Marufuku ya nishati asilia (Fossil fuels), dizeli, gesi, mafuta ya taa petroli na nyinginezo ipo njiani

HUNIJUI SIKUJUI

JF-Expert Member
Apr 4, 2015
1,335
1,547
Dunia inabadilika na sisi tunapaswa kubadilika, nishati asilia zinaongoza kwa kutoa gesi chafu zinazosababisha engezeko la joto duniani! Kama mpaka muda huu hujawahi kumiliki chombo chochote kile cha usafiri kinachotumia nishati asilia inawezekana usimiliki kabisa ndani ya miaka michache ijayo

Tanzania tuna gesi nyingi sana huko Mtwara ambapo nimeona MH. January Makamba ameingia mkataba na kampuni za Uarabuni kwa ajili ya kuchimba gesi hiyo yenye thamani ya TZ trilioni 70 ( =GDP ya nchi ) tupo katika 'now or never' situation maana tukishindwa kuichimba ndani ya miaka 10 ijayo inawezekana tusiichimbe tena maana tutakua tumepitwa na wakati na mzigo wote utachacha

Tayari makampuni ya magari kama vile Ford, General Motors, Mercedes na Mercedes-benz wamesema watayaondoa magari mengi ya dizeli na petroli katika masoko yao makuu ifikapo mwaka 2030 ila Toyota wamesema 2030 ni karibu sana kwao ila mpaka 2040 watakua wamefikia lengo hilo ( Cop26: carmakers agree to end sale of fossil fuel vehicles by 2040 ) kwa hiyo wale ndugu wenye long term plans au ndoto za kujenga sheli za mafuta wanatakiwa kuwa na tahadhari au wapenda magari kwa ujumla

Tunashuhudia mabadiliko katika nishati, hali ya hewa na utamaduni wa maisha ya binadamu kwa ujumla
 
Hata marcedes hayo makubaliano bado hajamwaga wino.

Shida hawa watu wanajali faida tu. Charger ya kucharge gari la tesla haiwezi charge gari la ford.

Pia system siku hizi ni kama ilivyo kwenye bidhaa za apple. Tesla gari ikiharibika mpaka ulipeleke kwa dealers wao ambapo ni expensive sana. Spare kupata mpaka kwa dealers wao. Kuna jamaa kadhaa naona ndo wanahack mfumo wa magari yao ili waweze kuwa wanafanya repair.

Sasa mambo kama hayo huku kwetu inakuwa shida.
 
... sasa sisi wa kusuburia hadi zichakae Ulaya au Japan ndio na sie tumiliki mikweche itakuwaje? Mingi tunayoagiza leo 2021 ni make za 2005 backwards. Kazi ipo.
 
Hata marcedes hayo makubaliano bado hajamwaga wino.
Shida hawa watu wanajali faida tu. Chatger ya kucharge gari la tesla haiwezi charge gari la ford.
Pia system siku hizi ni kama ilivyo kwenye bidhaa za apple. Tesla gari ikiharibika mpaka ulipelekr kwa dealers wao ambapo ni expensive sana. Spare kupata mpaka kwa dealers wao. Kuna jamaa kadhaa naona ndo wanahack mfumo wa magari yao ili waweze kuwa wanaganya repair.

ni kweli mkuu chaja za magari zinapaswa kua universal , makampuni yanayotengeneza betri yanatakiwa kutumia teknolojia moja nafkiri hili nalo litakuja ili kuzuia kila kampuni kua na chaji zake tu ambazo haziingiliani na kampuni nyingine?
 
... sasa sisi wa kusuburia hadi zichakae Ulaya au Japan ndio na sie tumiliki mikweche itakuwaje? Mingi tunayoagiza leo 2021 ni make za 2005 backwards. Kazi ipo.
sio kidogo, Africa tutakua dampo ya magari ya dizeli na petroli lakini maisha yenyewe yatatafuta njia tusihofu sana
 
Umenikumbusha story za enzi hizo ati wakati Tanzania imepaa kwenye sisal production, wazungu wakaanzisha kamba za nailon, tukabaki na mkonge wetu hadi leo. kabal ya hapo mkonge ulikuwa na soko hadi nyerere alitaka aanze kuuza kwa kiburi.
 
sasa hii gesi yetu inakuja kua chakula kilicho lala na kika chacha
kwa namna maendeleo ya dunia yanavyoenda kasi, si ukute mkaja kuiuza kwa hasara tu. wakati mwingine namkubali maza, kuwa maliasili zilizopo tuzichimbe haraka tutumie kuendeleza nchi kuliko kujifanya tuzihifadhi tuzitumie badaye wakati hatuna kitu mkononi cha kuendelezea nchi sasahivi. nakumbuka bimkubwa hadi alitaka tuanze kuchimba madini kwenye mbuga....kuliko kuyaacha chini. dunia yenyewe hii karibia inaisha, ni sawa na mfanyabiashara anayekopa mkopo apate mtaji aendeleze biashara, biashara yake inaenda vizuri kweli, halafu wewe kajambanani ati unaogopa mkopo unasubiri hadi siku Mungu akikujalia ukipata mkopo (from no where you even know) ndio uendeleze biashara. utaaachwa umesimama wenzio wanaendelea. wachakate tu hiyo gesi na madini yote, yaani popote penye resources chakata haraka tutumie hela hiyo kujenga nchi. tunasubiri nini?nyerere amesubirisha yawe chini kuna faida gani? kwani hadi leo hatuna akili bado.
 
Wanayowaza wa Ulaya sisi ittuchukua miaka 100 kama wao ni 20

Hatuna uwezo wa kuwa na magari ya umeme kwani ukichambua gharama za kuiendesha na service zote ni bora mafuta

Wao wenyewe wanaulizana kutwa je itakuwaje ?

Nchi nyingi ukiwa na 0 emission car hata road tax hulipi na pia sehemu za low emission zone unapeta tu ili kuwahimiza watu wanunue magari hayo

Kuhusu has na hata mafuta bado yatahitajika kwa miaka mingi tu kwani kuna viwanda na sio magari tu

Labda uko sahihi pia
 
Inaonekana una uwelewa mdogo!

Umefuatilia huo Umeme unaozishwa duniani ni asilimia ngapi unazalishwa kwa kutumia fossil fuels.

Kwa taarifa yako bado umeme unaozalishwa kwa njia nje ya burning fossil ni asilimia chache Sana hata 25% haifiki duniani!
Hii nchi wajinga ni wengi Sana!
Kila kitu unakisiasisha tu!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Tsh Tilioni 70 ndani ya hiyo miaka 20 itakuwa imepatikana?
Au ndio tumechelewa !!
ila hiyo hela ni ndogo sana aisee, wakati kwa mwaka mmoja tu tunaingiza zaidi ya trilion 10 kwa mapato tu ya ndani. yaani gesi yetu yoote ndio bei hiyo? si tuanze kutafuta maisha mengine tu hapo hakuna cha kutegemea sana. tusijekujiona tushakuwa matajiri, plus wapigaji/mafisadi hawajachukua chao hapo.
 
Dunia inabadilika na sisi tunapaswa kubadilika, nishati asilia zinaongoza kwa kutoa gesi chafu zinazosababisha engezeko la joto duniani! Kama mpaka muda huu hujawahi kumiliki chombo chochote kile cha usafiri kinachotumia nishati asilia inawezekana usimiliki kabisa ndani ya miaka michache ijayo

Tanzania tuna gesi nyingi sana huko Mtwara ambapo nimeona MH. January Makamba ameingia mkataba na kampuni za Uarabuni kwa ajili ya kuchimba gesi hiyo yenye thamani ya TZ trilioni 70 ( =GDP ya nchi ) tupo katika 'now or never' situation maana tukishindwa kuichimba ndani ya miaka 10 ijayo inawezekana tusiichimbe tena maana tutakua tumepitwa na wakati na mzigo wote utachacha

Tayari makampuni ya magari kama vile Ford, General Motors, Mercedes na Mercedes-benz wamesema watayaondoa magari mengi ya dizeli na petroli katika masoko yao makuu ifikapo mwaka 2030 ila Toyota wamesema 2030 ni karibu sana kwao ila mpaka 2040 watakua wamefikia lengo hilo ( Cop26: carmakers agree to end sale of fossil fuel vehicles by 2040 ) kwa hiyo wale ndugu wenye long term plans au ndoto za kujenga sheli za mafuta wanatakiwa kuwa na tahadhari au wapenda magari kwa ujumla

Tunashuhudia mabadiliko katika nishati, hali ya hewa na utamaduni wa maisha ya binadamu kwa ujumla
Tutapitwaje na wakati ukizingatia hiyo gesi itatumika kuzalisha umeme?, au gesi ni kwa ajili ya magari tu?
 
Hata marcedes hayo makubaliano bado hajamwaga wino.
Shida hawa watu wanajali faida tu. Chatger ya kucharge gari la tesla haiwezi charge gari la ford.
Pia system siku hizi ni kama ilivyo kwenye bidhaa za apple. Tesla gari ikiharibika mpaka ulipelekr kwa dealers wao ambapo ni expensive sana. Spare kupata mpaka kwa dealers wao. Kuna jamaa kadhaa naona ndo wanahack mfumo wa magari yao ili waweze kuwa wanaganya repair.
Sasa mambo kama hayo huku kwetu inakuwa shida.
Kwani hii gesi si itatumika kuzalisha umeme wa kuendesha hayo magari au? Huyu jamaa kachanganyikiwa?
 
gesi ikishachakatwa tu haiwezi kukosa soko. hata hapa tanzania tu kwa matumizi ya ndani, kenya matumizi ya ndani, rwanda, burundi na zambia, soko linatosha hata bila kupeleka ulaya au asia. kwa Tanzania sasahivi watu wengi wameshasahau kupika bila gesi.

tenchnolojia inaenda kasi sana. mwaka 2007 nilipoenda america kwa mara ya kwanza, nilizikuta hizi flat screen ambazo ninyi ndio zimefika huku siku hizi. tulikuwa tunaunua movie online kama tunavyoweza kufanya hapa sasahivi kwa hizi tv smart. kuna maendeleo mengi tu kabla hayajafika huku kwetu huko nje huwa yanakuwa yametumika karibu miaka 10 ndio yanatufukia. si ukute kuna alternative ya gas imeshaanza kutumika huko nje kwenye vitu ambavyo gas yetu ingetumia, miaka 10 ijayo tunakuja kukosa pa kuuza. uza tu.
 
kwa namna maendeleo ya dunia yanavyoenda kasi, si ukute mkaja kuiuza kwa hasara tu. wakati mwingine namkubali maza, kuwa maliasili zilizopo tuzichimbe haraka tutumie kuendeleza nchi kuliko kujifanya tuzihifadhi tuzitumie badaye wakati hatuna kitu mkononi cha kuendelezea nchi sasahivi. nakumbuka bimkubwa hadi alitaka tuanze kuchimba madini kwenye mbuga....kuliko kuyaacha chini. dunia yenyewe hii karibia inaisha, ni sawa na mfanyabiashara anayekopa mkopo apate mtaji aendeleze biashara, biashara yake inaenda vizuri kweli, halafu wewe kajambanani ati unaogopa mkopo unasubiri hadi siku Mungu akikujalia ukipata mkopo (from no where you even know) ndio uendeleze biashara. utaaachwa umesimama wenzio wanaendelea. wachakate tu hiyo gesi na madini yote, yaani popote penye resources chakata haraka tutumie hela hiyo kujenga nchi. tunasubiri nini?nyerere amesubirisha yawe chini kuna faida gani? kwani hadi leo hatuna akili bado.
Uiuze kwa hasara kwani si inazalisha umeme? Au baadae umeme hautahitajika? Nyie mmevuta bangi ya nchi gani?
 
umeambiwa kinachoweza kuzalisha umeme au kinachoweza kugundulika kuweza kuzalisha umeme hapo baadaye itakuwa ni gas tu? hata nyerere alikuwa haamini kama kuna siku zitaibuka kamba za nailon, akabaki na katani zake haadi leo.
 
Back
Top Bottom