SoC04 Mradi wa serikali na ukombozi wa vijana (mseuvija)

Tanzania Tuitakayo competition threads

karmaa Son

New Member
Jun 6, 2024
1
1
Ni ukweli usiopingika kwamba katika maendeleo ya nchi yeyote basi rasilimali watu ndio mhimili mkuu kwasababu wao ndio huwezesha kitu kinaitwa human capital kama ilivyotambulishwa na Theodore W. Schultz (1961) ambao ndio msingi a maendeleo katika Nyanja zote za siasa, uchumi, teknolojia, na jamii kwa ujumla wake.

Rasilimaliwatu ama watu kwa ujumla wake ni mjumuiko wa makundi tofauti tofauti ikiwemo, watoto(wakike na wakiume), vijana(wakiume na wakike{mabinti}) pamoja na wazee, makundi yote haya ni muhimu katika kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.

Andiko hili linajikita katika kundi mojawapo ambalo ni kundi la vijana juu ya namna ambayo serikali inaweza kuwa sababu ya kundi hili kuwa chachu ya mabadiliko na maendeleo.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa mujibu wa takwimu mbalimbali za hivi karibuni vijana wameonekana kuwa wengi kuliko makundi mengine ya watu, kwa mujibu wa tovuti ya www.fortune.com kufikia mwezi wa kwanza mwaka 2023 Nusu ya watu ulimwenguni ilikuwa ni walio chini ya umri wa miaka 30, kwa mujibu wa umoja wa mataifa, kufikia mwaka 2020 zaidi ya watu bilioni moja walikuwa ni vijana wa umri miaka 15 hadi 24, nchini Tanzania idadi ya vijana imeonekana kuwa kubwa pia kwani kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 vijana walikuwa ni zaidi ya milioni kumi na moja kwa waliokuwa na umri wa miaka 15 hadi 24 ikiwa ni 19.2% ya idadi ya watu wote huku wale wa miaka 15 hadi 35 wakiwa zaidi ya milioni ishirini na moja ikiwa ni 34.5%, hii inaonesha ni kwa kiasi gani kundi hili limesheheni idadi kubwa ya watu.

Kwa kutambua umuhimu wa kundi hili katika kuleta maendeleo, jumuiya za kimataifa zimeweka mkazo kwa vijana, mfano mzuri ni Malengo ya maendeleo endelevu (SDGs ) ambayo hayajaacha nyuma kundi la vijana na kwa mujibu wa umoja wa mataifa kanuni kuu kuelekea agenda ya maendeleo mwaka 2030 ni kwamba hakuna atakae achwa nyuma na katika malengo 17 ya maendeleo endelevu andiko hili linajikita zaidi katika lengo namba nane(8) ambalo ni ajira za heshima na ukuaji wa uchumi, hivyo basi yafuatayo ni mapendekezo yangu kwa serikali juu ya kundi hili muhimu kwa maendeleo.

SERIKALI IANZISHE MRADI WA BODABODA NA BAJAJI ZA SERIKALI UTAKAOAMBATANA NA MFUMO WA APP(PROGRAMU YA SIMU)

Kwa mujibu wa umoja wa mataifa, kwenye lengo namba nane la maendeleo endelevu (SDGs) kuhusu Kazi za heshima katika kujenga uchumi ni kwamba ukosefu wa ajira, uwepo wa ajira zilizo chini ya viwango na zisizo na staha yamekuwa ni mambo yanawoakabili vijana ulimwenguni ambapo kwa taarifa ya mwaka 2017 juu ya uwiano wa ukosefu wa ajira kati ya vijana na wale waliozidi umri wa ujana ni kuwa vijana wanaathirika na ukosefu wa ajira mara tatu zaidi, na hata wakipata kazi ama ajira basi hukabiliwa na ujira mdogo ama kazi zisizo rasmi.

Kwa kutambua hili huku serikali ikifahamu ukweli kwamba taifa lina idadi kubwa ya vijana basi kuna haja ya kuangalia kwa jicho la utashi ajira ya boda boda na bajaji hususan ni namna kazi hizi zimeleta ahueni kwa vijana wengi. Kuna haja ya serikali kuboresha kazi hii na kuifanya itambulike kama kazi ya heshima kwa kuanzisha utaratibu bora kwa kufanya mambo yafuatayo.

  • Serikali ianzishe chama maalum cha mradi wa Serikali kwa ukombozi wa vijana (MSEUVIJA)
  • Chama Hiki kitakuwa mahususi kwa miradi ya ukombozi wa vijana na kwa kuanza serikali itaanza na mradi wa Bodaboda na Bajaji ambao utahusisha idadi maalum ya vijana itakayopangwa na itakuwa ikiongezeka kila baada ya kipindi Fulani.

  • Kupitia mradi huu kutakuwa na pikipiki/Bajaji za Serikali katika kila mkoa Tanzania hususan kwenye ngazi za halmashauri ambapo kutakuwa na idadi maalum ya bodaboda/bajaji kuendana na idadi ya vijana watakaokuwa wamehitajika kwa wakati husika wa mradi.

  • Idadi hiyo ya vijana itapangwa na kutakuwa na haki sawa katika kupata fursa hizo kwani kutakuwa na usahili kwa kijana mmojammoja ili kuweza kupata nafasi na usahili utahusisha ujuzi madhubuti pamoja na vigezo vitavyowekwa kuendana na mradi.

  • Pikipiki/bajaji hizo zitakuwa zikimilikiwa na serikali pasipo kukandamiza mazingira ya kazi ya kijana jambo la msingi ni kuwa kijana atatakiwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi kwani atakuwa amekidhi vigezo vya usahili.

  • Kutakuwa na mfumo wa application maalum (ya simu ama kifaa cha kompyuta) utakaokua ukifuatilia mwenendo wa ufanyaji kazi wa pikipiki/bajaji hiyo(tracking) na kuwaunganisha vijana wote walio katika mradi na serikali husika, lakini pia mfumo huo utawezesha malipo mbali mbali ya mapato na ada rafiki za uanachama wa MSEUVIJA.
Mapato na faida.

Mapato.


  • Kutakuwa na malipo ya kuwa mwanachama wa MSEUVIJA, ambapo kijana mara baada ya kupita katika usahili atasajiliwa na kuwa mwanachama na atakabidhiwa pikipiki/bajaji na kitambulisho na malipo ya uanachama yatakuwa yakifanyika kwa kipindi kitakachopangwa kupitia mfumo wa application kwenda katika mapato ya serikali za halmashauri.

  • Kutakuwa na mgawanyo wa mapato kwa asilimia ambazo serikali itapanga lengo likiwa ni kumnufaisha kijana lakini kuimarisha pato la serikali kuanzia ngazi za halmashauri, mgawanyo utazingatia baina ya KIJANA na SERIKALI.

  • Kutakuwa na malipo ya aina mbili, mosi ni ada ya uanachama wa MSEUVIJA ambayo itakuwa ikilipwa na kijana kwa muda uliopangwa, pili ni malipo ya mapato ya kazi ya kijana kwenda kwa serikali ambapo serikali kupitia mfumo wa application itaweka kiwango cha malipo kwa kila kijana kwa mwezi.


  • Kijana atakuwa ni mnufaika mkuu katika mradi huu, lakini atatakiwa kutambua kwamba ana wajibu wa kuwezesha mapato ili kuleta tija ya mradi kwa pato la serikali.

  • Mapato binafsi ya kijana hayataathiriwa na serikali mradi tu kijana anatimiza wajibu wa malipo yake ya msingi anayohitajika kulipa.
FAIDA

  • Mradi huu utajumuisha faida kama kuwezesha kipato kwa kijana.
  • Kuboresha kazi ya bodaboa/bajaji kuwa na hadhi ya kutambulika na serikali.
  • Kuzalisha vijana mabalozi wa usalama barabarani hasa kutokana na vijana wa mradi kuwa mstari wa mbele katika kutii sheria za usalama barabarani na kutoa elimu kwa wengine.
  • Kuongeza chanzo cha mapato ya serikali hususan ngazi za halmashauri.
  • Kupunguza wimbi la vijana wasio na shughuli za kuwaingizia kipato cha kuweza kukidhi mahitaji muhimu.
 
Back
Top Bottom