Nchi yetu imeanza kuwa na matumaini ya safari ya maisha bora kwa kila mtanzania, tunaomba M/Mungu ampe maisha marefu Mama yetu SASHA,aongoze vyema hii nchi yetu. Bado tuna safari ndefu lakini inshanllah twaweza tukafika. M/Mungu ni mjuzi wa kila jambo, ndiyo maana huwenda yule jamaa aliteuliwa kwenda kuwatawala Malaika.Kweli Mungu fundi hasa.
 
Tushachoka kukuona kwenye magazeti na Tv,ukishamaliza teuzi ,fanya hima upitia na huku mikoani yote kwa sasa ni mitaa yako, ufike tujuane tusalimiane ujue shida zetu tujue zako ,maisha yaendelee.
kero zetu kwako ni zingi sana ,angalau utapata kufunguka macho na akili ukija kutujuvya hali zetu.
 
Kuna watumishi waadilifu waliofanya kazi kwa mafanikio makubwa katika miradi mikubwa ya Serikali ambayo ilitekelezwa na kumaliza muda wake. Baada ya miradi hii kuwa imekamilika watumishi hawa nao ukawa ndio mwisho wa ajira zao kwa mujibu wa mikataba yao.

Ninamwomba Mh. Mama Samia awatupie jicho na kuwafikiria kwa sababu

1. Asilimia 99 yao bado hawajafikia umri wa kustaafu;
2. Ni watu wenye elimu kubwa, uzoefu mkubwa wa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo ya serikali;
3. Ni resource iliyolala ambayo bado inaweza kutumika kuendesha miradi mikubwa ya maendeleo ya kijamii kwa mafanikio makubwa.
4. Wanaweza kutoa ushauri mzuri katika utekelezaji wa miradi inayolenga kuleta mabadiliko katika maisha ya watanzania wa vijijini.
5. Kutokana na uzoefu wao ni rahisi kuishauri serikali katika kubuni miradi yenye tija kwa wananchi.

Rais naomba utafute namna ya kuwatumia watu hawa wenye elimu kubwa, uzoefu mkubwa na uazlendo mkubwa katika shughuli na maendeleo ya ncchi yetu.

Miradi mikubwa iliyomaliza muda wake na kuacha idadi kubwa ya wataalam bila kazi mitaani ni, DASIP, AMSDP, RFSP, MIVARF...... Mingi ya miradi hii ilikuwa na mafanikio makubwa kwa wanajamii na ilitekelezwa kwa mafanikio na watanzania ambao wana elimu kubwa na uzoefu ila wengi wao wapo mtaani na ujuzi wao.

Hawa ikiwezekana wawe na forum ya kuisaidia serikali kwa namna inavyoona katika utekelezaji na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ya kijamii.
 
Bado mnataka one man show🙉🙉! Urais ni taasisi ndo maana kuna wakuu wa mikoa, RAS, DC, DAS, DED etc wote wapo kutatua kero zote!

Kama hawawasikilizi semeni watumbuliwe wachaguliwe wengine wanaoweza kumuwakilisha vyema Rais!

Uongozi ni Team Work! Ukimuona kiongozi ambaye yeye ndo kila kitu huyo siyo kiongozi! Kiongozi anatengene Teamwork ambayo hata kama hayupo bado mambo yanaenda kama yanavyotakiwa kuwa!
 
Akae huko huko Dar
 
Tushachoka kukuona kwenye magazeti na Tv,ukishamaliza teuzi ,fanya hima upitia na huku mikoani yote kwa sasa ni mitaa yako, ufike tujuane tusalimiane ujue shida zetu tujue zako ,maisha yaendelee.
kero zetu kwako ni zingi sana ,angalau utapata kufunguka macho na akili ukija kutujuvya hali zetu.
Kama CCM wana serikali yote na wabunge wote ni CCM na bado mnasema mko na kero nyingi sana basi tuko na UJINGA fulani, maana waliokuwa wanatukwamisha na kutuchelewesha ni Wapinzani.....
 
Tupatie taarifa kamili

IMG_20210511_083147_099.jpg
 
Niwasalimu kwa Jina la JAMHURI.

Naomba nianze mapema pasipo kupoteza muda,

Tatizo la Umeme linaanza kushika hatamu taratibu kabisa Rais Mtukufu yupo kimya watendaji husika wapo kimya nikimaanisha waziri pamoj na wizara nzima pia mkurugenzi wa shirika la Tanesco.

Saivi kukata umeme weekend imeanza kurudi ka zamani kukatika siku za kawaida nayo imerudi.

Mama samia kua makini hii kero tulianza kuisahau vile lakini naona kama inarudi hivi usipoangalia hili litakua shirika namba moja kukutia dosari naamini we ni msikivu sana nahisi ushaliona tunaomba ulifanyie ufumbuzi mapema watanzania tuendelee kujenga uchumi wetu wa kati.

FINITO
TANESCO kumeoza mkuu huduma ni mbovu vibaya sn poor customer care
 
Back
Top Bottom