Mama Magufuli aaga rasmi shule ya Mbuyuni

Nimshauri tu kama yumo humu akalifanyie kazi. Aanzishe NGO kama za watangulizi wake ya kuwajengea walimu nyumba karibu na mashule ili kuwapunguzia adha za wenye nyumba. Hili litamtofautisha na wale wenye WAMA na fursa sawa kwa wote kwani ataishi kwenye mioyo ya watanzania milele. Na hili linawezeka likiratibiwa na kusimamiwa vema. Anipm kwa msisitizo.
Hili wazo ni nzurii.. kwa kuwa washauri wake wanapita hukuuu naomba wamfikishieeee...
Yeye ajikite kusaidia walimu...
 
Wakumbuke Mama na wasikilize...maana unaweza kuwakumbuka ila usiwasikilize.Mwanzo mzuri,hatimaye walimu wataona nuru maana wapo kwenye giza tena totoro.
Mama na Imani naye naona ana moyo/utu wa kibinadamu na Upendo pia.
 
Aliepita nae alikuwa Mwalimu ila waalimu hadi leo wanalia na njaa, bora hata angesema angewatengenezea ile ofisi yao
 
Ni kweli aliyepita alikua mwalimu jk hakuna mwalimu lkn tofauti ni moja tu huyu wa sasa ni mwalimu na mzee nae ni mwalimu.
Aliepita nae alikuwa Mwalimu ila waalimu hadi leo wanalia na njaa, bora hata angesema angewatengenezea ile ofisi yao
 
12717629_1042473825817075_8844224208873748454_n.jpg
 
Mke wa Rais Magufuli ameyasema hayo maneno leo alipokua anawaanga wanafunzi wake na wafanyakazi wenzake (walimu). Ikumbukwe bi Janet kitaaluma ni mwalimu,na ameifanya hiyo kazi zaidi ya miaka kumi, aidha mama huyo amesisitiza kumkumbusha mume wake kutatua changamoto za walimu.
Mmewe mwenye alikuwa mwalimu kwaiyo kama walimu hawataweza hata awamu hii wajue hali zao haziwezekani kubadilishika
 
Pale ikulu sijui pana kaugonjwa gani! Mtu akiingia pale huwa anajisahau kabisa! Ndio maana hatukushangaa kiongozi mkubwa tu anaulizwa swali jepesi kwa nini wananchi wake ni maskini eti anajibu hata yeye hajui!!

Kwa huyu rais wa sasa tutaendelea kumpa muda kwa kuwa hajaanza vibaya. Tunamuombea asibadilike kama yule mwenzake aliyepita.
 
Kuna jamaaa haajuagi shughuli za kinamama au kujali mwaliko hata kitchen part anang'ang'ania kuingia...Mr.Misifa au Zero thinker au Mdogo nepi
 
Back
Top Bottom