Mhe. Bashe tengua kauli...

Mhe. Bashe kwanza hongera sana kwa kuingia bungeni baada ya kufanyiwa figisu nyingi 2010 na hatimaye ukaenguliwa eti wewe si mtanzania. Na kwa kipindi kifupi tu jina lako limeanza kuingia vichwani mwa watanzania wachache wanofuatilia bunge manane ya usiku.

Nakuja hapa kukutaka utengue kauli yako iliyonukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba "ualimu ni kichaka cha waliofeli". Binafsi sijakusikia wala kukuona moja kwa moja kwa kuwa hilo bunge lenu linalooneshwa manane ya usiku wala sina habari nalo. Lkn kwa kuwa hujakanusha nukuu hii iliyoenea katika vyombo vyote vya habari bila shaka uliitoa kauli hii.

Kauli hii inawezekana uliitoa kwa dhamira njema kabisa lkn hukufikiria madhara yake kwa ualimu na walimu. Maana inatweza na kudhalilisha ualimu na walimu. Kwa mtu wa hadhi yako unayesifika kuwa mwanasiasa machachari unayechipukia unapaswa kuwa makini kabla ya kufungua kinywa chako.

Jiulize maswali yafuatayo mhe. Bashe.
1. Kufeli maana yake nn?
2. Taasisi nyingine za serikali hakuna waliofeli?

Elimu ni uwezo wa kutambua na kupambana/kukabiliana na changamoto zilizopo ktk mazingira. Anaye elimika anapaswa kuwa huru kifikra na kiuchumi.

Kimsingi elimu ktk taifa letu haimpi msomi ujuzi na uwezo wa kutambua na kupambana na changamoto zinazomzunguka. Tumeshuhudia mkuu wa mkoa aliyekuwa mstari wa mbele kuhimiza vijana wajiajiri akilia njaa baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo.

Yawezekana hata wewe Bashe unajiona mwenye kufaulu kwasabb tu umepata ubunge. Nje ya ubunge huna mbinu ya kupata mlo au kuendesha maisha

Tunaona maprofesa wakililia mikataba ya kuendelea na kazi hata baada ya kufikia umri wa kustaafu. Hii ni ishara tosha kuwa hawana ujuzi na uwezo wa kupambana nje ya ajira.

Lkn kama taasisi nyingine zina waliofaulu. Inakuwaje walimu waliofeli wakaingia kwenye ajira ili hali mifumo ya kuajiri serikalini imeshikwa na walioelimika??
Mhe. Bashe ulikuwa too specific katika kauli yako. Ingekuwa vema ungesema "serikalini ni kichaka cha waliofeli".
-bungeni hakuna waliofeli?
-polisi hakuna waliofeli?
-mahospitalini hakuna waliofeli?
- jeshinini hakuna waliofeli?
- wizarani hakuna waliofeli?
-tra, pccb, ewura, n.k hakuna waliofeli huko?

Nionavyo mm watanzania wote wamefeli. Ndiyo maana hata chama chako kikakuzushia kashfa zisizo na miguu kuwa wewe ni msomali ili tu usiwe mbunge. Waliofaulu wanaweza kufanya hivyo?

Lkn waliofaulu wamefanya nn ktk nchi hii? Mm naona kuna walioenda shule na kupata vyeti tu. Ndiyo maana nchi ina kila kitu halafu umaskini umekithiri. Mpk leo nchi inaagiza vijiti vya kuchokonolea meno!!!? Hao waliofaulu wako wapi?

Majengo, yanaanguka hovyo, miji yetu yote haijapangwa, viwanda vinakufa kuna waliofaulu kweli? Kuna watakao kuja na majibu ya watunga sera na sheria. Hawa pia wamefaulu??

Daah!! Niishie hapa.
Wako Kigodoro.
sijaona tatizo LA kauli ya bashe, ili tuendelee tunahitahi kusema ukweli bila kujali utamuumiza nani,
 
No research no right to speak. Hvi mmenda nacte mkaona wanaotakiwa kusoma ualimu?
Baadhi yenu humu hamna sifa za kusomea ualimu.
By the way, mmi ni mwalimu kiukweli sijui maana ya wamefeli. Zero ndo faili lakini four ni pass. Sijui wanamaanishaga nini?
Tatizo hapa nchini kila mtu anaona anajua ualimu kumbe mbulula kabisa!!!
 
Ualimu ni sehemu nyeti huwezi kulinganisha na sehemu ulizozitaja.Wote uliowataja wanatokana na mwalimu, hivyo mwalimu akiwa mbovu kila kitu kinakuwa kibovu.
Let us face the reality! Kuna mwanafunzi aliyepata division 1 or 2 (nadhani hata three??????) akaenda ualimu?
Ebu tafuta majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha dar es salaam kusomea B.A (Ed) au BSc ( Ed) kwa miaka ya 2012,2013 na 2014 (kama sample) ukisha maliza njoo ufute ki posti chako!
 
Please watu wanakwenda kutafuta ajira za ualimu na mikopo hasa sisis tunaotoka familia masikini. Tatizo la Watanzania hawataki kusikia ukweli kama CCM. ! Sio kwa vile wanataka kusoma ualimu! please. Actually wenye akili zao wakipata hiyo degree nzuri na form six nzuri wanatafuta kazi zingine maana vyeti vyao ni vizuri. Kama imekugusa ukweli ni huo.
 
Kwa hiyo wakisha maliza kusoma wanaenda kuwa akina nani?
 
Hata einstein na billgate walifeli shule ila sio maisha

Billgate ni university drop out mkuu wangu...jamaa alikuwa kichwa balaa...tena alidrop Harvard kama sijakosea...kuhusu Einstein ebu fuatilia mambo ya kemia na fizikia utagundua mambo makubwa aliyoyafanya kamanda wangu...
 
Kwa hiyo wakisha maliza kusoma wanaenda kuwa akina nani?
Wanajishikiza kwenye ualimu muda mfupi maana vyeti vyao ni vizuri wanajiliwa kirahisi. Hata administration/rasilimali watu wanaajiliwa maana kwenye ualimu unasoma hata human resources management , psychology, philosophy of education and the like
 
Acheni blaa blaaa ualimu ni kichaka cha waliofeli kweli japo sio wote, ukienda kwny shule zote kubwa kama International school of Tanganyika hutakuta walimu wengi kutoka Tanzania kwa kuwa hawana qualuty zinaohitajika.
Kuna siku nilipitia Mtihani wa kijukuu changu cha darasa la nne somo la kiingerza anasoma shule za wakimbiza Mwenge na Wazalendo nikashangaa swali lina majibu ya kuchagua lakini hayo ya kuchagua hakuna jibu sahihi maswali karibia yote.
Kama fani zingine zina vilaza hao wasemwe pia sio kuleta blaa blaa! Hatua ya kwanza kutatua tatizo ni kukiri uwepo wa Tatizo
 
Nadhani huyo ni mwalimu anajitetea. Kuna mzazi anaweza kukubali mtoto wake Na div one aende ualimu baadala ya kwenda fomu faivu
Hilo ndilo swala ambalo jamii inatakiwa kulitafutia jibu. Nilipokuwa mdogo walimu walikuwa wakiheshimika sana hata kusomea ualimu ilikuwa sifa nzuri. Kukufikia miaka ya 80 hadhi ya mwalimu ikaanza kushuka, vijana wakagundua kufanya ulanguzi unapata pesa kuliko mwalimu. Na ufaulu ukaanza kuoroomoka kwa kasi. Kama jamii ili kumfanya mfaulu au mzazi akubali mwanae aliemgharimia aende ualimu, itabidi mtazamo wa Serikali kuhusu maslahi na madai ya walimu yashughulikiwe, kuboresha mazingira ya kazi, japo sehemu nyingi zinahitaji hili tuweke kiupambele taaluma hii. Sijasikia walimu, wa shule chini ya upili, wakilalamikia maslahi katika nchi zilizoendelea. Kupanga ni kuchagua.
 
Acheni blaa blaaa ualimu ni kichaka cha waliofeli kweli japo sio wote, ukienda kwny shule zote kubwa kama International school of Tanganyika hutakuta walimu wengi kutoka Tanzania kwa kuwa hawana qualuty zinaohitajika.
Kuna siku nilipitia Mtihani wa kijukuu changu cha darasa la nne somo la kiingerza anasoma shule za wakimbiza Mwenge na Wazalendo nikashangaa swali lina majibu ya kuchagua lakini hayo ya kuchagua hakuna jibu sahihi maswali karibia yote.
Kama fani zingine zina vilaza hao wasemwe pia sio kuleta blaa blaa! Hatua ya kwanza kutatua tatizo ni kukiri uwepo wa Tatizo
Afadhali umesema nimeandika humu nimeshambuliwa lakini sijaacha maana ndio ukweli. Walimu hawataki kusikia hilo. Tutalisema potelea mbali
 
Lkn unaweza ukawa na div 1 na bado ukashindwa tendo la kufundisha yale unayoyajua. kwa hiyo ualimu bado ni kazi ambayo haitegemei div 1 au 2 bila wito
 
msingi wa maisha ya mwanadamu umebebwa na dhana pana ya elimu , na wale waliobeba dhana hii ya elimu kwa mataifa mengi ni walimu sasa kama walimu watakuwa ni watu waliofeli maanake ni kwamba walimu watatengeneza jamii ya watu waliofeli, hata hao mnawaona wamefaulu kwa alama za juu nao vilevile ni felia kwakua kizazi chake ni cha walimu felia, leo china wanao mfumo wa wale walio faulu ndiyo wanapata daraja la kuwa walimu wa shule za upili.
my take Bashe yupo sahihi kwa hili na walimu ni wakati sasa wa kuubali ukweli huu leo hii mwalimu unakuta mwalimu hajawahi hata kusoma kitabu cha kuongeza maarifa hii nini kama sio ...
 
Bashe kasema ukweli ni kawaida kushambuliwa. Sekta ya elimu imejaa MAKAPI hasa walimu wa diploma na cheti. Uongo sijui uko wapi hapo, juzi tumeona ya St. Joseph waliofeli form four wanaandaliwa kuwa walimu wa ngazi ya shahada, kwanini hawakupelekwa udaktari au fani nyingine kama ualimu sio chaka la waliofeli? Four ya 33 hata huo upolisi uliosema hupati. Then leo tumeona yaliyotokea kule UDOM kwa hicho kiitwacho special diploma.
 
Ualimu ni sehemu nyeti huwezi kulinganisha na sehemu ulizozitaja.Wote uliowataja wanatokana na mwalimu, hivyo mwalimu akiwa mbovu kila kitu kinakuwa kibovu.
Let us face the reality! Kuna mwanafunzi aliyepata division 1 or 2 (nadhani hata three??????) akaenda ualimu?

kwa hiyo hakuna mwalimu mwenye dv 1 au 2 umefanya utafiti au umekurupuka tu kuandika?
 
Ata Rais wetu nae alifeli
Ata waziri mkuu nae alifeli
Ata Makamu wa Rais nae alifeli
Ata Nyerere nae alifeli......
Inshort Watanzania wote Tumefeli maana tumefika apa tulipo kwasababu Tulifundishwa na walimu waliofeli .
Hivi Somalia Hawajafeli Km Taifa?
nakushukuru mkuu. kiukweli kwenye mambo mengine tuache utani. hoja ya Bashe inahitaji umakini sana kuisifia. huyu amedhalilisha kazi ya uwalimu japo miongoni mwa baadhi yetu wanashangilia ingawa wamefundishwa na haohao waliofeli.
 
kwa hiyo hakuna mwalimu mwenye dv 1 au 2 umefanya utafiti au umekurupuka tu kuandika?
Kuna post nyingi humu tumeandika kwa nini wenye div 1&2 walikwenda ualimu. By the way, kukurupuka ni tusi, jiepushe na kauli hiyo, nimekustahi. kama ni mwalimu, pole sana. Hivi mshahara huwa ni shilingi ngapi, nasikia siku hizi wanachapwa na viboko na maDC!
 
Mm Nina hakika wapo wengi sana wana ufaulu wa division 1 or 2 ni waalimu. Huo ni udhalilishaji sana yaani mm nmeshangaa sana na mm naenda kwenye hili chaka la walio feli maana ndio wanatuongoza na nawakubali sana kuanzia nyerere mpaka magufuli. Binafsi nimekasirishwa na kauli hiyo. Ni vyema serikali imwambie bashe awe hata anajitolea kipindi kimoja kwa wiki ili waliofaulu wenzake waungane na wanafunzi wafaulu zaidi.
Mhe. Bashe kwanza hongera sana kwa kuingia bungeni baada ya kufanyiwa figisu nyingi 2010 na hatimaye ukaenguliwa eti wewe si mtanzania. Na kwa kipindi kifupi tu jina lako limeanza kuingia vichwani mwa watanzania wachache wanofuatilia bunge manane ya usiku.

Nakuja hapa kukutaka utengue kauli yako iliyonukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba "ualimu ni kichaka cha waliofeli". Binafsi sijakusikia wala kukuona moja kwa moja kwa kuwa hilo bunge lenu linalooneshwa manane ya usiku wala sina habari nalo. Lkn kwa kuwa hujakanusha nukuu hii iliyoenea katika vyombo vyote vya habari bila shaka uliitoa kauli hii.

Kauli hii inawezekana uliitoa kwa dhamira njema kabisa lkn hukufikiria madhara yake kwa ualimu na walimu. Maana inatweza na kudhalilisha ualimu na walimu. Kwa mtu wa hadhi yako unayesifika kuwa mwanasiasa machachari unayechipukia unapaswa kuwa makini kabla ya kufungua kinywa chako.

Jiulize maswali yafuatayo mhe. Bashe.
1. Kufeli maana yake nn?
2. Taasisi nyingine za serikali hakuna waliofeli?

Elimu ni uwezo wa kutambua na kupambana/kukabiliana na changamoto zilizopo ktk mazingira. Anaye elimika anapaswa kuwa huru kifikra na kiuchumi.

Kimsingi elimu ktk taifa letu haimpi msomi ujuzi na uwezo wa kutambua na kupambana na changamoto zinazomzunguka. Tumeshuhudia mkuu wa mkoa aliyekuwa mstari wa mbele kuhimiza vijana wajiajiri akilia njaa baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo.

Yawezekana hata wewe Bashe unajiona mwenye kufaulu kwasabb tu umepata ubunge. Nje ya ubunge huna mbinu ya kupata mlo au kuendesha maisha

Tunaona maprofesa wakililia mikataba ya kuendelea na kazi hata baada ya kufikia umri wa kustaafu. Hii ni ishara tosha kuwa hawana ujuzi na uwezo wa kupambana nje ya ajira.

Lkn kama taasisi nyingine zina waliofaulu. Inakuwaje walimu waliofeli wakaingia kwenye ajira ili hali mifumo ya kuajiri serikalini imeshikwa na walioelimika??
Mhe. Bashe ulikuwa too specific katika kauli yako. Ingekuwa vema ungesema "serikalini ni kichaka cha waliofeli".
-bungeni hakuna waliofeli?
-polisi hakuna waliofeli?
-mahospitalini hakuna waliofeli?
- jeshinini hakuna waliofeli?
- wizarani hakuna waliofeli?
-tra, pccb, ewura, n.k hakuna waliofeli huko?

Nionavyo mm watanzania wote wamefeli. Ndiyo maana hata chama chako kikakuzushia kashfa zisizo na miguu kuwa wewe ni msomali ili tu usiwe mbunge. Waliofaulu wanaweza kufanya hivyo?

Lkn waliofaulu wamefanya nn ktk nchi hii? Mm naona kuna walioenda shule na kupata vyeti tu. Ndiyo maana nchi ina kila kitu halafu umaskini umekithiri. Mpk leo nchi inaagiza vijiti vya kuchokonolea meno!!!? Hao waliofaulu wako wapi?

Majengo, yanaanguka hovyo, miji yetu yote haijapangwa, viwanda vinakufa kuna waliofaulu kweli? Kuna watakao kuja na majibu ya watunga sera na sheria. Hawa pia wamefaulu??

Daah!! Niishie hapa.
Wako Kigodoro.

Mkuu Kigodoro Kwa kauli yako mwenyewe kama ulivyopambanua tafasiri ya elimu. Inawezekana hata wewe kutokana na elimu uliyoipata imekupa uwezo mdogo wa kuchambua na kupanua mambo. Hebu tuwe realistic Mkuu kidogo, mie nadhani Bashe amesema Ualimu ni kichaka cha waliofeli kwa sababu alikuwa akichangia bajeti ya wizara ya elimu. Ila point aliyoisema hapa ni kweli kabisa hili ni tatizo kubwa la nchi yetu. Hapakuwa na mkakati madhubuti wa kuimarisha elimu. Kumbuka mwaka 1977 ilipopitishwa sera ya Walimu wa UPE hawa ni walimu walioajiriwa na serika ya wakati huo ili kupunguza tatizo la walimu lililolikumba taifa. Walimu wa UPE walikuwa vijana waliomaliza darasa la saba na wanajua kusoma na kuandika. Kumbuka hawakupelekwa hata vyuoni kupata mbinu za ufundishaji kwa wakati huo. Baada ya hapo tumeshuhudia vijana waliokuwa wakienda vyuo vya ualimu kusomea ualimu pindi wakimaliza darasa la saba (GRADE B). walikuwa wakisoma miaka minne, baada ya hapo wanaingia darasani kushika chaki. Pia tumeona pia secondary tulizosoma, walioenda ualimu ni wale walipata div four na baadhi wachache division 3. Form six pia wanaenda vyuo vya ualimu pia ni wale wenye ufaulu wa div 3 na four. Kwa mantiki hiyo mtu anaweza kusema ualimu ni kichaka cha waliofeli.
 
Yes jeshini kama ni infantry na siyo logistics, huitaji div 1. Jeshini walitwambia akili acha mlangoni, huko ni nguvu basi! Labda kama hukwenda jeshini! Nakumbuka afande Chacha alikuwa anasema msituletee form six yenu hapa. Tunataka nguvu!
Cruter.... "unareta Usomi hapa... Msituretee form six yenu hapa". Hahahahaha
 
Hivi ni kwa nini walimu ndio wanaonekana walifeli? Ili uwe qualified kusomea ualimu ngazi ya cheti ni lazima uwe na kuanzia div four ya point 27 kushuka chini, lakin kusomea fani zingine kama uhasibu, sheria na zinginezo kwa ngazi ya cheti wanachukua mpaka div 4 ya 30. Ila wanao onekana kufeli na walimu tu! Kwa diploma ni principal pass moja na subsidiary mbili sawa na fani zingine, ila ukisoma ualimu utaonekana umefeli, kwa shahada ni kitu kile kile minimum qualification zinajulikana ila bado tu walimu wataitwa waliofeli!!!!!! Duh, this is unfair, kosa kubwa la walimu kuzalauliwa na kutukanwa na jamii yao ni sababu ya umaskini wa familia zao, licha ya malipo duni walilazimika kusomea ualimu kwa sababu ndio kazi ambayo ina uhakika na uhalaka wa kupata ajira na mkopo wa maana unapokuwa chuoni! Kama government itaamua kuboresha posho na mishahara ya walimu nina hakika dharau zote hizi juu ya walimu wetu yatima na maskini wanaodhurumia, kutapeliwa, kuteswa na kutukanwa na watawala itakoma na hao wanaojiita "waliofaulu" watatamani na kukimbilia uualimu.Hivi ni kwa nini walimu ndio wanaonekana walifeli? Ili uwe qualified kusomea ualimu ngazi ya cheti ni lazima uwe na kuanzia div four ya point 27 kushuka chini, lakin kusomea fani zingine kama uhasibu, sheria na zinginezo kwa ngazi ya cheti wanachukua mpaka div 4 ya 30. Ila wanao onekana kufeli na walimu tu! Kwa diploma ni principal pass moja na subsidiary mbili sawa na fani zingine, ila ukisoma ualimu utaonekana umefeli, kwa shahada ni kitu kile kile minimum qualification zinajulikana ila bado tu walimu wataitwa waliofeli!!!!!! Duh, this is unfair, kosa kubwa la walimu kuzalauliwa na kutukanwa na jamii yao ni sababu ya umaskini wa familia zao, licha ya malipo duni walilazimika kusomea ualimu kwa sababu ndio kazi ambayo ina uhakika na uhalaka wa kupata ajira na mkopo wa maana unapokuwa chuoni! Kama government itaamua kuboresha posho na mishahara ya walimu nina hakika dharau zote hizi juu ya walimu wetu yatima na maskini wanaodhurumia, kutapeliwa, kuteswa na kutukanwa na watawala itakoma na hao wanaojiita "waliofaulu" watatamani na kukimbilia uualimu.
 
Mkuu Kigodoro Kwa kauli yako mwenyewe kama ulivyopambanua tafasiri ya elimu. Inawezekana hata wewe kutokana na elimu uliyoipata imekupa uwezo mdogo wa kuchambua na kupanua mambo. Hebu tuwe realistic Mkuu kidogo, mie nadhani Bashe amesema Ualimu ni kichaka cha waliofeli kwa sababu alikuwa akichangia bajeti ya wizara ya elimu. Ila point aliyoisema hapa ni kweli kabisa hili ni tatizo kubwa la nchi yetu. Hapakuwa na mkakati madhubuti wa kuimarisha elimu. Kumbuka mwaka 1977 ilipopitishwa sera ya Walimu wa UPE hawa ni walimu walioajiriwa na serika ya wakati huo ili kupunguza tatizo la walimu lililolikumba taifa. Walimu wa UPE walikuwa vijana waliomaliza darasa la saba na wanajua kusoma na kuandika. Kumbuka hawakupelekwa hata vyuoni kupata mbinu za ufundishaji kwa wakati huo. Baada ya hapo tumeshuhudia vijana waliokuwa wakienda vyuo vya ualimu kusomea ualimu pindi wakimaliza darasa la saba (GRADE B). walikuwa wakisoma miaka minne, baada ya hapo wanaingia darasani kushika chaki. Pia tumeona pia secondary tulizosoma, walioenda ualimu ni wale walipata div four na baadhi wachache division 3. Form six pia wanaenda vyuo vya ualimu pia ni wale wenye ufaulu wa div 3 na four. Kwa mantiki hiyo mtu anaweza kusema ualimu ni kichaka cha waliofeli.
Mkuu unataka kutuaminisha kuwa wanafunzi wote wanaomaliza kidato cha sita na kupata div 3 na 4 husomea ualimu?
 
Back
Top Bottom