Mafanikio makubwa yaliyochochewa na serikali ya awamu ya sita yawa kero kwa wapinzani wa maendeleo nchini

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
15,509
17,597
Ni dhahiri sasa, Dr.Samia Suluhu Hassan anapendwa nchi nzima. kazi za mikono yake na mipango mikakati yake kupitia serikali sikivu ya CCM zawafurahisha sana na kuwanufaisha wananchi nchini kote Tanzania..

Wananchi hivi sasa maeneo mengi nchini wana pata huduma nyingi muhimu kwa uhakika na kujitosheleza vyema,

Mathalani huduma za maji, umeme, kilimo, afya, usafirishaji, elimu, miundombinu, ufugaji, uvuvi, biashara na masoko, ulinzi, usalama, umoja, amani na utulivu ni vya uhakika nchini..

Sasa, kutokana na hayo masuala machache kati ya mengi ya maendeleo, ambayo yote ni kwa manufaa ya wananchi wote waTanzania, eti kuna watu mahali, hawapendi kabisa kuona wananchi wakifurahia huduma hizo.....

alaa sasa ndugu wapinzani wa maendeleo mnataka wananchi wasifurahie maendeleo?

sasa mnachukia kabisa na kujawa hasira hivyo, hamtaki kabisa kuskia wananchi wakimshukuru Rais Dr.Samia Suluhu Hassan kwa kwa kazi kubwa na jitihada zake madhubuti na makusudi za maendeleo, mnataka nini sasa?

Eti hata wananchi wakimsifia Rais kwa ile kazi kubwa na nzuri sana ya maendeleo ailyoifanya kwa manufaa ya wananchi wote eti wapinzani wa maendeleo wanakasirika ...ebooh

Sasa shida hasa ni nini kwa mfano? Kiongozi wa nchi amefanya kazi nzuri, wananchi wamemkubali, wamefurahia kazi yake, wananufaika nayo na sasa wanamuamini zaidi, wanampongeza, wanamsifia sana na wanapenda aendelee na hii kazi nzuri sana aliyoianza katika awamu ijayo..

Kwani, hapo kuna shida gani hasa ndrugu zangu? kwana mnataka nini sasa kama sio maendeleo?

Mungu Ibariki Tanzania
 
Duh acha ninyamaze.
nikikumbuka jirani yangu alimaliza chuo toka 2015 yuko mtaani, nashindwa nilie ama nicheke.
 
Duh acha ninyamaze.
nikikumbuka jirani yangu alimaliza chuo toka 2015 yuko mtaani, nashindwa nilie ama nicheke.
biashara, ufugaji au kilimo ni ajira ya wazi sana, ni kujipanga tu my friend 🐒
 
biashara, ufugaji au kilimo ni ajira ya wazi sana, ni kujipanga tu my friend 🐒
anza kuamiambia serikali ijipange kwanza kuweka mazingira safi na salama ya uwekezaji kwa wananchi wake. Kuanzia Ngorongoro mpaka iseresere..
 
Screenshot_20240825_192226.jpg

Hii ni taarifa ya Mwezi huu,. Muwe mnawadanganya wajinga wenzenu kwenye vijiwe. ya kahawa, kule ndio kumejaaa wajinga wenu wale
 
Back
Top Bottom