Mradi wa usambazaji wa maji ya ziwa Victoria - kata saba, jimbo la Igunga

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,038
974
Mbunge wa Jimbo la Igunga Nicholaus George Ngassa tarehe 20 Februari 2023 alifanya Ziara kwenye Mradi wa Usambazaji wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Vijiji vya Kata Saba za Jimbo la Igunga.

Ngassa (MB) alimtaka Mkandarasi wa Mradi kuzingatia ratiba ya utekekelezaji wa Mradi na kuongeza kasi.

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Igunga inawataarifu Wananchi wa Vijiji na Vitongoji vya Kata za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining'inila, Mwamakona, Igurubi na Kinungu kuwa mkandarasi kaanza kufikisha mabomba 'site'.

Tuendelee kutoa ushirikiano wetu ili mradi ukamilike kwa wakati. Serikali imetupatia Bilioni Ishirini na Moja (Tshs. 21,000,000,000/=) katika utekekelezaji wa Mradi wa Usambazaji wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Vijiji na Vitongoji vya Jimbo la Igunga.

"Kazi na Maendeleo"

Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Igunga
2 Machi, 2023

WhatsApp Image 2023-03-02 at 11.40.02.jpeg
 
Back
Top Bottom