MBUNGE INNOCENT KALOGERIS, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Vijijini Akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji kwa Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025 Bungen

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,994
961

MBUNGE INNOCENT KALOGERIS, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Vijijini Akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji kwa Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025 Bungeni Jijini Dodoma.

"Nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kumtua Mama Ndoo kichwani, hii ilikuwa ni ajenda yake alipokuwa Makamu wa Rais na sasa kama Rais ameisimamia kwa dhati. Nampongeza Waziri Aweso na Naibu Waziri, Eng. Kundo na watendaji wote wa Wizara kwa kazi kubwa mnayoifanya Morogoro vijijini" - Mhe. Innocent Edward Kalogeris, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Vijijini

"Nakuomba Mheshimiwa Waziri wa Maji, nilikuja Ofisini kwako kwa suala la mradi wa Kibana Group unaojumuisha Kata Nne (4) na Vijiji 13. Mwaka 2023 tuliweka Shilingi Milioni 200 lakini mradi huu pamoja na VAT unahitaji Shilingi Bilioni 10 lakini mwaka 2024 tumetenga Shilingi Bilioni 1.8, naomba bajeti itakapopita mkatangaze huu mradi wananchi wapate maji safi na salama"

"Mkoa wa Morogoro Jimbo la Morogoro Kusini ndiyo linatoa maji kwa asilimia 76 kwa viwanda Dar es Salaam na Pwani. Mwaka 2023 kuna mradi wa Kilagiu Tower kuna fedha ilitengwa lakini haikupatikana. Kuna mradi wa Mvua Bara, kuna mradi wa Lumbi. Waziri ulitoa ahadi ya fedha ili maji yafike kwenye Kijiji cha Milango Miwili. Nikuombe Waziri wa Maji angalia namna moja ama nyingine ili miradi ikamilike"

"Nakupongeza Waziri wa Maji kwa visima vitano vya maji tulivyopata ambapo tutakwenda kuchimba Ukurunge, Vije, Kibangire, Viengero na Tuo ambavyo vitaenda kuondoa kero kwa wananchi wetu. Sisi watu wa Morogoro vijijini kuendelea kupata Maji ya visima siyo sawa, sisi kama wahifadhi wa maji tunahitaji tupate mradi wa Maji ya mserereko"

"Ujenzi wa Bwawa la Kidunda umefikia asilimia 17.5, Mheshimiwa Waziri naomba utamke kuhusu huu mradi maana ndani ya mpangilio wako haionekani. Bado kuna changamoto kwa DAWASA katika kulipa makaburi. Mwaka 2023 tuliambiwa kuna shilingi bilioni 1.8 lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika, naomba wananchi wafidiwe makaburi yao ili mradi uendelee"

"Wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu anatoa taarifa ya Mafuriko nilizungumzia nini mpango wa Serikali katika kuvuna maji yanayotokana na mafuriko hasa Mkoa wa Morogoro ambao kila mwaka kuna mafuriko. Tuna mito mitano ambayo inakwenda kutengeneza Bwawa la Kidunda, kama tukiweza kutengenezea Mabwawa kwa juu tutaweza kuondoa matatizo makuu ya mafuriko makubwa kwa wananchi wetu"

"Natamani Wizara ya Maji watueleze kwa Mkoa wa Morogoro wana mpango gani wa kuchimba Mabwawa ambayo yatapunguza mafuriko, yatahifadhi maji kwa Mifugo na kwa matumizi ya binadamu" - Mhe. Innocent Edward Kalogeris, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Vijijini
 

Attachments

  • EzEF7PMWUAAjgrL.jpg
    EzEF7PMWUAAjgrL.jpg
    64.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom