Madai ya Kenya kuhusu Olduvai Gorge iko Kenya

View attachment 326295
Hiyo ni ndege ya kenya ina maandishi ya Mount Kilimanjaro, wanatumia majina ya vivutio vyetu kujitangaza duniani huku waziri wa maliasili na utalii yupo tu amekaa kimya akila pesa za umma na kuendeshwa kwenye shangingi za kifahari. Inasikitisha sana, maana watu wamepiga kelele sana ila serikali haichukui hatua yoyote. Kama waziri wa maliasili na utalii ataendelea kukaa kimya kutowachukulia hatua wakenya nitaamini ana maslahi binafsi na kenya.

wa tz wapumbavu kweli, wenzenu wanakaa chini ku plan strategies za kuinua utari nyie mmejifungia maofisini.

ki mantiki hawana kosa hawa wakenya maana wanataka mugawana masilahi, mtarii anakuja kenya anaachfungu halafu anakuja tanzania anaacha fungu, wakati wa kurudi anaenda kenya anaacha fungu theen anasepa.

nyie pigeni domo kudai ni chenu wenzenu wanaumiza kichwa.

hakuna pesa inayokuja kirahisi-nyie siasa za ccm na chadema tu
 
Sioni ubaya as long wote ni wana east africa,nyinyi mlishindwa nini kuutangaza siku zote?na bado huo ni mwanzo tu
 
Na Wakenya nako wanazidi! wanafanya makusudi au hawaelewi ramani? inawezekana huyo mtu kaenda ziara "Masai Mara"(kenya) akavuka mpaka hadi Serengeti(TZ) akashukia Ngorongoro(olduvai george-TZ) akaona hajamaliza masai Mara
 
Haisadii kitu kusema hivyo. Sasa kama sisi (Tanzania) yenyewe imekaa kimya haijitangazi ngoja wakenya wajitangaze kupitia Mali zetu . Leo hii ukisema tanzanite inatokea Tanzania dunia nzima itashangaa na kustaajabu maana wanajua wakenya ndo wameishikilia.

Shida yetu hatukubali vitu vyetu sisi kazi yetu majungu na maslai binafsi ndiyo yanaiacha nchi yetu isitambulike wala kuwa maarufu duniani. Leo hii kila mahali duniani Kenya inatambulika kupitia utalii, michezo nk.... Tanzania hata kidogo haijulikani. Shirika la ndege ni sawa limekufa tuu, utalii hautangazwi, majangili wanafanya yao wanyama wanauwawa , mazingira yanaharibiwa

sisi tumewekeza kwenye siasa za kushindana na kuchagua vyama. eti kwasababu Mimi nipo chama A, chochote kitakachosemwa na chama B hatakama ni kizuri Mimi sitaunga mkono hoja huko bungeni. Wananchi nao tumekuwa wafuasi wa vyama na sio Sera za vyama. kwakuwa tumewekeza kwenye siasa, ubinafsi na maono ya kurudi nyuma haya ndiyo matokeo yake,

Ilipaswa Tanzania iongoze kuingiza pato kubwa kupitia utalii kwasababu kuna vivutio adimu duniani pia nchi inautulivu na usalama wa hali ya juu.

Hapo kwenye shirika la ndege ndio nasikia kichefuchefu. Wamefanya fastjet kuwa Air Tanzania huu ni upungua uliopitiliza ndio maana nawaangalia na mbwembwe zao za kufufua hili shirika naona wanajichungulia wenyewe alafu wanashangaa
 
View attachment 326295
Hiyo ni ndege ya kenya ina maandishi ya Mount Kilimanjaro, wanatumia majina ya vivutio vyetu kujitangaza duniani huku waziri wa maliasili na utalii yupo tu amekaa kimya akila pesa za umma na kuendeshwa kwenye shangingi za kifahari. Inasikitisha sana, maana watu wamepiga kelele sana ila serikali haichukui hatua yoyote. Kama waziri wa maliasili na utalii ataendelea kukaa kimya kutowachukulia hatua wakenya nitaamini ana maslahi binafsi na kenya.

Hio itakuwa tu naming ya ndege kuendana na vivutio vya route za KQ (ambazo nyingi ni hapa hapa Africa) na sio Tanzania pekee. Kwa mfano kuna ndege ina maandishi Victoria Falls;Zimbabwe, Maasai Mara/Longonot/MtKenya;Kenya, Ruwenzori;Uganda, Zuma Rock;Nigeria, Great Rift Valley.... etc.
 
kwaupande wangu sioni kosa na Wakenya,
Siku zote wajinga ndio waliwao,kama taifa likiwa la kijinga,waache wajanja wafaidi kupitia ujinga wa taifa usika.
kama tanzania ni mzalishaji mkubwa wa TANZANITE lakini INDIA na KENYA wanaongoza kwa uuzaji wa tanzanite duniani,kwann wakenya wasijivune?,kwann wasivitumie vivutio vya tanzania kujitangaza?
Kwa upande wango naona wako sahih 100%
ni maoni na mtazamo wangu ivyo msinielewe kivingine
Mkuu India na kenya wanapata wapi Tanzanite wakati tunaambiwa inapatikana Tanzania tu?
 
Hio itakuwa tu naming ya ndege kuendana na vivutio vya route za KQ (ambazo nyingi ni hapa hapa Africa) na sio Tanzania pekee. Kwa mfano kuna ndege ina maandishi Victoria Falls;Zimbabwe, Maasai Mara/Longonot/MtKenya;Kenya, Ruwenzori;Uganda, Zuma Rock;Nigeria, Great Rift Valley.... etc.
Hiyo ndege route zake hazifiki Tanzania.
 
Jamani naomba kuuliza,hivi hili sijui kongamano aliloongea huyu Miss Odinga la IYLA lina tofauti na YILA ile ambayo vijana wa Kitanzania hupelekwa USA na kukaa kambi??ambayo kwa sasa Obama kaibadili na kuiita NELSON MANDELA??
 
Hapo sasa wamevuka mipaka Kilimanjaro walijimilikisha sasa wanaingia ndani kabisa mwisho watasema ngorongoro ni yakwao.

Nakumbuka awamu iliyopita tulitoa tamko la kupunguza safari za ndege zao kuingia Tanzania wao wakafunga mipaka watalii wasije Tanzania.

Baadala nasisi kuonyesha ujasiri wetu tukawachekea siku yapili naona maraisi wanashikana mikono ni udhaifu mkubwa sana tumeuonyesha ndio maana hata leo wanasema watakacho kwasababu wanajua hatuwaambii kitu.

Tungewafungia alafu sisi tungefungulia kiwanja chetu chakilimanjaro ndege zitue nyingi alafu tungeona jeuri yao na vimbuga vyao.
Tena usisahau kamwe hawataki kuona Air Tanzania ikirudi.
 
dawa yao ni hii..

[HASHTAG]#foundinTanzanianotKenya[/HASHTAG]
 

Attachments

  • 1456831299165.jpg
    1456831299165.jpg
    42.5 KB · Views: 12
Hahahaha Watanzania bwana,kweli watu wa maajabu,saa nyie wenyewe mnashidwa kutangaza mali asili zenu,...hivi kweli mshawahi kusikia mtanzania yoyote anaesifia au kuzinadi mali asilia za Tanzania....,watanzania kazi yao ni majungu na kazuia wanawake wasivae wanachopenda kuvaa,,,.kwa taarifa yako hata mkata viuno "Diamond Platinamz" wanajitangazia wa kwao.,wakati nyie mnazuia kazi zake nyingine zisichzwe kwenye radio na televition za Tanzania...,,kazi yenu majungu tu,hahahahaha

Hii ni habari nimeipata kwenye Dar 24 "KUMBE DIAMOND PLATNUMZ NI MKENYA?!

Na hawa wameandika kuwa video mpya ya mwanamuziki AKA aliyomshirikisha DIAMOND PLATNUMZ kutoka KENYA imevunja rekodi kwa kutazamwa mara milioni 1 ndani ya siku kumi."


Wakenya wanatafuta kick kupitia watanzania maana duniani wanatambulika kwa kazi yao ya wizi na utapeli.
 
Ombi Muhimu:
Kwa yeyote mwenye account ya facebook ya Zuhura Kassim au Salim Kikeke wa BBC Swahili awambie wamtafute Rosemary Odinga kwa mahojiano ya presentation yake mbele ya UN kwamba amedanganya ulimwengu. Part of journalism ni kuweka ukweli wazi. Simply a naked lie.
Ni kweli Rosemary Odinga alitamka hivyo. Mimi naona hakuna haja ya kupiga kelele nyingi bali ni kulipuuza tamko hilo, maana ukweli ni kwamba Olduvai iko Tanzania na si Kenya. Ni kama ambavyo Mwl Nyerere alivyomjibu mwandishi wa habari wa Kenya alipomuuliza kuhusu dai la kwamba yeye si Mtz bali ni Mrundi kwamba mtu akikwambia kuwa mimi ni baba yako niliyekuzaa na mama yako ataandika upuuzi huo? Pia sisi watanzani tungechangamka kutangaza raslimali zetu tulizonazo. Si ajabu ukakuta Kenya wanauza Olduvai kuliko sisi. Maana kwa upande wa utalii ni kawaida kabisa kuuza attractions ambazo haziko kwenye nchi yako na ukipata watalii unawapeleka huko. Na nadhani hicho ndicho ndicho kinachofanyika kwamba Kenya wanauza sana Olduvai kama ambavyo wanauza Kilimanjaro, Zanzibar n.k. Hebu tufanye aggressive marketing na tuache kulalamika.
 
Back
Top Bottom