Makonda Alienda Clouds Kufuatilia Documentary Yake ya Mwaka Mmoja Madarakani

Status
Not open for further replies.
Hiyo Documentary ilikuwa irushwa na SHILAWADU?
Ndio ushangae hapo

Yani bora unyimwe kila kitu hapa duniani lakini upewe akili

Ukilaza ni mbaya sana,yani MTU unajichoresha bila kujijua unajichoresha
 
Kuna uwongo mwingine unaogopa kumwambia hata mwanao wa chekechea nyumbani kweli. Kwani clouds huwa hawana muda maalum wa kazi wa kupokea wageni?
 
Bashite rafiki yangu umeshindwa ata kutafuta walioenda shule kidogo wakusaidie kukutea uku mtandaoni rafik yangu?
 
Licha ya watu wengi kuzungumza mengi kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam 'kuvamia' ofisi za Clouds Media kwa lengo la kuwatisha vijana wachapakazi wanaopendwa mpaka na viongozi wa juu serikalini, Shilawadu (Qwisa na Soud Brown), inaelezwa kwamba mkuu huyo wa mkoa, hakwenda kwa shari.
Inaelezwa kwamba alikwenda kufuatilia utaratibu wa documentary yake ya mwaka mmoja madarakani, iliyofanyika pale Officers Mess, Oysterbay kwa sababu anataka irushwe kwenye kituo hicho, ili watu wengi zaidi waone matunda ya jitihada zake za kupambana na madawa ya kulevya na namna anavyoungwa mkono na waathirika wenyewe.
Clip inayosambaa, haioneshi popote kwamba mheshimiwa alitumia nguvu kuingia, na zaidi kuna mtu anaonekana mapokezi ambaye ndiye aliyekuwa akiwafungulia mlango wa ndani. Hakuna mtangazaji yeyote aliyepigwa na kulikuwa na mazungumzo ya kawaida tu ambayo hata hiyo, haifahamiki yaliishaje.
News Spinning...
Ilikuwaje aingie na wanajeshi wenye silaa watano ndani ya chumba cha habari. Kwani hiyo video yake ilikuwa studio
1. kwanini asiulizie mapokezi??
2. Kwanini afuatilie video usiku wa saa nne??
3. Kwanini askari alivaa Magwanda anatoa saini ya Open Mlangoni na kugeuza yaani kuweka ya closed??

Msitufanye watanzania ni wapumbavu yaani wewe Bashite na Magufuli wako ndio ........
 
Licha ya watu wengi kuzungumza mengi kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam 'kuvamia' ofisi za Clouds Media kwa lengo la kuwatisha vijana wachapakazi wanaopendwa mpaka na viongozi wa juu serikalini, Shilawadu (Qwisa na Soud Brown), inaelezwa kwamba mkuu huyo wa mkoa, hakwenda kwa shari.
Inaelezwa kwamba alikwenda kufuatilia utaratibu wa documentary yake ya mwaka mmoja madarakani, iliyofanyika pale Officers Mess, Oysterbay kwa sababu anataka irushwe kwenye kituo hicho, ili watu wengi zaidi waone matunda ya jitihada zake za kupambana na madawa ya kulevya na namna anavyoungwa mkono na waathirika wenyewe.
Clip inayosambaa, haioneshi popote kwamba mheshimiwa alitumia nguvu kuingia, na zaidi kuna mtu anaonekana mapokezi ambaye ndiye aliyekuwa akiwafungulia mlango wa ndani. Hakuna mtangazaji yeyote aliyepigwa na kulikuwa na mazungumzo ya kawaida tu ambayo hata hiyo, haifahamiki yaliishaje.
News Spinning...
Documentary ndo awe Armed kias hicho, Uliepost acha kushika masikio watu wazima ww, shida vijana wa lumumba hamnaga point kabisa, poleni
 
RUGE MUTAHABA ANASHIKILIWA NA POLISI.

Vyanzo vya uhakika vinaeleza kwamba asubuhi ya leo kulikuwa na kikao cha wafanyakazi wa Clouds. Kikao hicho kiliitishwa na Mkurugenziwao wa Vipindi na Uzalishaji bwana RugeMutahaba ambaye aliwaeleza wafanyakazi wote juu ya kituo chao kuvamiwa siku ya Ijumaa.

Baada ya hilo na mengine yanayohusu tukio hilo, Ruge alitakiwa kuripoti katika kituo cha Polisi cha Oysterbay. Mpaka sasa Ruge anashikiliwa Polisi hao.

Hofu kubwa imetanda kwa wafanyakazi wa Clouds na sasa mabosi waowanaonekana kuwamashakani baada ya kuvuja kwa video ya CCTV inayomuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akivamia ofisi hizo za Clouds.

======
UPDATES:

Ruge sasa inadaiwa amehamishiwa Central Police kwa mahojiano zaidi.
 
Fa Fa Fa fa....bunduki nzito vile ni documentary ya mwaka mmoja?? Kwa lipi?? JPM si angeenda na vifaru sasaa?????
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom