Madai ya Kenya kuhusu Olduvai Gorge iko Kenya

Masonara duniani wanajua kwamba ukihitaji Tanzanite ya bei nafuu ununue India au kwenye gems fairs za Hong Kong etc. Bei ya Tanzanite huko ni ndogo kuliko bei ya Arusha yenyewe na unaweza kupata rough stones kibao... tatizo si Kenya kuiba vivutio vya Tanzania ila watanzania wenyewe kuwa serious na imara katika kuzuia wizi wa raslimali ya Tanzania, na kupromote jina la Tanzania zaidi kama nchi nzuri. Kulalamika haisaidii.
 
Kara kwenye huo Mkutano inamaana kulikuwa hakuna representative wa Tanzania??Kama alikuwepo alisadiaje TAIFA lake??Nimesikia RAIS wetu na delegation yake ilikuwepo kwenye huo Mkutano,Je,na wao walimpigia Makofi huyo dada??Au walimpigia sababu ni Mtoto wa Kigogo wa Kenya?Kwanini at that Point RAIS hakupeleka pingamizi??

Sidhani kama akina Kikeke watatusaidia.Mie nadhani ni kupeleka mabango ya STOP SELLING TANZANIA kwenye Ubalozi wa KENYA.We have to stop huu ujinga,wanasiasa wetu waliopo Madarakani wako pale kwa ajili ya matumbo yao tu na si kulinda TAIFA.
Nimeipenda hii
Tujumuike wote
 
Ombi Muhimu:
Kwa yeyote mwenye account ya facebook ya Zuhura Kassim au Salim Kikeke wa BBC Swahili awambie wamtafute Rosemary Odinga kwa mahojiano ya presentation yake mbele ya UN kwamba amedanganya ulimwengu. Part of journalism ni kuweka ukweli wazi. Simply a naked lie.
Nimeshawatumia email
 
Nitamkumbuka sana Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa utawala wake pesa ilikua nje nje, sisi wafanya biashara tulikua na mahusiano mazuri na watu wa Bandari na TRA lakini kumetokea upepo mbaya umevunja kabisa mahusiano yetu yaliyokua yametukuka chini Rais wa 'WATU' I miss you JK
Hahaha pole sana
 
moja ya njia za kujitangaza kimataifa ni michezo pia lugha ya jamii husika...kenya wako vizr kwa michezo hususani riadha...niliona marathon moja wanariadha wakenya wajiongea wakiwa katikati ya mbio...mtangazaji akasema...i sure they are using kiswahili ,kenyan national language.....utaona jinsi tunavyozidiwa....wabongo hata kuongea kisw hawataki.....wakenya wakisema ni cha kwao mnalaumu....kaz ipo
 
View attachment 326295
Hiyo ni ndege ya kenya ina maandishi ya Mount Kilimanjaro, wanatumia majina ya vivutio vyetu kujitangaza duniani huku waziri wa maliasili na utalii yupo tu amekaa kimya akila pesa za umma na kuendeshwa kwenye shangingi za kifahari. Inasikitisha sana, maana watu wamepiga kelele sana ila serikali haichukui hatua yoyote. Kama waziri wa maliasili na utalii ataendelea kukaa kimya kutowachukulia hatua wakenya nitaamini ana maslahi binafsi na kenya.
Magufuli awapige marufuku Wakenya kuleta ndege zao Tanzania hadi watakapofuta hayo maneno "Mt Kilimanjaro" kwenye ndege zao!
 
Naomba msinielewe vibaya.
JF haiko kimataifa sana lakini hii movement ingekuwa ktk Tweeter na tungemention UN na agency zake zote na top leaders wa UN wote hakika hii ingeanza kufuatiliwa zaidi na huyo Mkenya kusahihisha alichodanganya lakini tukikaa kimya gvt nayo iko kimya kumbuka uongo ukisemwa sana unaweza ukaaminika yatakiwa tukanushe
Nakuunga mkono mkuu. Mimi sio mfuatiliaji mkubwa sana wa tweeter lakini hii kitu ikianzishwa nitaifuatilia hadi mwisho. I am tired of these Kenyans!
 
Jamani walisema wahenga cha kuokota hakina mwenyewe, wameona kuliko olduvai isahaulike ni bora waihamishie kenya, iendelee kuwepo kwenye historia ya Afrika, ndio yale ukiona cha nini mwenzio anasema nitakipata lini. TZ wameona hakuna haja ya kuitangaza ndio matokeo haya.
 
Ombi Muhimu:
Kwa yeyote mwenye account ya facebook ya Zuhura Kassim au Salim Kikeke wa BBC Swahili awambie wamtafute Rosemary Odinga kwa mahojiano ya presentation yake mbele ya UN kwamba amedanganya ulimwengu. Part of journalism ni kuweka ukweli wazi. Simply a naked lie.
lazima huyo rosemary odinga aabishwe kwa huu uongo wake wa kitoto. kama ndio mkakati wa nchi yao kujidai kila kitu kizuri cha tanzania kiko kenya ndio tujue ukweli. wanaifanya nchi yetu third third country kwa kuhujumu uchumi wetu sasa wanatuibia hata historia.
 
mulugo aliposema Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zimbabwe, tena katika kikao cha kimataifa, mlishitakiwa wapi????
 
Mfa maji haishi kutapatapa. Kutotangaza mali yako haimpi jirani yako haki ya kumiliki kisicho chake. Hawa jamaa wameishiwa mbinu ya kuitangaza nchi yao. Watakoma tu.
 
Binafsi sioni ubaya wa KQ kuweka neno "Mount Kilimanjaro" kwenye ndege zao. Maana kiuhalisia haiondoi ukweli kuwa Mlima upo Bongo. Sasa na sisi badala ya kukaa tu na kulalama tunatakiwa tu-launch kampeni za kutangaza vivutio vyetu ili kuwazidi kete.

Kwa mfano wao wameweka tu neno "Mount Kilimanjaro", basi sisi tunaweza kwenda mbele zaidi tukaweka neno "Mount Kilimanjaro, The Pride of Tanzania" kwenye ndege zetu "''''zinazoruka kimataifa"''''.....

"Instead of cursing the darkness light a candle..." - Ben Franklin
 
Back
Top Bottom