Mbunge Ndaisaba Ruhoro Aililia Serikali Sakata la Kikokotoo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,004
964

MBUNGE NDAISABA AILILIA SERIKALI SAKATA LA KIKOKOTOO

"Je, Serikali ina mpango gani wa kurekebisha kanuni ya Kikokotoo ili kuongeza kiwango cha mafao ya mkupuo kwa wastaafu? - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara

"Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba inalipa madeni ya Mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuiongezea ukwasi Mifuko hiyo ili iendelee kuwanufaisha wanachama wake?
 
Kikokotoo kiwe hivi:

Watumishi wote wa umma walipwe ⅓ ya jumla ya michango yao yote(yake na ya mwajiri) pindi amalizapo muda wake wa utumishi au kazi itakapokwisha, umri wowote.
  • ⅓ ni pesa yake halali aliyokatwa bila ridhaa yake, ikawekwa kwa muda, ikatumika kuzalisha na faida hagaiwi, hivyo hata kupewa kama ilivyo ni dhuluma; basi apewe tu yote kama alivyokatwa!
  • ⅔ iliyobaki, pia ni haki yake kwa makubaliano na mwajiri wake ingawa ndo hivyo tena! Sasa hiyo ipangieni nyie jinsi mnavyotaka aitumie ila iwe ni lazima kuwe na malipo ya kila mwezi kwa muda usiokoma na endapo atafariki, basi mwenza wake aendelee kupokea ½ ya aliyokuwa anapokea principal!

Watumishi wa sekta binafsi, nao walipwe ½ ya jumla ya mafao yao yote(ya mwajiri na yake) kwakuwa wanachangia sawa, 10% kila mmoja!
- Ilibaki, utaratibu ule ule ufuatwe, kikomo iwe ni kifo cha muajiriwa na mwenza wake.

Angalau basi nijue kuwa halali yangu kabisa haikupokwa!

Mwisho, wote waliokuwa exempted na utaratibu huu, kuanzia raisi mpaka wabunge, hawana HAKI wala mamlaka ya KUWASEMEA wahusika, iwe KOSA kwa mbunge ambaye kimsingi ni MWIZI wa mali za UMMA na mvunjifu wa sheria namba moja kwa kisingizio cha UBUNGE na sheria tofauti, kutaka KUSEMEA kitu kisichomgusa wala KUMHUSU!
 
Back
Top Bottom