Mhe. Bashe tengua kauli...

Ualimu IV NS vi lakini ni mwalimu
sehemu nyeti huwezi kulinganisha na sehemu ulizozitaja.Wote uliowataja wanatokana na mwalimu, hivyo mwalimu akiwa mbovu kila kitu kinakuwa kibovu.
Let us face the reality! Kuna mwanafunzi aliyepata division 1 or 2 (nadhani hata three??????) akaenda ualimu?
Sidhani kama unajua unachokiongea. Mimi nilipata dv 2 form iv na form vi lakini ni mwalimu. Isitoshe walimu wengi wa sekondari ni wale wenye div I-III.
 
Kila mtu siku hizi anakosoa walimu hata kama hajui vigezo na majukumu ya mwalimu kwa ufasaha. Wengi wanadhani ile mtoto kufaulu nikujibu maswali kama nwalimu alivyo jibu. Wanajisahaulisha kuwa binadamu anautashi hivyo yampasa kutafakari. Nimeshuhudia vyuoni watu wakifanya discussions katika vikundi lakini ikitokea swali likatoka lenye mlengo unaoelekea kufanana na waliyojadili kuna watakao kosa kabisa kwakuandika kila kitu kama walivyojadiliana na kuna wengine watakao jiongeza nakugundua mlengo wa swali na watalipata. Ufahamu ni jambo ambalo kila mtu anakiwango tofauti na ni nadra sana mtu kufundishwa ufahamu. Ninachokiona kiona nikuwatwisha mzigo walimu usiokuwa wao,jamii isiyotayali kupokea na kujifunza hatimae kubuni njia zake kwakusaidiwa na nyenzo tofauti kama mwalimu, vitabu na mazingira halisi ya nje huyo hafai. Matokeo ya wanafunzi sio kama mgonjwa anae enda kutibiwa na kufanikiwa kwa dactari ni pale nafuu inapopatikana tena ndani ya mda mfupi.
Naamini kama vyuoni wanafunzi mitihani yao ingetungwa na chombo kingine nje ya yule aliyefundisha nakusahihiswa kwa mfumo huohuo,nakwambia pamoja na ukubwa wao,habari hii ya ufaulu vyuoni ingekuwa habari nyingine na uwepo wa ma PhD,na professors. 75% ufaulu unamtegemea mhusika ( mwanafunzi ) mwenyewe.
 
Mhe. Bashe kwanza hongera sana kwa kuingia bungeni baada ya kufanyiwa figisu nyingi 2010 na hatimaye ukaenguliwa eti wewe si mtanzania. Na kwa kipindi kifupi tu jina lako limeanza kuingia vichwani mwa watanzania wachache wanofuatilia bunge manane ya usiku.

Nakuja hapa kukutaka utengue kauli yako iliyonukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba "ualimu ni kichaka cha waliofeli". Binafsi sijakusikia wala kukuona moja kwa moja kwa kuwa hilo bunge lenu linalooneshwa manane ya usiku wala sina habari nalo. Lkn kwa kuwa hujakanusha nukuu hii iliyoenea katika vyombo vyote vya habari bila shaka uliitoa kauli hii.

Kauli hii inawezekana uliitoa kwa dhamira njema kabisa lkn hukufikiria madhara yake kwa ualimu na walimu. Maana inatweza na kudhalilisha ualimu na walimu. Kwa mtu wa hadhi yako unayesifika kuwa mwanasiasa machachari unayechipukia unapaswa kuwa makini kabla ya kufungua kinywa chako.

Jiulize maswali yafuatayo mhe. Bashe.
1. Kufeli maana yake nn?
2. Taasisi nyingine za serikali hakuna waliofeli?

Elimu ni uwezo wa kutambua na kupambana/kukabiliana na changamoto zilizopo ktk mazingira. Anaye elimika anapaswa kuwa huru kifikra na kiuchumi.

Kimsingi elimu ktk taifa letu haimpi msomi ujuzi na uwezo wa kutambua na kupambana na changamoto zinazomzunguka. Tumeshuhudia mkuu wa mkoa aliyekuwa mstari wa mbele kuhimiza vijana wajiajiri akilia njaa baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo.

Yawezekana hata wewe Bashe unajiona mwenye kufaulu kwasabb tu umepata ubunge. Nje ya ubunge huna mbinu ya kupata mlo au kuendesha maisha

Tunaona maprofesa wakililia mikataba ya kuendelea na kazi hata baada ya kufikia umri wa kustaafu. Hii ni ishara tosha kuwa hawana ujuzi na uwezo wa kupambana nje ya ajira.

Lkn kama taasisi nyingine zina waliofaulu. Inakuwaje walimu waliofeli wakaingia kwenye ajira ili hali mifumo ya kuajiri serikalini imeshikwa na walioelimika??
Mhe. Bashe ulikuwa too specific katika kauli yako. Ingekuwa vema ungesema "serikalini ni kichaka cha waliofeli".
-bungeni hakuna waliofeli?
-polisi hakuna waliofeli?
-mahospitalini hakuna waliofeli?
- jeshinini hakuna waliofeli?
- wizarani hakuna waliofeli?
-tra, pccb, ewura, n.k hakuna waliofeli huko?

Nionavyo mm watanzania wote wamefeli. Ndiyo maana hata chama chako kikakuzushia kashfa zisizo na miguu kuwa wewe ni msomali ili tu usiwe mbunge. Waliofaulu wanaweza kufanya hivyo?

Lkn waliofaulu wamefanya nn ktk nchi hii? Mm naona kuna walioenda shule na kupata vyeti tu. Ndiyo maana nchi ina kila kitu halafu umaskini umekithiri. Mpk leo nchi inaagiza vijiti vya kuchokonolea meno!!!? Hao waliofaulu wako wapi?

Majengo, yanaanguka hovyo, miji yetu yote haijapangwa, viwanda vinakufa kuna waliofaulu kweli? Kuna watakao kuja na majibu ya watunga sera na sheria. Hawa pia wamefaulu??

Daah!! Niishie hapa.
Wako Kigodoro.
Nimesoma robo tu ya andiko lako, lakini nikajua kwa haraka haraka unaona dosari ya hoja za Mh Bashe. Kutoka moyoni, BASHE yuko SAHIHI. nampongeza kwa kujipambanua kuwa msema ukweli. Sina hakika chama kama kitamuona ni mbaya au la,lakini hoja zake ziko Kizalendo!
 
Nimesoma robo tu ya andiko lako, lakini nikajua kwa haraka haraka unaona dosari ya hoja za Mh Bashe. Kutoka moyoni, BASHE yuko SAHIHI. nampongeza kwa kujipambanua kuwa msema ukweli. Sina hakika chama kama kitamuona ni mbaya au la,lakini hoja zake ziko Kizalendo!
CCM watamfukuza! Hawataki ukweli
 
Hapana sikufundishwa na hao please. Nimemaliza University 1983! Hapakuwa na upuuzi wa sasa. Afterall University ilikuwa moja usingelithubutu kwenda huko bila sifa
Umesomea ualimu kwa vile labda kwa ajili ya uhaba wa ajira/mikopo- wazazi kutokuwa na uwezo kifedha. Watoto wetu wanakwenda huko na div 1 ya form six (kupata ajira with hope kuwa kwa vile form six pass zangu ni nzuri nitabadilisha mbele, na wengi wamefanya hivyo kama vyeti vyao vya form six ni vizuri) not form 4.
kwa hiyo walimu wenu walikuwa na ufaulu gani mkuu? walikuwa na division one tu?
 
Kwa nini hukwenda form five? Mwaka gani na shule gani? Kama kuna wengine kama wewe wana sababu au wewe una sababu zako unazozijua wewe na ni WACHACHE- NEGLIGIBLE!
mkuu usikariri vibaya. sio kila mwenye division one lazima aende form five. amka.
 
nn Einstein na billgate,?
Usilinganishe hao na Tanzania situation. Einstein alikataliwa kuwa lecturer kwa vile hakuwa na vigezo walivyokuwa wanavihitaji pale-passes, sio kuwa alikuwa na div 4 or zero! Hatujui Billgates background yake kwa nini alifeli! Kuna wanafunzi wana akili lakini hawasomi. Tulikuwa naye alikuwa na akili sana form 4 akafeli zero kabisa. Baba yake alikuwa afisa elimu Mtwara, akarudia form3 akapata div 1 form 4&6. Akasoma medicine Muhimbili with flying colours. Akaenda Zimbabwe etc... He is dead now-RIP.
 
hii tabia ya kila mtu kuujua na kuukosoa uwalimu ni tatizo. kiujumla lengo la bashe lilikuwa jema ila kwenye kuwasilisha hoja yake imejaa ukakasi na imejaa udhalilishaji. kusema walimu ni chaka la watu waliofeli kiujumla sio sawa. je fani zingine huchukua watu wenye sifa zipi? je vipi polis? vipi uganga? hoja ya bashe imedhalilisha walimu kiukweli.
 
Kila secta inawatu wenye ufaulu tofauti,lakini naami kama ulipata certificate ina maana uli pasi. Swala sasa lingebaki ni grade ipi ya ufaulu inafaa kada ipi na kwanini? Je nikosa la nani kama waliruhusiwa kusoma? Je nikwakiwango gani( statistical data) hiyo grade imechangia kwa matokeo hayo?
NB: mwalimu anaefundisha darasa lenye watoto 50, harafu 2 wakaenda shule wanazoziita special, 8 wakaenda za kawaida je hapo mwalimu unamhukuje?
 
Hili swala la ufaulu mbona linatambulika tangu kitambo? Waliopata division one na two O'level huchaguliwa kwenda form five, na waliopata division three kombi zikakubali pia huchaguliwa moja kwa moja na nacte. Wale ambao kombi hazijakubali lakini wana credit tatu yaani "C" tatu husoma shule za private. Siku hizi huenda kufanya mitihani ya mchujo kwa ajili ya kusoma shule za english medium na zingine za private. Hali ipo hivyo hivyo kwa "A" level ingawa huyu anaweza kuchagua kusomea ualimu kwa ngazi ya degree. Sasa huyo mwanafunzi mwenye ufaulu wa division one, two na three mnayemtaka akasomee ualimu atapatikana wapi? Mbona mnataka kuficha ukweli ambao unafahamika tangu kitambo? Ni mfumo wa serikali ambao imejiwekea tangu siku nyingi. Hawa wenye division four ndiyo huenda kusomea ualimu na fani zingine kwa sababu hawakuchaguliwa kuendelea na shule moja kwa moja. Ngoja niishie hapa lakini walimu wengi ni wale wenye ufaulu wa division four ya point 28

Mshua.
 
Ualimu ni sehemu nyeti huwezi kulinganisha na sehemu ulizozitaja.Wote uliowataja wanatokana na mwalimu, hivyo mwalimu akiwa mbovu kila kitu kinakuwa kibovu.
Let us face the reality! Kuna mwanafunzi aliyepata division 1 or 2 (nadhani hata three??????) akaenda ualimu?

Ndugu; ukiwa huna data nivizuri ukakaa kimya! One , two kwa uwalimu zimejaa . Nyie mnaonyooshea walimu vidole kwa nini mlipofaulu na hizo one za 7 na 3 hamkwenda uwalimu Kama mnaupenda sana kuukosoa?
 
Ndugu; ukiwa huna data nivizuri ukakaa kimya! One , two kwa uwalimu zimejaa . Nyie mnaonyooshea walimu vidole kwa nini mlipofaulu na hizo one za 7 na 3 hamkwenda uwalimu Kama mnaupenda sana kuukosoa?
Soma kuna sabau kwa nini mtu wa div 1&2 anakwenda ualimu. Soma watu wametoa sabubu kwenye uzi huu! All in all ni wachache na wana sababu zao.
 
Ni ukweli ni sawa mtu akisema wabunge ni watu waliofeli au mafisadi au wala rushwa akilenga Sijui kubadili mfumo sidhani kama watamuelewa au utakuwa amewatendea haki.! Maana humo kuna watu makini pia kwa hiyo bora uende kwenye hoja kuliko kushambulia watu kwanza.
 
mkuu usikariri vibaya. sio kila mwenye division one lazima aende form five. amka.
Anakwenda wapi? Labda clinical officer very rare kwenye ualimu. Kuna ambao na mimi tunatoka kwenye familia masikini tunataka kusaidia familia, ni wachache!
 
Back
Top Bottom