HIMARS
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 70,957
- 98,732
Tajiri wa Urusi, Mmiliki wa Club ya Chelsea awekewa vikwazo, vikwazo hivyo vinahusu mali zote zilizo UK na Club ya Chelsea yahusika
Uuzwaji wa Chelsea umesitishwa kwa muda. Chelsea haitaruhusiwa kuuza, kununua wachezaji.
Chelsea haitaruhusiwa kuongeza mikataba ya wachezaji waliopo.
Chelsea haitaruhusiwa kuuza jezi.
Kwa mbali naona makampuni yakiiacha Chelsea.
===
Mmiliki wa Club ya Chelsea Roman Abramovich ameongezwa katika orodha ya waliowekewa vikwazo nchini Uingereza na sasa mali zake zote zilizopo Uingereza zinashikiliwa na Serikali.
Mchakato wa kuiuza Chelsea pia umezuiwa, vilevile Chelsea imezuiwa kuuza tiketi kwa Mashabiki hivyo watakaokuwa wanaingia uwanjani kwa sasa ni wale tu wenye tiketi za msimu.
Bilionea huyo wa kirusi ambaye amekua akiishi Uingereza kwa zaidi ya miaka 20 anakuwa miongoni mwa Mabilionea 7 wa Urusi ambao mali zao zimewekewa vikwazo na baadhi ya mataifa kutokana na Urusi kuvamia Ukraine.
Mbali na hayo pia Roman amepigwa marufuku kufanya miamala ya pesa na Watu binafsi na pia Wafanyabiashara wa Uingereza, pia amepigwa marufuku ya kusafiri na vikwazo vya usafiri.
Chanzo: Millad Ayo