunua maji mbili na mafuta mbili na sijaona kitu oote
Mambo ya kiimani hayaendi hivyo Bwashee.

Mungu anajibu maombi Kwa muda wake.
 
Mambo ya kiimani hayaendi hivyo Bwashee.

Mungu anajibu maombi Kwa muda wake.
Sa mbona kilasiku mwamposa anasema Leo utafunguliwa utapata baraka dabodabo?
Si aseme kama mudawako umefika Leo utafunguliwa?? Hawa wanafanya kind of a business bana tuwe wakweli lini umeona anamtoa kiongozi mapepo?
 
Uzuri wa Makonda ni kwamba keshajua kuwa "siasa ni mchezo mchafu " hivyo kajiandaa ipasavyo. Hata kama akichafuka, anajua sabuni za kujikosha zinapatikana wapi.
 
Back
Top Bottom