Magufuli inaonekana hajawahi pata shida ya dharura.Ukipata shida hata shilingi mia inakuwa na thamani kuliko elfu kumi wakati wa neema.Watu wa Kagera wanahitaji misaada.Na toka mwanzoni watu walijitolea kuwasaidia moja kwa moja wananchi matokeo yake waliokuwa wanawasaidia moja kwa moja wahanga wakapigwa stop mpaka wengine kukamatwa.Leo michango imekamilika ndo anasema waende kuwachangia wananchi.Sasa ye aliomba michango ya nini?Hivi kama serikali inauwezo wa kupunguza baadhi ya kodi kwa wananchi wa eneo hilo kulikuwa na ugumu gani?
Eti ajenge kiwanda! Huo mchakato mpaka uje uishe kweli wanakagera watakuwa na uhaba kama walio nao sasa!
Unapopata tatizo halafu huna hata wa kumsimulia jinsi tatizo lako lilivyo kibinadamu huwa inaumiza sana
Hiki ni kiburi cha wazi wazi kabisa
Masuala ya kutokuwa na shida na uongozi yanahusiana vipi na kuwasaidia wahanga wa tetemeko?Safi kabisaa,jibu murua sana.Huyo lwakatare si majuzi hapa alikua anasema eti hana shida na uongozi wa mh. Eti uko safi kabisaa.
Huyu naye anatikea huko, nahic ndugu zake pia wameathirika na hii ktu, ila kwa kwa kuwa unafiki ni huruka ya binadamu, ukichanganya na kujipendekeza ukajumlisha na uwezo mdogo wa kuchanganua mambo, ila ukirudi nyuma unagundua kuwa huyu mtu ni bendera fuata upepo anajua kabisa kuwa kilichofanywa kagera sio sawa, hapo sasa unampuuza tu.wewe sijui kama ni mzima unafikiri bei zinashushwa tuuu....
Mnafiki ni wewe faru john.Nani aliyekuambia lwakatare anataka vifaa vya ujenzi vya bure.Tofautisha kati ya punguzo la bei na bure.Kamjibu VIZURI SANA akili ya VYA BURE SI KWA ZAMA HIZI.......kwenye hili acheni UNAFIKI
Mkuu serikali inao uwezo wa kushusha bei ya hizo vitu wameomba either kwa kufuta VAT au kuweka ruzuku maalum. Nadhani shida yako ni roho mbaya kutaka wahaya wenzio wazidi kuteseka, au elimu ndogo hujui serikali inavyofanya kazi, au njaa inakufanya ujikombe kwa wenye mamlaka ili wakukomboewewe sijui kama ni mzima unafikiri bei zinashushwa tuuu....
Akili unayo hivyo jiongeze kidogo tu. Asilimia kubwa tu ya mabati yanatoka nje au kama ni ya ndani basi kuna material zinatoka nje. Wauza mabati ni watu private wanataka faida. Hilo punguzo litatolewaje, kwani jamaa wanaagiza mzigo kwa ajili ya Bukoba tu??? Too much lawama zinawapofusha.Nyie Leo hii akipunguza kodi ya hivyo vifaa mtakuwa wa kwanza kushangilia hapa jukwaani,!
Kwa hiyo maafa ya aina hiyo ikitokea bahati mbaya yatokee kwa mfano Dodoma wataambiwa nao wajenge viwanda vya vifaa vya ujenzi!
Yakitokea Rukwa, na wao wajenge.... Yakishuka kwa kishindo Geita, wajenge viwanda....!
Hivi kile kitengo cha maafa kimefutwa au bado kipo???
Mbunge wa Bukoba Wilfred Lwakatare kwenye mkutano wa Magufuli na Bukoba aliomba Bukoba wapunguziwe vifaa vya ujenzi kama bati na simenti kwa kuwa serikali haiwezi kumjengea kila mwananchi nyumba
Akitolea mfano Kikwete kuwapa fidia ya ng'ombe wafugaji waliopatwa na janga la Ukame walipewa ng'ombe na Nyerere alivyofanya kwa CDA dodoma kwa kuwapa msaada wa kodi
Magufuli alimjibu kwa kumpa changamoto ya kujenga kiwanda Kyelwa wauze mabati hata kwa 1,000 kwa sababu kuna madini ya bati Kyelwa na sio mabati ya kutoka Dar na China na ni ya wafanyabiashara.
HIVI ALIVYOKUWA ANAOMBA TUCHANGIE MADAWATI NA SISI TUNGEMJIBU KUSANYA KODI MHESHIMIWA! TUNGEKUWA TUMEKOSEA?Huyo ndio Magufuli hakopeshi.!
HIVI ALIVYOKUWA ANAOMBA TUCHANGIE MADAWATI NA SISI TUNGEMJIBU KUSANYA KODI MHESHIMIWA! TUNGEKUWA TUMEKOSEA?Huyo ndio Magufuli hakopeshi.!