Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Leo nimekumbuka mkasa mmoja uliotokea enzi ya awamu ya tano!

Ilikuwa ni Julai 16 ya mwaka 2019 Jumanne tulivu tu ndani ya jiji la Mwanza, ghafla Gereza Kuu la Butimba likapata ugeni wa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Basi baada ya maofisa wa juu kutonywa kuwa Rais angeweza kufika pale, wakajipanga kumpokea.

Punde si punde, hayati Magufuli akawasili na bila kupoteza muda akaomba kuongea na wafungwa ili asikie matatizo yao kama ilivyoada yake.

Wafungwa walifurahi sana kumuona Rais, basi wakaambiwa watoe kero zao. Wakazungumza wengi mpaka ilipofika kwa mfungwa mmoja aliyeamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Mmoja ya wafungwa waliopata nafasi ya kuongea na hayati Magufuli alikuwa ni Kalikenye Thomas Nyamboge, mfungwa mwenye ulemavu wa ngozi, aliyekuwa anatumikia kifungo cha Miaka 30 jela.

Mfungwa Kalikenye yeye akatoa kero yake kuhusu Afisa Usalama wa Gereza hilo, Afande Mwasifiga kuwa anashirikiana na wafungwa wengine kwa kuwapa simu waongee na watu wa nje ya Gereza kinyume na utaratibu uliowekwa lakini pia anashirikiana na baadhi ya wafungwa wenye hela kuingiza simu kwenye Gereza hilo la Butimba.

Mfungwa wa miaka 30 Jela, Bwana Thomas Kalikenye akaendelea kumsagia kunguni Afande kuwa, msako ukipita simu hazionekani na wao akina Thomas wasiohusika na kuingiza simu wanamwagiwa vitu vyao kama vile Karanga, Sukari, Sabuni na saa nyingine vinachukuliwa kwa nguvu na team ya Afande Mwasifiga.

Ghafla hayati Magufuli anabadilika na kuuliza yuko wapi huyo Afande Mwasifiga? Afande anatokea na kupiga saluti na kuanza kujibu shutuma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Afande Mwasifiga anaanza kubishana na Rais Magufuli kuhusu suala la uwepo wa simu kwa wafungwa katika Gereza la Butimba.

Afande Mwasifiga katika ubishani wake akamuambia Rais Magufuli, “huyu alitaka kuniinua” Maneno hayo yalimchefua sana Rais.

Magufuli akamwambia afande kuwa”inaonekana una dharau sana wewe” akawa ameshakasirika huku wasaidizi wa Rais wakimtonya Afande Mwasifiga aombe msamaha kwa Rais. Kweli akaomba msamaha huku akipiga saluti, lakini haikusaidia kitu.

Kama utani Rais Magufuli akamwambia ninaweza nikang’oa hizo nyota zako hapo (huyu Afande alikuwa na nyota mbili).

Basi Rais akaachana nae akamalizia kuongea na wafungwa kama alivyopanga ana akatoa agizo kwa Mkuu wa Gereza la Butimba, ole wake mfungwa yoyote aliyetoa kero anyanyaswe, basi atachukua hatua mara moja. Akamaliza akaaga akaondoka zake.

Usiku wake, Afande Mwasifiga akapokea maelekezo kuwa ameondolewa Gereza la Butimba na kupewa uhamisho wa kwenda Ukerewe.

Sambamba na hilo, akavuliwa nyota yake moja alitoka kuipata siku chache kabla ya kubishana na Rais. Hivyo basi akabaki na nyota moja tu badala ya mbili kama hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi yake.

Kama haitoshi, baada ya miezi sita akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, akastaafishwa kwa maslahi ya umma na utumishi wake ndani ya Jeshi la Magereza ukawa umefikia kikomo.

Ikumbukwe alipewa miaka mitano ya ziada jeshini baada ya kupewa nyota ya pili kabla ya kuipoteza nyota hiyo kutokana na kubishana na Rais.

Ukawa ndio mwisho wa Afande Mwasifiga, aliyepata kuwa Mkuu wa Usalama ndani ya Gereza la Butimba na waliopata kufanya nayr kazi wanakwambia alikuwa ni mjivuni, kiburi kwelikweli.

Kwasasa amerudi kwao Mbeya akiwa ni mkulima akiendeleza maisha baada ya kustaafishwa kwa maslahi ya Umma!View attachment 3164402
Afande Mwasifiga, siku Magufuli anadumbukizwa, kaburini, alikuwa anajisikiaje ?
 
Kuna uonevu wa kiaina ulifanywa mwingi sana,tatizo tukimpenda hata marehemu,hatupendi aambiwe ukweli,au akosolewe.Kuna doctor pale Tabora alishughukiwa kisa alienda hospital binafsi kufuata maslah kwa ajili ya maisha yake.Baba akasahau aliacha ualimu akaingia kwenye siasa.Tuamini ya Mungu ni mengi
 
Logical non sequitur fallacy.

Hataishi milele ila Magufuli katangulia kufa kamuacha afande analifaidi jua bado.

Magufuli na mabobish yake yote ya "Naweza kukuvua manyota" hayakumsaidia kukishinda kifo.

Cheo ni dhamana, usikitumie kujimwambafy na kutishia watu.

Duniani wote tunapita tu.
Jua analifaidi au linamchoma ? Alafu kutangulia sio zambi na wala haiashirii ukitangulia ndio wewe ni mkosaji sana kuliko aliebaki.

Mbona Babu yako alimdunda sana Bibi yako na ndie alitangulia akamwacha bibi yako.
 
Kuna uonevu wa kiaina ulifanywa mwingi sana,tatizo tukimpenda hata marehemu,hatupendi aambiwe ukweli,au akosolewe.Kuna doctor pale Tabora alishughukiwa kisa alienda hospital binafsi kufuata maslah kwa ajili ya maisha yake.Baba akasahau aliacha ualimu akaingia kwenye siasa.Tuamini ya Mungu ni mengi
Magufuli alikuwa mpuuzi sana kwenye ubishiubishi na watendaji.

Najua serikalini wapigaji wengi na rais anatakiwa kukomaa, ila Magufuli alikuwa anabishana kwa ligi. Hataki kushindwa.

Ila kiboko yake ni yule jamaa aliyebishana naye kuhusu kuweka lift hospitali, Magufuli akamuuliza kwani wewe nyumbani kwako kuna lift? Jamaa akamjibu nyumbani kwangu si hospitali.

Halafu jamaa hata hakujibu kwa kiburi, ni kama alikuwa anamuelewesha rais tu kitaalamu lift hospitali ni muhimu, kuna wagongwa wataihitaji. Magufuli na ushamba wake hataki kuelewa somo.

Pale wenye akili walimuona Magufuli mjinga sana kulinganisha hospitali na nyumbani kwa mtu.
 
Jua analifaidi au linamchoma ? Alafu kutangulia sio zambi na wala haiashirii ukitangulia ndio wewe mi mkosaji sana kuliko aliebaki.

Mbona Babu yako alimdunda sana Bibi yako na ndie alitangulia akamwacha bibi yako.
Mimi mtu asiyejua tofauti ya zambi na dhambi siwezi kufanya mjadala naye wa kimantiki.

Kama hajui tofauti ya zambi na dhambi kiswahili atajuaje logical fallacy kilatini?

Kutojua tofauti ya zambi na dhambi ni ishara ya umbumbumbu na mimi sitaki mijadala na mbumbumbu.
 
Leo nimekumbuka mkasa mmoja uliotokea enzi ya awamu ya tano!

Ilikuwa ni Julai 16 ya mwaka 2019 Jumanne tulivu tu ndani ya jiji la Mwanza, ghafla Gereza Kuu la Butimba likapata ugeni wa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Basi baada ya maofisa wa juu kutonywa kuwa Rais angeweza kufika pale, wakajipanga kumpokea.

Punde si punde, hayati Magufuli akawasili na bila kupoteza muda akaomba kuongea na wafungwa ili asikie matatizo yao kama ilivyoada yake.

Wafungwa walifurahi sana kumuona Rais, basi wakaambiwa watoe kero zao. Wakazungumza wengi mpaka ilipofika kwa mfungwa mmoja aliyeamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Mmoja ya wafungwa waliopata nafasi ya kuongea na hayati Magufuli alikuwa ni Kalikenye Thomas Nyamboge, mfungwa mwenye ulemavu wa ngozi, aliyekuwa anatumikia kifungo cha Miaka 30 jela.

Mfungwa Kalikenye yeye akatoa kero yake kuhusu Afisa Usalama wa Gereza hilo, Afande Mwasifiga kuwa anashirikiana na wafungwa wengine kwa kuwapa simu waongee na watu wa nje ya Gereza kinyume na utaratibu uliowekwa lakini pia anashirikiana na baadhi ya wafungwa wenye hela kuingiza simu kwenye Gereza hilo la Butimba.

Mfungwa wa miaka 30 Jela, Bwana Thomas Kalikenye akaendelea kumsagia kunguni Afande kuwa, msako ukipita simu hazionekani na wao akina Thomas wasiohusika na kuingiza simu wanamwagiwa vitu vyao kama vile Karanga, Sukari, Sabuni na saa nyingine vinachukuliwa kwa nguvu na team ya Afande Mwasifiga.

Ghafla hayati Magufuli anabadilika na kuuliza yuko wapi huyo Afande Mwasifiga? Afande anatokea na kupiga saluti na kuanza kujibu shutuma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Afande Mwasifiga anaanza kubishana na Rais Magufuli kuhusu suala la uwepo wa simu kwa wafungwa katika Gereza la Butimba.

Afande Mwasifiga katika ubishani wake akamuambia Rais Magufuli, “huyu alitaka kuniinua” Maneno hayo yalimchefua sana Rais.

Magufuli akamwambia afande kuwa”inaonekana una dharau sana wewe” akawa ameshakasirika huku wasaidizi wa Rais wakimtonya Afande Mwasifiga aombe msamaha kwa Rais. Kweli akaomba msamaha huku akipiga saluti, lakini haikusaidia kitu.

Kama utani Rais Magufuli akamwambia ninaweza nikang’oa hizo nyota zako hapo (huyu Afande alikuwa na nyota mbili).

Basi Rais akaachana nae akamalizia kuongea na wafungwa kama alivyopanga ana akatoa agizo kwa Mkuu wa Gereza la Butimba, ole wake mfungwa yoyote aliyetoa kero anyanyaswe, basi atachukua hatua mara moja. Akamaliza akaaga akaondoka zake.

Usiku wake, Afande Mwasifiga akapokea maelekezo kuwa ameondolewa Gereza la Butimba na kupewa uhamisho wa kwenda Ukerewe.

Sambamba na hilo, akavuliwa nyota yake moja alitoka kuipata siku chache kabla ya kubishana na Rais. Hivyo basi akabaki na nyota moja tu badala ya mbili kama hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi yake.

Kama haitoshi, baada ya miezi sita akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, akastaafishwa kwa maslahi ya umma na utumishi wake ndani ya Jeshi la Magereza ukawa umefikia kikomo.

Ikumbukwe alipewa miaka mitano ya ziada jeshini baada ya kupewa nyota ya pili kabla ya kuipoteza nyota hiyo kutokana na kubishana na Rais.

Ukawa ndio mwisho wa Afande Mwasifiga, aliyepata kuwa Mkuu wa Usalama ndani ya Gereza la Butimba na waliopata kufanya nayr kazi wanakwambia alikuwa ni mjivuni, kiburi kwelikweli.

Kwasasa amerudi kwao Mbeya akiwa ni mkulima akiendeleza maisha baada ya kustaafishwa kwa maslahi ya Umma!View attachment 3164402
Cc Stuxnet
 
Umepuy
Unaweza kujitapa sana kwamba unaweza kumvua mtu manyota wakati wowote lakini huyo unayemvua manyota akaendelea kuishi na wewe na tambo lako lote la kumvua manyota ukafa ukamuacha.

Cheo ni dhamana, tusipende sana kujimwambafy kwa dhamana ya cheo.

Magufuli angeweza kumsikiliza Afande na kuamua kesi kwa busara bila kujimwambafy kwamba anaweza kumvua manyota.
Umepuyanga kijana...
Acha kujitetea.
Kifo ni lazima kwa kila mtu.
Atakufa Jambazi, Padri, Shekhe, asiye na dini, mwehu, mzinzi, mstaarabu, mkorofi, mtoto, mkubwa, raisi, raia na n. K na huwezi kwepa
 
Back
Top Bottom