Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Aisee... Yaani bado unaandika pumba, wewe ni hamnazo.
Asingevua watu vyeo, je asingekufa..?
Pumba nyingi sana zina virutubisho muhimu sana vya protini.

Wewe tu hujajua kwa ujinga wako.

Hakuna popote niliposema kwamba asingevua watu vyeo asingekufa.

Wewe tu hujui kusoma kwa ufahamu unaweka logical non sequitur fallacy na strawman argument fallacy.

Google that.

I know you don't know.
 
Hapana,

Sikusema hupaswi kutumia mamlaka yako.

Kiongozi anapaswa kutumia mamlaka kwa kujenga hoja, kuonesha hapa mantiki iko hivi, tufanye hivi.

Si kwa kauli za "unanijua mimi nani? Nitakuvua nyota".

Magufuli alitumia hoja ya nguvu badala ya nguvu ya hoja. Alitumia turufu yake ya mamlaka kama "argument from authority". Logical fallacy.Kwamba mtu anayeweza kuvua nyota ndiye yuko sawa, anayeweza kuvuliwa nyota akae kimya tu.

Hili ni tatizo kubwa sana kwa viongozi wetu.

Hawawezi kutumia nguvu ya hoja, wanatumia hoja ya nguvu.
Hoja Yako ni dhaifu mkuu na imeharibika kabisa uliposema JPM kafa mapema afande kabaki hai.

Una uhakika upi kama asinge muondoa Ile nyota1 JPM angebaki kuwa hai Hadi Leo?
 
Leo nimekumbuka mkasa mmoja uliotokea enzi ya awamu ya tano!

Ilikuwa ni Julai 16 ya mwaka 2019 Jumanne tulivu tu ndani ya jiji la Mwanza, ghafla Gereza Kuu la Butimba likapata ugeni wa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Basi baada ya maofisa wa juu kutonywa kuwa Rais angeweza kufika pale, wakajipanga kumpokea.

Punde si punde, hayati Magufuli akawasili na bila kupoteza muda akaomba kuongea na wafungwa ili asikie matatizo yao kama ilivyoada yake.

Wafungwa walifurahi sana kumuona Rais, basi wakaambiwa watoe kero zao. Wakazungumza wengi mpaka ilipofika kwa mfungwa mmoja aliyeamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Mmoja ya wafungwa waliopata nafasi ya kuongea na hayati Magufuli alikuwa ni Kalikenye Thomas Nyamboge, mfungwa mwenye ulemavu wa ngozi, aliyekuwa anatumikia kifungo cha Miaka 30 jela.

Mfungwa Kalikenye yeye akatoa kero yake kuhusu Afisa Usalama wa Gereza hilo, Afande Mwasifiga kuwa anashirikiana na wafungwa wengine kwa kuwapa simu waongee na watu wa nje ya Gereza kinyume na utaratibu uliowekwa lakini pia anashirikiana na baadhi ya wafungwa wenye hela kuingiza simu kwenye Gereza hilo la Butimba.

Mfungwa wa miaka 30 Jela, Bwana Thomas Kalikenye akaendelea kumsagia kunguni Afande kuwa, msako ukipita simu hazionekani na wao akina Thomas wasiohusika na kuingiza simu wanamwagiwa vitu vyao kama vile Karanga, Sukari, Sabuni na saa nyingine vinachukuliwa kwa nguvu na team ya Afande Mwasifiga.

Ghafla hayati Magufuli anabadilika na kuuliza yuko wapi huyo Afande Mwasifiga? Afande anatokea na kupiga saluti na kuanza kujibu shutuma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Afande Mwasifiga anaanza kubishana na Rais Magufuli kuhusu suala la uwepo wa simu kwa wafungwa katika Gereza la Butimba.

Afande Mwasifiga katika ubishani wake akamuambia Rais Magufuli, “huyu alitaka kuniinua” Maneno hayo yalimchefua sana Rais.

Magufuli akamwambia afande kuwa”inaonekana una dharau sana wewe” akawa ameshakasirika huku wasaidizi wa Rais wakimtonya Afande Mwasifiga aombe msamaha kwa Rais. Kweli akaomba msamaha huku akipiga saluti, lakini haikusaidia kitu.

Kama utani Rais Magufuli akamwambia ninaweza nikang’oa hizo nyota zako hapo (huyu Afande alikuwa na nyota mbili).

Basi Rais akaachana nae akamalizia kuongea na wafungwa kama alivyopanga ana akatoa agizo kwa Mkuu wa Gereza la Butimba, ole wake mfungwa yoyote aliyetoa kero anyanyaswe, basi atachukua hatua mara moja. Akamaliza akaaga akaondoka zake.

Usiku wake, Afande Mwasifiga akapokea maelekezo kuwa ameondolewa Gereza la Butimba na kupewa uhamisho wa kwenda Ukerewe.

Sambamba na hilo, akavuliwa nyota yake moja alitoka kuipata siku chache kabla ya kubishana na Rais. Hivyo basi akabaki na nyota moja tu badala ya mbili kama hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi yake.

Kama haitoshi, baada ya miezi sita akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, akastaafishwa kwa maslahi ya umma na utumishi wake ndani ya Jeshi la Magereza ukawa umefikia kikomo.

Ikumbukwe alipewa miaka mitano ya ziada jeshini baada ya kupewa nyota ya pili kabla ya kuipoteza nyota hiyo kutokana na kubishana na Rais.

Ukawa ndio mwisho wa Afande Mwasifiga, aliyepata kuwa Mkuu wa Usalama ndani ya Gereza la Butimba na waliopata kufanya nayr kazi wanakwambia alikuwa ni mjivuni, kiburi kwelikweli.

Kwasasa amerudi kwao Mbeya akiwa ni mkulima akiendeleza maisha baada ya kustaafishwa kwa maslahi ya Umma!View attachment 3164402
Umenielewesha vema mtiririko wa tukio zima kuliko hata video yenyewe. Thanks kwa update na maelezo mazuri
 
Pumba nyingi sana zina virutubisho muhimu sana vya protini.

Wewe tu hujajua kwa ujinga wako.

Hakuna popote niliposema kwamba asingevua watu vyeo asingekufa.

Wewe tu hujui kusoma kwa ufahamu unaweka logical non sequitur fallacy na strawman argument fallacy.

Google that.

I know you don't know.
Wewe ni fala tu.
Hapa nilazima nitoke nduki, bila shaka kuna chizi ameng'ang'ania keyboard ⌨️ ana type uharo.
🙌🙌🏃🏃🏃
 
Hoja Yako ni dhaifu mkuu na imeharibika kabisa uliposema JPM kafa mapema afande kabaki hai.

Una uhakika upi kama asinge muondoa Ile nyota1 JPM angebaki kuwa hai Hadi Leo?
Kwani wapi nimesema asingemuondoa nyota angebaki hai?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Hujaelewa hoja kubwa kwamba cheo ni dhamana, rais hakutakiwa kusema mimi naweza kukuondoa nyota. Ile ilikuwa lugha ya "Unanijua mimi nani? " kwa maneno mengine tu. Rais alitakiwa kutumia nguvu ya hoja, si kutumia hoja ya nguvu.

Kwa kufanya vile rais amedogosha nyota za jeshi na kuzifanya kama zinatolewa kwa hisani ya rais tu, si kwa merit ya mtu.

Kwa kusema hivyo, rais ameonesha kiburi kwamba yeye ndiye mwenye mamlaka yote. Guess what, hakuwa na mamlaka ya kukishinda kifo.

Kafa na kamuacha afande anadunda.
 
Kwani wapi nimesema kifo si lazima kwa kila mtu?

Nimesema Magufuli pamoja na ugangwe wake wote wa"naweza kukuvua nyota" kafa mapema kamuacha afande anadunda.

Sasa hapo ndiyo nimesema kifo si lazima kwa kila mtu?

Unajua kusoma kwa ufahamu wewe ngumbaru?
Kufa kwa Magufuli haku justify tabia mbovu za huyo afande aliyestaafishwa.
 
Kuna mtu nilikuwa nafuatiliaga sana comment zake huwa anaonheaga vitu vya msingi sana.....leo nimeshangaa kwenye huu uzi ame comment mashudu tupu
Mtu gani? Mtaje tu.

Inawezekana katoa mashudu yenye virutubisho vingi vya protein ni wewe tu hujaelewa.

Halafu,

Usimfuatilie mtu, fuatilia hoja.

Ukimfuatilia mtu ndiyo mwanzo wa kujifunga kwa mahaba na mtu hata akikosea usione makosa yake kwa sababu una mahaba naye.
 
Unaweza kujitapa sana kwamba unaweza kumvua mtu manyota wakati wowote lakini huyo unayemvua manyota akaendelea kuishi na wewe na tambo lako lote la kumvua manyota ukafa ukamuacha.

Cheo ni dhamana, tusipende sana kujimwambafy kwa dhamana ya cheo.

Magufuli angeweza kumsikiliza Afande na kuamua kesi kwa busara bila kujimwambafy kwamba anaweza kumvua manyota.
Watu wengi hawajui story ya "who will rid me of this troublesome priest?", inafundisha viongozi kuwa makini na kauli zao wakati wana hasira, zinaweza kuwa na madhara makubwa.

Ninavyokumbuka jamaa alijibu "nilijua utaniinua" akimaanisha kuinuliwa kujibu swali.... Sasa mkuu akadhani, anamanaisha atampandisha chati.... Ndio mwisho ukawa hivyo
 
Leo nimekumbuka mkasa mmoja uliotokea enzi ya awamu ya tano!

Ilikuwa ni Julai 16 ya mwaka 2019 Jumanne tulivu tu ndani ya jiji la Mwanza, ghafla Gereza Kuu la Butimba likapata ugeni wa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Basi baada ya maofisa wa juu kutonywa kuwa Rais angeweza kufika pale, wakajipanga kumpokea.

Punde si punde, hayati Magufuli akawasili na bila kupoteza muda akaomba kuongea na wafungwa ili asikie matatizo yao kama ilivyoada yake.

Wafungwa walifurahi sana kumuona Rais, basi wakaambiwa watoe kero zao. Wakazungumza wengi mpaka ilipofika kwa mfungwa mmoja aliyeamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Mmoja ya wafungwa waliopata nafasi ya kuongea na hayati Magufuli alikuwa ni Kalikenye Thomas Nyamboge, mfungwa mwenye ulemavu wa ngozi, aliyekuwa anatumikia kifungo cha Miaka 30 jela.

Mfungwa Kalikenye yeye akatoa kero yake kuhusu Afisa Usalama wa Gereza hilo, Afande Mwasifiga kuwa anashirikiana na wafungwa wengine kwa kuwapa simu waongee na watu wa nje ya Gereza kinyume na utaratibu uliowekwa lakini pia anashirikiana na baadhi ya wafungwa wenye hela kuingiza simu kwenye Gereza hilo la Butimba.

Mfungwa wa miaka 30 Jela, Bwana Thomas Kalikenye akaendelea kumsagia kunguni Afande kuwa, msako ukipita simu hazionekani na wao akina Thomas wasiohusika na kuingiza simu wanamwagiwa vitu vyao kama vile Karanga, Sukari, Sabuni na saa nyingine vinachukuliwa kwa nguvu na team ya Afande Mwasifiga.

Ghafla hayati Magufuli anabadilika na kuuliza yuko wapi huyo Afande Mwasifiga? Afande anatokea na kupiga saluti na kuanza kujibu shutuma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Afande Mwasifiga anaanza kubishana na Rais Magufuli kuhusu suala la uwepo wa simu kwa wafungwa katika Gereza la Butimba.

Afande Mwasifiga katika ubishani wake akamuambia Rais Magufuli, “huyu alitaka kuniinua” Maneno hayo yalimchefua sana Rais.

Magufuli akamwambia afande kuwa”inaonekana una dharau sana wewe” akawa ameshakasirika huku wasaidizi wa Rais wakimtonya Afande Mwasifiga aombe msamaha kwa Rais. Kweli akaomba msamaha huku akipiga saluti, lakini haikusaidia kitu.

Kama utani Rais Magufuli akamwambia ninaweza nikang’oa hizo nyota zako hapo (huyu Afande alikuwa na nyota mbili).

Basi Rais akaachana nae akamalizia kuongea na wafungwa kama alivyopanga ana akatoa agizo kwa Mkuu wa Gereza la Butimba, ole wake mfungwa yoyote aliyetoa kero anyanyaswe, basi atachukua hatua mara moja. Akamaliza akaaga akaondoka zake.

Usiku wake, Afande Mwasifiga akapokea maelekezo kuwa ameondolewa Gereza la Butimba na kupewa uhamisho wa kwenda Ukerewe.

Sambamba na hilo, akavuliwa nyota yake moja alitoka kuipata siku chache kabla ya kubishana na Rais. Hivyo basi akabaki na nyota moja tu badala ya mbili kama hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi yake.

Kama haitoshi, baada ya miezi sita akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, akastaafishwa kwa maslahi ya umma na utumishi wake ndani ya Jeshi la Magereza ukawa umefikia kikomo.

Ikumbukwe alipewa miaka mitano ya ziada jeshini baada ya kupewa nyota ya pili kabla ya kuipoteza nyota hiyo kutokana na kubishana na Rais.

Ukawa ndio mwisho wa Afande Mwasifiga, aliyepata kuwa Mkuu wa Usalama ndani ya Gereza la Butimba na waliopata kufanya nayr kazi wanakwambia alikuwa ni mjivuni, kiburi kwelikweli.

Kwasasa amerudi kwao Mbeya akiwa ni mkulima akiendeleza maisha baada ya kustaafishwa kwa maslahi ya Umma!View attachment 3164402
Kalikenye yupo bunda
 
Back
Top Bottom